OK! twende kwa hoja;kutokana
na hoja zako mimi nina mashaka na uelewa wako na unachokiandika kama
ifuatavyo;
1.Unasahau kuwa wabunge wamechaguliwa na wananchi ili kuwawakilisha
na sio cuf, sasa katika jambo lolote linalogusa maslahi ya wananchi
lililojadiliwa bungeni si la chama ni la wananchi na wabunge hao
wanatekeleza majukumu waliotumwa na wananchi na si chama kwahiyo wa
kuhoji ni wazanziibar waliowatuma sio maalim seef wala cuf kwa sababu
katiba inayotengenezwa ni ya wananchi na si ya cuf.
2.Hoja yako ya pili haina mashiko na kama ni maalim seef amekutuma
useme hivyo mwambie amelewa madaraka na anataka kuwasaliti wa zanzibar
kwa sababu hoja si kwamba, hoja hiyo imetolewa na nani au chama gani,
hoja ni kwamba hoja iliyotolea bungeni ina maslahi gani kwa
wananchi(wazanzibar) kwa hiyo hoja za chadema zilikuwa na maslahi kwa
uma ndo maana wabunge wote wa upinzani wakiwemo wa cuf waliwaunga mkono.
3.Kwa hoja ya tatu ndo aibu kabisa coz inshu ya katiba mpya
inahitaji uwakilishi mpana, yeye anasema alishirikishwa eti kwa sababu
yeye yumo ndani ya serikali sasa amesahau kuwa katiba haikuwa ni ya
serikali ni yawananchi wote na serikali haikuwa na mamlaka kisheria ya
kuingilia mchakato wa katiba mpya bali wananchi wote ndo walipaswa
washiriki kama ilivyokuwa kwa upande wa bara.
4.Kwa hoja ya nne ni kwamba kama chadema imekuwa na kauli hasi dhidi
ya hoja za wanzanzibar,je kwa hoja ambazo zinagusa maslahi ya
wazanzibar zinazo tolewa na chadema na wabunge wote wa zanzibar wakaunga
mkono kwa niaba ya wa zanzibar maalim seef anatoa wapi mamlaka ya
kupinga? sasa alitaka wapinge maslahi ya wazanzibar? inamaana adui yako
akitaka kukuokoa usiliwe na simba utakataa eti kwa sababu ni adui yako
au utamshukuru kwa kuokoa uhai wako?
5.Kwa hoja ya tano, maalim seef anataka kusema sikuhizi katiba ya
tanzania inakataza mtu au kikundi chochote kuwa na uhuru wakutoa maoni
mpaka awe mwakilishi wa kundi fulani?eti anasema misimamo ya chadema
dhidi ya waanzibar inajulikana mbona hakuitaja kama kweli anawapenda
wazanzibar?
6.Kwa hoja ya sita,inshu ya katiba mpya na wafuasi wa kisiasa ni
wapi na wapi? sasa maalim seef anataka kusema kama jambo ni la msingi
kwa maslahi ya wazanzibar hata chadema isipoungana na cuf anataka kusema
wazanzibar watakataa jambo jema kwao eti kwa sababu tu limeletwa na
chadema na kuwaunga cuf ambao wataleta jambo ambalo halina maslahi kwa
wazanzibar eti kwa sababu tu limeletwa na cuf?
NB.Wazanzibar tuwakatae viongozi kama maalim seef anaewaza maslahi yake
pekee badala ya maslahi ya wazanzibar.