Maalim Seif Atinga Washington DC na ujumbe wake

Maalim Seif Atinga Washington DC na ujumbe wake

Mwarabu kwao arabuni Na wamatumbi kwao afrika

Tatizo hampendi maendeleo mmejaa ukwetu na uAfrika wakati nchi za wengine mnapewa vingi.

Ukiambiwa kuna watu wasio Afrika walipata kuishi unakoita kwa waAfrika nako unakataa make umeshikishwa hivyo. Hii no ardhi kuna watu waliishi kabla rangi unachoita Afrika kuishimo
 
Nzuri, mpigieni makofi.Lakini ingekuwa "more factual and sensible" kama ungeandika na kutafakari baadae kama hivi:
" Mgeni aliotoka Oman 1698 akaja Zanzibar na kuzaliana sasa ndio pamekuwa kwake , na mwenyeji aliemkarabisha, ambapo Shirazi Association (1930) ndio chama cha wajukuu wa Mwinyimkuu, wao wenye nchi yao na African Association walikuja baada ya " Siti binti Saad" kuimba kwenye mapema 1900, kuwa " Zanzibar ni njema atakae aje" wanaitwa wakuja ambao wengi wao ni makuli wa bandarini kutoka bara na chimbuko la African Association"

Kisa cha kuhitalifiana Thabit Kombo wenzake Sheikh Ameoir Tajo na Moh'd Shamte ni kukubali muungano wa chama chao kiongozwe na " Mkuja" Karume, na wakaona hilo haliwezekani, wakajitoa kwenye chama cha ASP(1957) na kuunda chama chao ZPPP kilicho weza kuzaa uhuru mwaka 1963 N kutoa Waziri Mkuu wa kwanza mzawa Mo'hd Shamte.
Acheni ubaguz wakuja ndio nn kwa maneno yako unadhihirisha Cuf ni chama kilichojengwa kwa misingi ya kibaguzi ilihali zanzibar kuna wanzibar na wazanzibara. Siku Cuf wakitwaa Zanzibar kwa maneno yako ya kibaguz Unguja na Pemba zitatengana. Rudin mkamsikilize mwl. Julius Kambarage Nyerere acheni kupuuza maneno ya watu waliowazidi vision dunian hatupo sawa ndio maana yesu na Mohamad wana wafuasi kila kona ya dunia kwa hyo sio mbaya na nyie wabaguzi mnaotumia neno WAKUJA mkajifunza kwa Nyerere.

Acheni kuamini katika ubaguzi.
 
Swadakta!, nimeipenda hii ya "wakuja", mgeni aliyetoka kwao Oman akaja Zanzibar na kuzaliana, sasa ndio Zanzibar pamekuwa kwake, na mwenyeji aliyemkaribisha, ambapo ASP ndicho chama cha wajukuu wa Mwinyimkuu, wao wenye nchi yao sasa ndio wanaitwa wakuja!.

Zanzibar sio kama Marekani, wageni watasubiri sana!.
Ila pia nashukuru kumbe watu hawawajui wafadhili wakuu wa CUF, wangewajua ndipo wangejua kwa nini CUF anashinda lakini hapewi!. Endelea kujifariji kuwa wafadhili ni hawa wageni wakaazi!, lila bango la maskani Kisonge limesema ukweli japo mchungu!, ndio ukweli wenyewe!.

Pasco
 
Swadakta!, nimeipenda hii ya "wakuja", mgeni aliyetoka kwao Oman akaja Zanzibar na kuzaliana, sasa ndio Zanzibar pamekuwa kwake, na mwenyeji aliyemkaribisha, ambapo ASP ndicho chama cha wajukuu wa Mwinyimkuu, wao wenye nchi yao sasa ndio wanaitwa wakuja!.

Zanzibar sio kama Marekani, wageni watasubiri sana!.
Ila pia nashukuru kumbe watu hawawajui wafadhili wakuu wa CUF, wangewajua ndipo wangejua kwa nini CUF anashinda lakini hapewi!. Endelea kujifariji kuwa wafadhili ni hawa wageni wakaazi!, lila bango la maskani Kisonge limesema ukweli japo mchungu!, ndio ukweli wenyewe!.

Pasco
 
Ni upumbavu kuamin kua marekan ndio mkombozi wa matatizo yako ya serikali kwa sababu wao hawaji Africa kuomba ushauri au usaidizi kwa nchi yoyote juu ya matatizo yao.
Waafrica tunabaguana wenyewe kwa wenyewe kisha tunaenda kwenye nchi za magharibi kuomba back up ya ujinga wetu.
You have spoken the truth!
 
Kwa hiyo wakati wa oman walipofika zanzibar,walimkuta nami hapo kisiwani? au kulikuwa hakuna mtu? Sababu wengi wanaongelea waamiaji kutoka Oman na kutoka bara, je natives wa zanzibar ni nani??.
Hii hali ya kusema huyu kaamia mwaka flani na huyu kaja kama mtumwa ndio inawapa matatizo wa zanzibar miaka yote,kwa sababu huwezi kujenga nchi iwapo mnajiwekea matabaka!

Natives walikuwa ni wale ambao siku hizi tunawaita Wachina.
 
Maalim amechelewa saaana! halafu kibali cha kusafiri nje ya nchi katoa wapi?
 
Oman walikuja Zanzibar kwa minajili ya kuuondosha utawala wa mabavu na wa kikafiri wa kireno uliodumu takriban kuanzia 1503 - 1698. Kipindi chote na tarehe hizo walikuwepo watu wanaishi visiwa hivi wanaokuja kujuulikana kama wazanzibari.

Lakini hata kabla kuja Mreno kuvivamia visiwa hivi kulikuwa na utawala wa kijadi/kimila, uliokuwa unaongozwa na Malkia Mwana wa mwana, Mtumbatu na mumewe Mwarabu wa Yemen, na makazi yao yalikuwa ilipo Ngome Kongwe.

Walipovamia Wareno kuumaliza utawala wake, Mwana wa mwana alikimbilia Yemen pamoja na mumewe , na akaishi uhai wake wote.

Uislam Zanzibar ulianza karne ya nane ( 8th Century) na kila mtu alikuwa muumini wa dini hiyo. Watu waliotokana na kizazi hiki, pamoja na mimi ndio tunajinasibu na kujiita Washirazi wa Zanzibar na ndio wazawa. Ukiwa si mshirazi, haijalishi uwe mweupe, mweusi, unamachale na sio muislamu , wewe unakuwa ni wakuja tu
Wee bulushi mbaguzi Balagashi hapo ndipo unapofanya makosa na ni makosa kama haya ndiyo yanayopelekea hata mshinde vipi, kamwe hamtakabidhiwa nchi mpaka pale mtakapokubali kuwa Zanzibar ina wenyewe, nyinyi mlikaribishwa tuu na baada ya kuzaliana nyote sasa ni Wanzanzibar wanaopaswa kuwa sawa na sio wengine kujiona bora zaidi kwa sababu ya ubulushi au uchotara wao hivyo kujisikia karibu zaidi na Mwarabu ilihali wenye Zanzibar yao wale wa asili kabisa ya Mwinyi Mkuu wangalipo wapo!.

Umeanza vyema uliposema "walikuwepo watu wanaishi visiwa hivi wanaokuja kujuulikana kama wazanzibari", japo husemi watu hawa ni kina nani, sasa hawa ndio hao wenye Zanzibar yao!.

Ni kweli "Oman walikuja Zanzibar kwa minajili ya kuuondosha utawala wa mabavu na wa kikafiri wa kireno", ila hawakujijia tuu, walikaribishwa au waliombwa na wenyeji chini ya Mwinyi Mkuu!. Jee unajua Waomani hawa baada ya kukaribishwa kuwasaidia wenyeji kuwatimua Wareno, hao Waomani waliwafanya nini wenyeji kisha kutawala wao?!. Jee unakijua nini kiliwakuta wajukuu wa Mwinyi Mkuu walipotaka haki yao toka kwa Waomani waliowakaribisha?!.

Jee unajua Mtumbatu Malikia Mwana wa Mwana aliupataje umalkia na ni nini kilimkimbiza Malikia Mwana wa Mwana hadi kwenda kufia Yemen?!.

Mtu wa mwanzo kuandika historia ya Zanzibar ni Ibin Batuta, na hakuandika ya Zanzibar tuu bali hata ya Kilwa nabaadaye mwandishi mwingine Al-Mutahar bin Tahir al Makdisi, ambapo Mshirazi Sultani Hassan bin Ali alikinunua kisiwa cha Kilwa toka kwa Hasan Bin Amiri kwa gharama ya kitambaa cha kuzunguka Kilwa yote!. Sultan Seyyid Said alilipa nini kukimiliki kisiwa cha Zanzibar na Pemba toka ukoo wa Mwinyimkuu?!.

Bila aibu, haya wala soni, unaona sifa kujinasibu na ubaguzi wa "Washirazi wa Zanzibar na ndio wazawa. Ukiwa si mshirazi, haijalishi uwe mweupe, mweusi, unamachale na sio muislamu , wewe unakuwa ni wakuja tu!", Nguvu ya ASP sio Washirazi ni ile herufi ya kwanza ya Afro!. Mwanzo walipokuwepo Shiraz Association si walishindwa!, hata Afican Association pia walishindwa, hata baada ya African Association na Shiraz Association kuungana kuunda ASP ambao ndio walikuwa the majority, bado hawakupewa!, wakaona huu ni ujinga, ndipo January 1964 wakaamua kutwaa kwa yale Mapinduzi Matukufu!, sasa baada ya hayo kweli kuna mtu mwenye akili zake timamu atathubutu kuwaita wenye nchi yao wakuja?!. Kwa kauli za kibaguzi kama hizi, kiukweli mtasubiri sana!, sasa ndio nimeanza kuelewa mantiki ya lile bango la Maskani Kisonge!, kuna watu wanatia hasira sana! na labda ndio sababu Magufuli kajikalia pembeni!.

Pasco
 
Leo macho na masikio yetu ni nchini Marekani majira ya 10:00 am hadi saa 11:30 saa za huko, Maalim atamwaga nondo!

The main area of concentration ni solution ya huo mgogoro wa kubuniwa na CUF na wamarekani wao!, uchaguzi wa Zanzibar ulifanyika, matokeo yakafutwa kinyume cha sheria lakini hakuna yoyote aliyepinga rasmi!.
Uchaguzi wa marudio ukaitishwa rasmi na hakuna yoyote aliyepinga rasmi, bali kuna watu walisusa!.
Uchaguzi ukarudiwa kwa huru na haki na matokeo yakatangazwa rasmi aliyeshinda kashinda na kaapishwa, sasa ni rais halali wa Zanzibar!, na uchaguzi umemalizika, uchaguzi mwingine ni 2020!.

Uwongo ukiachwa kutamalaki bila kukanushwa hugeuka ndio ukweli wenyewe, vivyo hivyo haramu ikiachwa kutamalaki, hugeuka ndio halali yeyewe, japo ni kweli kufutwa kwa uchaguzi wa October kulikuwa ni haramu, lakini kwa vile hakuna yoyote aliyepinga rasmi haramu ile, kutokupinga huko, kumeihalalisha haramu ile kugauka halali!, hivyo Dr, Shein amechaguliwa kwenye uchaguzi halali huru na wa haki hivyo ni rais halali!. Ikumbukwe ni haramu tuu ikiachwa ndio huweza kugeuka halali lakini kamwe halali haiwezi kugeuka haramu!.

Ruksa kujifaiji kuwahutubia Wamarekani na dunia isikie bali no one can do anything hadi 2020!.

Ngoja tusikie!.

Pasco
 
Uzi za vijana wa Ufipani zimenichosha yule kaenda kufuturu.Kwani hamjui katiba ya Tz kuhusu matokeo ya uchaguzi
 
Tatizo hampendi maendeleo mmejaa ukwetu na uAfrika wakati nchi za wengine mnapewa vingi.

Ukiambiwa kuna watu wasio Afrika walipata kuishi unakoita kwa waAfrika nako unakataa make umeshikishwa hivyo. Hii no ardhi kuna watu waliishi kabla rangi unachoita Afrika kuishimo

Mmatumbi anatoka kilwa, Tanzania - Africa this is a fact upende usipende, Mwarabu kwao we unakujua na hakuna mmatumbi atakaye jinasibu kwao Oman hata kama alizaliwa huko. Kupata kuishi bado hakuja futa ukweli huu.
 
Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na ujumbe wake leo amewasili mjini Washington DC kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi nchini Marekani. Ziara hiyo itaanza rasmi J...umatatu, tarehe 13 Juni kwa kushiriki mkutano ulioandaliwa na Centre for Strategic and International Studies (CSIS) kujadili matokeo na matukio ya uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na nini unapaswa kuwa mwelekeo baada ya ubakaji wa demokrasia uliofanywa kule Zanziabr. View attachment 355971 View attachment 355972
 
Mpuuzi mkubwa karne ya 7 mpaka 9 Ibun Batuta anasimulia kuhusu kuwapo kwa Himaya ya Zenj ikiwa na maana Himaya ya mtu mweusi. Kama hao wakuja wa 1600 walifanya hila dhidi ya wenyeji.
Wanahistoria husoma kitu kinachoitwa Historiography Hili somo humuwezesha mwanahistoria kuwa makini wakati akipita maandiko mbalimbali ya wanahistoria na kuangalia jinsi maandishi yao yalivyoathiriwa na mitazamo yao ya kisiasa, kijamii, na kundi la kiuwezo wa kiuchumi alilimo mwandishi. Mambo hayo yanamchango mkubwa sana kwa mwandishi kufanya tafasiri ya tukio.
Hivyo si kila mwanahistoria aliyeandika anasifa ya kufanyiwarejea kibubusa. Vitabu vingine unachukua kisa na wahusika tu tafasili ya kisa unaenda kupata kutoka kwenye vyanzo vingine. Rai yangu usituijie na maeleze ya wajinga wakijitetea kwa wake zao au ndugu zao juu ya mambo ya kisiasa na kutwambia ndio ushahidi wa kihistoria.
Ni vizuri kuwa na mathinker kama ninyi hapa JF maana wengi wameshalewa na mihemko ya vyama wameacha akili zao zitawaliwe na kina JK, Mbowe na Seif kama huyu unayejibizana naye. Sitashangaa akianza kuwaita weusi walio kuwa wazawa ni makafiri ndiyo maana hii damu ya waarabu haitaacha unafiki wana mali lakini kwaajili ya unafiki wao wanauana wenyewe kwa wenyewe huko mashariki ya kati.
 
Busara na hekma vinayaongoza maisha yake yote. Mungu ambariki afanikiwe.
 
hata baada ya African Association na Shiraz Association kuungana kuunda ASP ambao ndio walikuwa the majority, bado hawakupewa!,
Pasco usijifanye kalumekenge, unajua kuwa " rules of the game must be obeyed" Uchaguzi wa Zanzibar mshindi alikuwa akipimwa wa wingi wa viti na sio wingi wa mamluki.

Mamluki kutoka bara walishindwa kujipenyeza katika majimbo yaliokuwa yanakaliwa na wazawa, sasa ikawalazimu wote wajikusanye pamoja kama tonge kwenye majimbo yaliokuwa na yanakaliwa na" wakuja", vibarua, makuli na wahalifu. Maeneo hayo mpaka leo ndio ngome ya CCM na kila " mkuja" mpya anaekuja mpaka sasa anakimbilia huko huko.

Siti binti Saad amenituponza alipoimba " Zanzibar ni njema atakae aje" bahati mbaya wamekuja kwa makundi kutoka kila pahali, Uganda, , msumbiji, Malawi,Kenya, kumbe kuleta fujo.

C:\DOCUME~1\ib\LOCALS~1\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg


Mwenye akili zake timamu atathubutu kuwaita wenye nchi yao (John Okello and assassins),hapo juu wakuja?!!!!!. ( Pasco)

Nimekuvulia kofia, lakini chinichini una nifurahisha kuwa ndani ya nafsi yako unamjua mzawa na " mkuja" ni nani
 
Kumbe zile fujo zake zimeorijinet huko?
 
Back
Top Bottom