Oman walikuja Zanzibar kwa minajili ya kuuondosha utawala wa mabavu na wa kikafiri wa kireno uliodumu takriban kuanzia 1503 - 1698. Kipindi chote na tarehe hizo walikuwepo watu wanaishi visiwa hivi wanaokuja kujuulikana kama wazanzibari.
Lakini hata kabla kuja Mreno kuvivamia visiwa hivi kulikuwa na utawala wa kijadi/kimila, uliokuwa unaongozwa na Malkia Mwana wa mwana, Mtumbatu na mumewe Mwarabu wa Yemen, na makazi yao yalikuwa ilipo Ngome Kongwe.
Walipovamia Wareno kuumaliza utawala wake, Mwana wa mwana alikimbilia Yemen pamoja na mumewe , na akaishi uhai wake wote.
Uislam Zanzibar ulianza karne ya nane ( 8th Century) na kila mtu alikuwa muumini wa dini hiyo. Watu waliotokana na kizazi hiki, pamoja na mimi ndio tunajinasibu na kujiita Washirazi wa Zanzibar na ndio wazawa. Ukiwa si mshirazi, haijalishi uwe mweupe, mweusi, unamachale na sio muislamu , wewe unakuwa ni wakuja tu