Mbowe kama Mandela, Maalim Seif na Mwalimu Nyerere

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
7,171
10,705
Kuhusu Mbowe, Mandela, Nyerere na Maalim Seif...

Mlisoma kitabu cha Nelson Mandela cha The Long Walk to Freedom, kiongozi huyo wa zamani wa ANC na baadaye Afrika Kusini anasema wakati alipoanza mazungumzo ya faragha ya kusaka maridhiano na serikali ya makaburu wakati akiwa jela, wenzake ndani ya ANC walianza kumtuhumu kwa kununuliwa hata ikafika hatua wakamuona ni sell out.

Anasema hakukata tamaa, alisonga mbele hadi mwisho akaachiwa huru na wenzake pia wakaachiwa na ilichukua muda mrefu sana kumuelewa.

Hivi ndivyo ilivyo leo kwa Freeman Aikaeli Mbowe. Wenzake wamekaza shingo hawataki kabisa kumuelewa.

Kama ilivyokua kwa Mandela kwanza na Pieter Willem Botha (Pik Botha) na baadaye F. W. De Klerk, ndivyo ambavyo leo Mbowe anatuhumiwa kununuliwa na Samia na sasa anahusishwa hadi na kile kinachoitwa fedha za Abdul.

Kama ilivyokuwa kwa Mandela, Mwenyekiti Mbowe anao wajibu wa kulitolea maelezo ya kifikra na si kimapambano suala hili ili kubadili si tu hizo tuhuma dhidi yake bali kulielimisha taifa kwamba, katika mapambano ya kupigania demokrasia, utawala bora, uongozi na haki, kunahitajika maarifa makubwa na hekima kuliko hisia, na harakati zisizo na tija.

Zipo rejea za kutosha kihistori- za kitaifa na kimataifa za kuwapa darasa watu wasiojua mzigo mkubwa wa dhamana wanaoubeba viongozi wanaoongoza mapambano ya kudai mabadiliko wa aina ya Mbowe.

Huwezi ukawa Mwenyekiti wa Taifa wa chama kikubwa cha upinzani ambaye wewe mwenyewe na watu wako, mnatendewa vitendo vya hiyana, mateso, kupotea, kuuawa na uonevu wa kila namna halafu ukang’ang’ania njia moja tu ya kupiga mdomo na kufokafoka majukwaani na ukaacha kutumia fursa ya kujadiliana na Rais au taasisi zenye mamlaka ya kidola kama njia na namna ya kufikiwa kwa muafaka wa kitaifa.

Ukimwacha Mandela tunayo mifano mikuu miwili hapa nchini pia ya namna hiyo wa kwanza ukiwa ni ule wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwanza wakati wa kudai uhuru alipolazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kuanza mazungumzo na gavana wa kikoloni ambaye serikali yake ilishakitangaza chama cha TANU kuwa taasisi ya kihalifu.

Nyerere huyo huyo alifanya hivyo pia wakati taifa lilipokubali kuanza kwa mfumo wa vyama vingi alipokutana kwa nyakati mbili tofauti na viongozi wa vyama viwili vikuu vya upinzani vya NCCR Mageuzi na CUF wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1995.

Mfano mwingine ni ule wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF na mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad aliyefikia hatua kama hii ya sasa ya Mbowe ya kuzomewa hadharani na wafuasi wake na hata wapenda mabadiliko Zanzibar alipoanza kufanya mazungumzo na hasimu wake mkubwa, aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume hata kukapatikana mwafaka na maridhiano yaliyozaa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

Leo hii, Mandela, Nyerere na Maalim Seif wanaimbwa kila mmoja kwa namna yake kwa sababu ya kuwaongoza watu wao ambao wakati fulani waliwatusi na kuwakejeli.

Hivi ndivyo itakavyokuja kuwa huko tuendako ambako, Mbowe anayedhihakiwa leo na kukejeliwa atakapokuja kueleweka na kubebeshwa kila aina ya sifa ya kuwa kiongozi mwenye maono.
 
Mwenye akili ndogo hawez kukuelewa hasa hawa watz ambao wamekuwa mashabiki wa Simba na yanga na wanadhan hata maisha pia unaweza yaletea ushabiki
 
Back
Top Bottom