Chiwaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 5,725
- 3,795
Ili mradi mkono uende kinywani.Maalim Seif anafanya siasa za kisasa sana !
Ili mradi mkono uende kinywani.Maalim Seif anafanya siasa za kisasa sana !
usipotoshe umma. wakati ASP ikitetea maslahi ya mzanzibar mnyonge, ZPPP ilikuwa ikitetea maslahi ya waarabu wachache kutoka Oman, na kile kikundi cha wachache kikapewa uhuru Dec 1963, na baadae kupinduliwa na wanyonge kwa maslahi ya wote ASP na Karume akawa RaisNzuri, mpigieni makofi.Lakini ingekuwa "more factual and sensible" kama ungeandika na kutafakari baadae kama hivi:
" Mgeni aliotoka Oman 1698 akaja Zanzibar na kuzaliana sasa ndio pamekuwa kwake , na mwenyeji aliemkarabisha, ambapo Shirazi Association (1930) ndio chama cha wajukuu wa Mwinyimkuu, wao wenye nchi yao na African Association walikuja baada ya " Siti binti Saad" kuimba kwenye mapema 1900, kuwa " Zanzibar ni njema atakae aje" wanaitwa wakuja ambao wengi wao ni makuli wa bandarini kutoka bara na chimbuko la African Association"
Kisa cha kuhitalifiana Thabit Kombo wenzake Sheikh Ameoir Tajo na Moh'd Shamte ni kukubali muungano wa chama chao kiongozwe na " Mkuja" Karume, na wakaona hilo haliwezekani, wakajitoa kwenye chama cha ASP(1957) na kuunda chama chao ZPPP kilicho weza kuzaa uhuru mwaka 1963 N kutoa Waziri Mkuu wa kwanza mzawa Mo'hd Shamte.
Sura zote tatu za mtu mnafiki umezionesha Pasco. Hata kama utajipanga rangi tofauti utabakia kinyonga tu.japo ni kweli kufutwa kwa uchaguzi wa October kulikuwa ni haramu, lakini kwa vile hakuna yoyote aliyepinga rasmi haramu ile, kutokupinga huko, kumeihalalisha haramu ile kugauka halali!,
Kwanza kwenu wapi? tusihangaishaene. Unajua walioanzisha ASP na unawajua walioanzisha ZPPP?usipotoshe umma. wakati ASP ikitetea maslahi ya mzanzibar mnyonge, ZPPP ilikuwa ikitetea maslahi ya waarabu wachache kutoka Oman, na kile kikundi cha wachache kikapewa uhuru Dec 1963, na baadae kupinduliwa na wanyonge kwa maslahi ya wote ASP na Karume akawa Rais
Mzanzibari mnyonge 1963 , leo amezidi kuwa mnyonge marudufu. Yeye alipokwenda shule alikuwa anakaa kwenye dawati,maziwa kila siku wakati wa mapumziko, shida ilikua kutafuta kuni tu, health care inafuata mashuleni, michezo ( vifaa), vyoo vya kutosheleza, vifaa vya kuandikia nakusomea kedekede na vyote bure na bila mchango wowote. Leo imekuwa hadithi ya kusimulia wajukuu na watoto.ASP ikitetea maslahi ya mzanzibar mnyonge
Unaelewa kiswahili vizuri, soma hii tena "ASP klimeguka baada ya wazawa kutoridhishwa na uvamizi wa " wakuja". Sasa utasemaje agenda ya ZPPP hazikuwa na maslahi na Zanzibar wangejimegua na ASPajenda ya ZPPP hazikuwa na maslai mapana kwa taifa la Zanzibar
Lowassa hakushinda uchaguzi ndiyo maana amenyamaza.Hizi kasoro za,uchaguzi hazikufanyika Zanzibar peke yake hata huku bara vipi Lowassa mbona umekuwa kimya hivyo?
Kaburini?mkajifunze kwa Nyerere.
Mamluki kutoka bara walishindwa kujipenyeza katika majimbo yaliokuwa yanakaliwa na wazawa, sasa ikawalazimu wote wajikusanye pamoja kama tonge kwenye majimbo yaliokuwa na yanakaliwa na" wakuja", vibarua, makuli na wahalifu. Maeneo hayo mpaka leo ndio ngome ya CCM na kila " mkuja" mpya anaekuja mpaka sasa anakimbilia huko huko.
Nina heshimu na mtazamo wako mkuu na kwa hilo nakushukuru. Ila umeghafilika kueleza mchango wa " mamluki" katika chaguzi zote za Zanzibar ni donda ndugu na ndio linalotupeleka pabaya na kupelekea dhana ya kibaguzi ya wazawa na wakuja.Ina uma sana mtu aliezaliwa Zanzibar lakini anakoseshwa haki ya kitambulisho cha kuweza kupiga kura na wakuja anakuja Zanzibar mwezi mmoja anapata shahada ya kupiga kura kwa sababu atapigia chama fulani. Nisaidie msamiati sanifu wa kuelezea hali hii na ifahamikeMkuu Baragash, maelezo yako yanaweza kuwa ya ukweli kutokana na itikadi uliyonayo kuhusu unavyotamani Zanzibar iwe. Kuna mchanganyiko wa maelezo ambayo yapo halali kihistoria, lakini pia, unachomekea mambo mengi yanayokuza itikadi yako " ya kuendeleza ubaguzi". Maneno yako hapo juu, ni maneno yanayoendeleza chuki na kutokutoa mwelekeo wa kutatua tatizo la Zanzibar. Kama wewe ni mmoja wa wasemaji wakuu wa hilo kundi linaloendeleza huo ubaguzi,waambie wenzio kuwa mwaiangamiza Zanzibar. Mnahitaji kutulia, na kutatua matatizo ya Zanzibar kwa kutokuendelea kubaguana.
Kwa maelezo yako, pamoja na maelezo ya Pasco, inaonyesha kuwa Zanzibar kuna tatizo kubwa la watu kubaguana na pia zinatumika mbinu mablimbali kutaka kutatua tatizo hilo bila kuangalia "root causes" za tatizo. Mbinu za kutumia "mamaluki" kwa mfano, ni njia nzuri kwa kundi moja na mbaya kwa kundi jingine, kama ulivyoeleza katika post yako na litaendeleza mgogoro. kwa watu kama wewe ambao wamaeyaona hayo, ni kuyaweka wazi kwa umma( kama unavyofanya hapa), na kutafuta njia zisizo za kibaguzi katika kutatua suala hili. Ni tatizo lililodumu kwa miaka mingi sana ( kama ulivyoeleza historia yake...ofcourse mimi sijui sana kama hiyo historia ni sahihi) , lakini halijafikia kuwa sugu kama tatizo la wapalestina na waisrael. Hili la kwetu, linaweza tatulika kwa upendo , bila chuki au umwagaji wa damu.Ina uma sana mtu aliezaliwa Zanzibar lakini anakoseshwa haki ya kitambulisho cha kuweza kupiga kura na wakuja anakuja Zanzibar mwezi mmoja anapata shahada ya kupiga kura kwa sababu atapigia chama fulani.
....Wapemba walinunuliwa na waarabu wakaambiwa wao ni karibu na mwarabu ! Ndio maana Pemba nzima bado kasumba inawasumbua !Unaelewa kiswahili vizuri, soma hii tena "ASP klimeguka baada ya wazawa kutoridhishwa na uvamizi wa " wakuja". Sasa utasemaje agenda ya ZPPP hazikuwa na maslahi na Zanzibar wangejimegua na ASP
1. INASTAABISHA, mtu mwenye sifa, maarifa, na mdadisi kama wewe mpaka leo humjui mfadhili wa CUF.
Mfadhili mkuu wa CUF ni wazanzibari wazawa, walioikataa ASP siku ya Ameir Tajo na Moh'd Shamte walipojiengua na chama hicho na kuunda ZPPP.
Waliikataa ASP kwasababu ya sera zake za kuwakumbatia "wakuja" na wataendelea kuikataa ASP ( CCM) hata itawale mfululizo kwa miaka hata 200 kama walivyotawala wareno, lakini haitaweza kuzibadilisha nyoyo za wazanzibari khusu kisiwa chao.
2. Kulikopelekea ishinde vipi hakuna kupewa: Kuna mtawala mwengine alioitia Zanzibar kwapani. Pamoja na kuwatumia wazanzibara na kutumia umwamba wake wa kubeba rocket launchers mabegani, na vifarui mitaani wakati wa kampeni na uchaguzi havikuweza kuteteresha imani ya wazanzibari wazawa juu ya chama na viongozi wanaowataka.
Mtawala huyu anaringia uwezo wa kijeshi wa (45:1) na Zanzibar inaringia uzalendo uliotukuka, ujasiri na ustahamilivu na uchamungu wa wazanzibari!