Maalim Seif Atinga Washington DC na ujumbe wake

Maalim Seif Atinga Washington DC na ujumbe wake

5525

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
5,428
Reaction score
6,343
Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na ujumbe wake leo amewasili mjini Washington DC kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi nchini Marekani.
Ziara hiyo itaanza rasmi J...umatatu, tarehe 13 Juni kwa kushiriki mkutano ulioandaliwa na Centre for Strategic and International Studies (CSIS) kujadili matokeo na matukio ya uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na nini unapaswa kuwa mwelekeo baada ya ubakaji wa demokrasia uliofanywa kule Zanziabr.

13435501_912139728894375_6476165601227691260_n.jpg

13445444_1171014726265879_4722904844815866106_n.jpg
 
Attachments

  • 13435501_912139728894375_6476165601227691260_n.jpg
    13435501_912139728894375_6476165601227691260_n.jpg
    15.6 KB · Views: 119
Hii ni ziara muhimu sana!, kwa vile MCC wametunyima zile fedha kwa sababu ya kadhia ya uchaguzi huru na wa haki wa marudio Zanzibar, kulikopelekea CUF kuwekwa kando ndani ya SUK,

Then Wamarekani ni watu muhimu sana haswa kufuatia lile andiko la Balozi wao aliyekuwa Zanzibar ile 1964, hivyo angalau sasa CUF inaibua uwezekano wa kufadhiliwa na fedha za MCC, hivyo 2020 CUF ikishinda itapewa!.

Miaka yote ya nyuma CUF inashinda na haipewi kufuatia taarifa za kiiteligensia za mfadhili mkuu wa CUF ni nani, kulikopelekea hata CUF ishinde vipi hakuna kupewa kufuatia hofu ya "he who pays the piper!", Wamarekani hatuna matatizo nao!, sio wale ...

Hivyo ziara hii ni muhimu sana, ila uchaguzi mwingine ni mpaka 2020 kwa sababu no one can do anything now!.

Pasco
 
mfadhili mkuu wa CUF ni nani, kulikopelekea hata CUF ishinde vipi hakuna kupewa
1. INASTAABISHA, mtu mwenye sifa, maarifa, na mdadisi kama wewe mpaka leo humjui mfadhili wa CUF.

Mfadhili mkuu wa CUF ni wazanzibari wazawa, walioikataa ASP siku ya Ameir Tajo na Moh'd Shamte walipojiengua na chama hicho na kuunda ZPPP.

Waliikataa ASP kwasababu ya sera zake za kuwakumbatia "wakuja" na wataendelea kuikataa ASP ( CCM) hata itawale mfululizo kwa miaka hata 200 kama walivyotawala wareno, lakini haitaweza kuzibadilisha nyoyo za wazanzibari khusu kisiwa chao.

2. Kulikopelekea ishinde vipi hakuna kupewa: Kuna mtawala mwengine alioitia Zanzibar kwapani. Pamoja na kuwatumia wazanzibara na kutumia umwamba wake wa kubeba rocket launchers mabegani, na vifarui mitaani wakati wa kampeni na uchaguzi havikuweza kuteteresha imani ya wazanzibari wazawa juu ya chama na viongozi wanaowataka.

Mtawala huyu anaringia uwezo wa kijeshi wa (45:1) na Zanzibar inaringia uzalendo uliotukuka, ujasiri na ustahamilivu na uchamungu wa wazanzibari!
 
1. INASTAABISHA, mtu mwenye sifa, maarifa, na mdadisi kama wewe mpaka leo humjui mfadhili wa CUF. Mfadhili mkuu wa CUF ni wazanzibari wazawa, walioikataa ASP siku ya Ameir Tajo na Moh'd Shamte walipojiengua na chama hicho na kuunda ZPPP. Waliikataa ASP kwasababu ya sera zake za kuwakumbatia "wakuja" na wataendelea kuikataa ASP ( CCM) hata itawale mfululizo kwa miaka hata 200 kama walivyotawala wareno, lakini haitaweza kuzibadilisha nyoyo za wazanzibari khusu kisiwa chao.
2. Kulikopelekea ishinde vipi hakuna kupewa: Kuna mtawala mwengine alioitia Zanzibar kwapani. Pamoja na kuwatumia wazanzibara na kutumia umwamba wake wa kubeba rocket launchers mabegani, na vifarui mitaani wakati wa kampeni na uchaguzi havikuweza kuteteresha imani ya wazanzibari wazawa juu ya chama na viongozi wanaowataka. Mtawala huyu anaringia uwezo wa kijeshi wa (45:1) na Zanzibar inaringia uzalendo uliotukuka, ujasiri na ustahamilivu na uchamungu wa wazanzibari!
Swadakta!, nimeipenda hii ya "wakuja", mgeni aliyetoka kwao Oman akaja Zanzibar na kuzaliana, sasa ndio Zanzibar pamekuwa kwake, na mwenyeji aliyemkaribisha, ambapo ASP ndicho chama cha wajukuu wa Mwinyimkuu, wao wenye nchi yao sasa ndio wanaitwa wakuja!.

Zanzibar sio kama Marekani, wageni watasubiri sana!.
Ila pia nashukuru kumbe watu hawawajui wafadhili wakuu wa CUF, wangewajua ndipo wangejua kwa nini CUF anashinda lakini hapewi!. Endelea kujifariji kuwa wafadhili ni hawa wageni wakaazi!, lila bango la maskani Kisonge limesema ukweli japo mchungu!, ndio ukweli wenyewe!.

Pasco
 
Zitto naye awasiliane kwa njia ya tele conferencing kuhusu ishu yake
 
Swadakta!, nimeipenda hii ya "wakuja", mgeni aliyetoka kwao Oman akaja Zanzibar na kuzaliana, sasa ndio Zanzibar pamekuwa kwake, na mwenyeji aliyemkaribisha, ambapo ASP ndicho chama cha wajukuu wa Mwinyimkuu, wao wenye nchi yao sasa ndio wanaitwa wakuja!.

Zanzibar sio kama Marekani, wageni watasubiri sana!.
Ila pia nashukuru kumbe watu hawawajui wafadhili wakuu wa CUF, wangewajua ndipo wangejua kwa nini CUF anashinda lakini hapewi!. Endelea kujifariji kuwa wafadhili ni hawa wageni wakaazi!, lila bango la maskani Kisonge limesema ukweli japo mchungu!, ndio ukweli wenyewe!.

Pasco
Pasco bana! Umewatwanga penyewe
 
mgeni aliyetoka kwao Oman akaja Zanzibar na kuzaliana, sasa ndio Zanzibar pamekuwa kwake, na mwenyeji aliyemkaribisha, ambapo ASP ndicho chama cha wajukuu wa Mwinyimkuu, wao wenye nchi yao sasa ndio wanaitwa wakuja!.
Nzuri, mpigieni makofi.Lakini ingekuwa "more factual and sensible" kama ungeandika na kutafakari baadae kama hivi:
" Mgeni aliotoka Oman 1698 akaja Zanzibar na kuzaliana sasa ndio pamekuwa kwake , na mwenyeji aliemkarabisha, ambapo Shirazi Association (1930) ndio chama cha wajukuu wa Mwinyimkuu, wao wenye nchi yao na African Association walikuja baada ya " Siti binti Saad" kuimba kwenye mapema 1900, kuwa " Zanzibar ni njema atakae aje" wanaitwa wakuja ambao wengi wao ni makuli wa bandarini kutoka bara na chimbuko la African Association"

Kisa cha kuhitalifiana Thabit Kombo wenzake Sheikh Ameoir Tajo na Moh'd Shamte ni kukubali muungano wa chama chao kiongozwe na " Mkuja" Karume, na wakaona hilo haliwezekani, wakajitoa kwenye chama cha ASP(1957) na kuunda chama chao ZPPP kilicho weza kuzaa uhuru mwaka 1963 N kutoa Waziri Mkuu wa kwanza mzawa Mo'hd Shamte.
 
Kwa hiyo wakati wa oman walipofika zanzibar,walimkuta nami hapo kisiwani? au kulikuwa hakuna mtu? Sababu wengi wanaongelea waamiaji kutoka Oman na kutoka bara, je natives wa zanzibar ni nani??.
Hii hali ya kusema huyu kaamia mwaka flani na huyu kaja kama mtumwa ndio inawapa matatizo wa zanzibar miaka yote,kwa sababu huwezi kujenga nchi iwapo mnajiwekea matabaka!
 
1. INASTAABISHA, mtu mwenye sifa, maarifa, na mdadisi kama wewe mpaka leo humjui mfadhili wa CUF. Mfadhili mkuu wa CUF ni wazanzibari wazawa, walioikataa ASP siku ya Ameir Tajo na Moh'd Shamte walipojiengua na chama hicho na kuunda ZPPP. Waliikataa ASP kwasababu ya sera zake za kuwakumbatia "wakuja" na wataendelea kuikataa ASP ( CCM) hata itawale mfululizo kwa miaka hata 200 kama walivyotawala wareno, lakini haitaweza kuzibadilisha nyoyo za wazanzibari khusu kisiwa chao.
2. Kulikopelekea ishinde vipi hakuna kupewa: Kuna mtawala mwengine alioitia Zanzibar kwapani. Pamoja na kuwatumia wazanzibara na kutumia umwamba wake wa kubeba rocket launchers mabegani, na vifarui mitaani wakati wa kampeni na uchaguzi havikuweza kuteteresha imani ya wazanzibari wazawa juu ya chama na viongozi wanaowataka. Mtawala huyu anaringia uwezo wa kijeshi wa (45:1) na Zanzibar inaringia uzalendo uliotukuka, ujasiri na ustahamilivu na uchamungu wa wazanzibari!
Hivi wewe burushi kwa akili zako Mtu mweusi kutoka pwani ya Afrika mashariki alizuiwa na nani kuweka makazi katika visiwa vya pemba na Unguja mpaka akasubiri kuja kwa waarabu ndipo kwenda kuishi visiwani humo?
Jina lenyewe uhalisia wake ni nchi ya watu weusi Zenj. Bila aibu weusi unawaita wakuja na jamii ya kina seif na Jusa ndio wanaitwa wenyeji. Angalia sana haya uyaandikayo hayana tija kabisa na yanaibua hisia.
Zanzibar ni ya yeyote aliyeamua kuweka makazi yake huko na kufuata sheria na taratibu za nchi ya zanzibar awe mweupe au mweusi. Nilisikitika sana kusikia kauli zikisema warabu au washirazi waondoke, nashukuru chama husika kilitoa kanusho. Wewe je nani atakanusha huu upuuzi unaoutapika humu.
Acha siasa za kipumbavu za kubaguana. Rudi kasome kitabu Nyota ya Rehema huenda ikausuuza moyo wako utokane na hii shombo ya ubaguzi uliyokuzwa nayo.
 
Mi siioni mantiki ya kukomalia "u-kuja na uzawa" ikiwa Zanzibar ni Nchi huru na kwa umoja wao wamekubali na kuruhusu democrasia itamalaki kama nyanja kuu ya kubadilishana madaraka na uongozi wa nchi.
Let democracy prevail.
Maamzi ya wananchi yaheshimiwe na vyombo vya dora visimamie amani pasipo mlengo wowote. Huko ndo kukomaa kisiasa na kustaarabika kwa wakaazi wa visiwa vya Zanzibar.
Kiini kikuu cha migogoro yote inayoendelea visiwani ni muungano wa Tanzania. Laiti kama Jamhuri ya Watu wa Zanzibar isingekuwa kwenye huu muungano, haya yote tusingeyasikia.
 
Haa kweli, baada kushindwa anaenda kuwaambia CSIS lmsaidie kuendeleza vurugu kama kule Iraq na Syria.
Ningemwelewa kama anaenda kupata matibabu mazuri zaidi badala ya yale ya India
 
Kwa hiyo wakati wa oman walipofika zanzibar,walimkuta nami hapo kisiwani? au kulikuwa hakuna mtu? Sababu wengi wanaongelea waamiaji kutoka Oman na kutoka bara, je natives wa zanzibar ni nani??.
Hii hali ya kusema huyu kaamia mwaka flani na huyu kaja kama mtumwa ndio inawapa matatizo wa zanzibar miaka yote,kwa sababu huwezi kujenga nchi iwapo mnajiwekea matabaka!
Oman walikuja Zanzibar kwa minajili ya kuuondosha utawala wa mabavu na wa kikafiri wa kireno uliodumu takriban kuanzia 1503 - 1698. Kipindi chote na tarehe hizo walikuwepo watu wanaishi visiwa hivi wanaokuja kujuulikana kama wazanzibari.

Lakini hata kabla kuja Mreno kuvivamia visiwa hivi kulikuwa na utawala wa kijadi/kimila, uliokuwa unaongozwa na Malkia Mwana wa mwana, Mtumbatu na mumewe Mwarabu wa Yemen, na makazi yao yalikuwa ilipo Ngome Kongwe.

Walipovamia Wareno kuumaliza utawala wake, Mwana wa mwana alikimbilia Yemen pamoja na mumewe , na akaishi uhai wake wote.

Uislam Zanzibar ulianza karne ya nane ( 8th Century) na kila mtu alikuwa muumini wa dini hiyo. Watu waliotokana na kizazi hiki, pamoja na mimi ndio tunajinasibu na kujiita Washirazi wa Zanzibar na ndio wazawa. Ukiwa si mshirazi, haijalishi uwe mweupe, mweusi, unamachale na sio muislamu , wewe unakuwa ni wakuja tu
 
Nzuri, mpigieni makofi.Lakini ingekuwa "more factual and sensible" kama ungeandika na kutafakari baadae kama hivi:
" Mgeni aliotoka Oman 1698 akaja Zanzibar na kuzaliana sasa ndio pamekuwa kwake , na mwenyeji aliemkarabisha, ambapo Shirazi Association (1930) ndio chama cha wajukuu wa Mwinyimkuu, wao wenye nchi yao na African Association walikuja baada ya " Siti binti Saad" kuimba kwenye mapema 1900, kuwa " Zanzibar ni njema atakae aje" wanaitwa wakuja ambao wengi wao ni makuli wa bandarini kutoka bara na chimbuko la African Association"

Kisa cha kuhitalifiana Thabit Kombo wenzake Sheikh Ameoir Tajo na Moh'd Shamte ni kukubali muungano wa chama chao kiongozwe na " Mkuja" Karume, na wakaona hilo haliwezekani, wakajitoa kwenye chama cha ASP(1957) na kuunda chama chao ZPPP kilicho weza kuzaa uhuru mwaka 1963 N kutoa Waziri Mkuu wa kwanza mzawa Mo'hd Shamte.
Mpuuzi mkubwa karne ya 7 mpaka 9 Ibun Batuta anasimulia kuhusu kuwapo kwa Himaya ya Zenj ikiwa na maana Himaya ya mtu mweusi. Kama hao wakuja wa 1600 walifanya hila dhidi ya wenyeji.
Wanahistoria husoma kitu kinachoitwa Historiography Hili somo humuwezesha mwanahistoria kuwa makini wakati akipita maandiko mbalimbali ya wanahistoria na kuangalia jinsi maandishi yao yalivyoathiriwa na mitazamo yao ya kisiasa, kijamii, na kundi la kiuwezo wa kiuchumi alilimo mwandishi. Mambo hayo yanamchango mkubwa sana kwa mwandishi kufanya tafasiri ya tukio.
Hivyo si kila mwanahistoria aliyeandika anasifa ya kufanyiwarejea kibubusa. Vitabu vingine unachukua kisa na wahusika tu tafasili ya kisa unaenda kupata kutoka kwenye vyanzo vingine. Rai yangu usituijie na maeleze ya wajinga wakijitetea kwa wake zao au ndugu zao juu ya mambo ya kisiasa na kutwambia ndio ushahidi wa kihistoria.
 
Back
Top Bottom