Maalim Seif ateuliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuwa mgombea Urais Zanzibar

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Hatimaye Mwenyekiti wa ZEC amethibitisha kuteuliwa kwa Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar.


=====

ZEC YAMPITISHA MAALIM SEIF KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imempitisha Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif kuwa mgombea wa Urais baada ya kuwekewa mapingamizi 2 siku ya jana

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Hamid Mahmoud amesema kuwa rufaa iliyokatwa dhidi ya Maalim haina mashiko

#Uchaguzi2020

Zaidi, soma: Zanzibar 2020 - Njama? Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Maalim Seif awekewa Pingamizi
seif 2.jpg
 
Huyu Seif inasemekana sijui ni mtu wa system, aya majina ya kuitana watu wa system hakuna uzalendo wowote.

2015 alishinda uchaguzi ila akaifyata, 2020 pia ni hivyo hivyo tu. Tanzania tunahitaji watu wasioufyata kama akina Lissu, Lema n.k

Hatuwezi kupoteza muda wetu na nguvu zetu kumuunga mkono mtu ambae upande wa pili wanajiitana wa system, hawezi kufanya maamuzi magumu mtu kama huyu.

Yangu ni hayo, nimemaliza.
 
Haikuwa jambo la kushtusha au kumfanya Maalim akose usingizi, japo walikuwa wanasubiri majibu ya komando kwa mgombea wa ccm ili tume itoe majibu ya kumruhusu au lah😁!.
 
Shida ya waTanzania hii itaishia hivi hivi! Yule aliyefoji ile barua anatakiwa achukuliwe hatua. Kwakuwa Tume imejiridhisha kuwa ile barua ni ya kufoji basi wakabidhi hiyo barua na aliyeileta kwa polisi.

Kama ni mgombea wa CCM au wa cham chochote ndio aliweka hilo pingamizi kwa ushahidi wa barua ile ya kufoji na achukuliwe hatua za kisheria kwa kufoji
 
Shida ya waTanzania hii itaishia hivi hivi! Yule aliyefoji ile barua anatakiwa achukuliwe hatua. Kwakuwa Tume imejiridhisha kuwa ile barua ni ya kufoji basi wakabidhi hiyo barua na aliyeileta kwa polisi. Kama ni mgombea wa CCM au wa cham chochote ndio aliweka hilo pingamizi kwa ushahidi wa barua ile ya kufoji na achukuliwe hatua za kisheria kwa kufoji
Tunasubiri kuwasikia polisi wamemchukulia hatua gani aliyefoji nyaraka za serikali.
 
Mtanikumbusha aliyeimba wimbo wenye kibwagizo hicho, lakini mambo ndo kama hivyo.
IMG-20200911-WA0031.jpg
 
Back
Top Bottom