Zanzibar 2020 Maalim Seif achukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
FB_IMG_1593943591148.jpg

Maalim Seif akabidhiwa fomu za kuomba ridhaa ya Chama cha ACT Wazalendo kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Kakabidhiwa fomu hizo na Katibu Mkuu wa Chama, Ndugu Ado Shaibu katika Ofisi Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo iliopo Vuga, Zanzibar.

Maalim Seif amewashukuru sana wanachama wa ACT Wazalendo waliojitokeza kwa wingi kwenye Ofisi Kuu ya Chama, Vuga, Zanzibar kushuhudia tukio la kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar leo asubuhi. "Ahsanteni sana kwa imani na mapenzi yenu kwangu". Kasema Maalim Seif.
FB_IMG_1593945233728.jpg
FB_IMG_1593945238260.jpg
FB_IMG_1593945243808.jpg
 
Maalim Seif akabidhiwa fomu za kuomba ridhaa ya Chama cha ACT Wazalendo kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Kakabidhiwa fomu hizo na Katibu Mkuu wa Chama, Ndugu AAdo Shaibu katika Ofisi Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo iliopo Vuga, Zanzibar.
Ni jambo jema!
 
Alipo tupo, ACT Wazalendo sasa bila shaka wataimaliza safari hii ndefu kuhitimisha kiu ya Zanzibar huru ndani ya Muungano. Urefu wa safari na changamoto nyingi baharini tangu 1995 umemfanya anayeongoza chombo cha ACT wazalendo na timu yake, kuwa mahiri yenye ari kufanya kazi kama timu moja kufika salama salimini kutia nanga Ikulu Zanzibar.

Nahodha wa jahazi la CCM hana uzoefu amebebwa na kuwekwa ktk sukani hivyo atakipeleka mrama chombo chake katika mbio za kujaribu kufikia uongozi wa Taifa la Zanzibar. Sababu timu yake chomboni wanafanya zogo jingi kuuliza nani ni nani ndani ya jahazi pia hawataki kupokea simu za upepo toka Dodoma wakihisi zinawapoteza dira na muelekeo wa safari.

Toka maktaba :
Tendai Biti : This Political Disease of intolerance in Africa is far bigger than Covid-19

 
Mwenyekiti wa Chama, Ndugu @SeifSharifHamad amekabidhiwa fomu kugombea nafasi ya ( 480 X 640 ).jpg

Gwiji la siasa za Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, leo amekabidhiwa rasmi fomu za chama chake za kugombea Urais wa Zanzibar.

Ikumbukwe kwamba Salum Jecha wa CCM tayari alishakatwa na chama chake, huku Lipumba wa CUF kwa mara ya kwanza akikosa mgombea wa Urais mwenye ushawishi hapa Zanzibar.
 
Maalim Seif ndiyo chaguo la waZanzibari hilo halina ubishi, katika siasa za visiwani huyu kila mtu atataka kuja kuonana naye



Video toka Maktaba :

9 Mar 2016
Weekend iliyopita Maalim Seif ambaye ni kiongozi wa chama cha Wananchi C.U.F Maalim Seif alipata kizunguzungu kikali akiwa uwanja wa ndege Zanzibar na kumlazimu kuomba msaada wa kupanda ndege, akasafirishwa kuja Dar akalazwa na ikagundulika ni uchovu tu, jana akatoka Hopsitali leo kaenda kutembelewa Hotelini alikofikia Serena Dar es salaam
Source : millard ayo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom