Maajabu ya wilaya ya Rombo-Kilimanjaro

Maajabu ya wilaya ya Rombo-Kilimanjaro

Wilaya ya rombo ni wilaya iliompakani mwa Kenya na Tanzania iliyo na hali ya hewa nzuri huku ikizungukwa na msitu mnene wa mlima kilimanjaro zao kuu la kibiashara ni ndizi na kahawa japo kahawa imepoteza thamani.

Ni wilaya ilio karibu sana na jiji la Nairobi ni takribani masaa matatu au manne hivi kutoka wilaya ya rombo hadi Jiji la nairobi . Wakazi wake wengi hufanya biashara jiji la Nairobi kuliko miji ya Tanzania . Wakazi wake ni wa kipato cha kati sio maskini sana na wala sio matajiri sana . Wilaya ya Rombo ina miundombinu ya barabara nzuri sana.

Wananchi wake wengi wanatumia bidhaa kutoka nchini Kenya kutokana na kukosekana kwa vyombo vya habari vya kutangaza bidhaa za Tanzania Jambo la kusikitisha wilaya hii hamna station ya redio ya Tanzania inayoshika tofauti na Redio maria. Kwa hiyo wakazi wengi wa Rombo wanasikiliza sana station redio za kenya .

Hili limefanya wilaya hii kutojulikana vizuri na watu kutokuwepo na uelewa mpana wa mambo yanayoendelea nchini mwao. Wilaya ya Rombo japokuwa ni wilaya kongwe hapa nchini haina hospitali ya wilaya. Iliopo ni ya kanisa

Njoo sasa kwenye majengo ya mahakama, kituo cha polisi cha wilaya pamoja na Magereza ya wilaya hazina hadhi kabisa ni zaidi ya magofu . Wilaya ya Rombo ni wilaya iliosahulika kama iko Tanzania japokuwa ina wafanyabiashara wakubwa Tanzania na kenya.

Ni vyema serikali ikayatazama hayo niliyodokeza japo matatizo ni mengi sana yalio kwenye wilaya ya Rombo
Mh! umenikumbusha mbali sana " je huu ni ungwana na lenad mambo mbotela"
 
Kwa mwendo huu bora waendelee kusikiliza matangazo ya Redio Kericho Sub location ...
 
Hii Rombo unayoiongelea ni Rombo Bar au ni hii Rombo ya Useri, Mkuu, Mashati, Tarakea.... Niijuayo mimi??
Rombo ubungo
Wilaya ya rombo ni wilaya iliompakani mwa Kenya na Tanzania iliyo na hali ya hewa nzuri huku ikizungukwa na msitu mnene wa mlima kilimanjaro zao kuu la kibiashara ni ndizi na kahawa japo kahawa imepoteza thamani.

Ni wilaya ilio karibu sana na jiji la Nairobi ni takribani masaa matatu au manne hivi kutoka wilaya ya rombo hadi Jiji la nairobi . Wakazi wake wengi hufanya biashara jiji la Nairobi kuliko miji ya Tanzania . Wakazi wake ni wa kipato cha kati sio maskini sana na wala sio matajiri sana . Wilaya ya Rombo ina miundombinu ya barabara nzuri sana.

Wananchi wake wengi wanatumia bidhaa kutoka nchini Kenya kutokana na kukosekana kwa vyombo vya habari vya kutangaza bidhaa za Tanzania Jambo la kusikitisha wilaya hii hamna station ya redio ya Tanzania inayoshika tofauti na Redio maria. Kwa hiyo wakazi wengi wa Rombo wanasikiliza sana station redio za kenya .

Hili limefanya wilaya hii kutojulikana vizuri na watu kutokuwepo na uelewa mpana wa mambo yanayoendelea nchini mwao. Wilaya ya Rombo japokuwa ni wilaya kongwe hapa nchini haina hospitali ya wilaya. Iliopo ni ya kanisa

Njoo sasa kwenye majengo ya mahakama, kituo cha polisi cha wilaya pamoja na Magereza ya wilaya hazina hadhi kabisa ni zaidi ya magofu . Wilaya ya Rombo ni wilaya iliosahulika kama iko Tanzania japokuwa ina wafanyabiashara wakubwa Tanzania na kenya.

Ni vyema serikali ikayatazama hayo niliyodokeza japo matatizo ni mengi sana yalio kwenye wilaya ya Rombo
 
Rombo ni moja kati ya wilaya zinazosubiri kupandishwa hadhi na kuwa mji na mitaa badala ya vijiji
 
Ila kama mtu una stress fika Rombo, Machame na Marangu...the places are simply romantic; kuna maeneo Mungu aliamua kuyabariki... Nilikuepo Marangu na Rombo majuzi nikatamani kuoa kabisa huko,kuzuri mno wakuu!
 
Suala la maji linapatiwa majibu hivi karibu ni ROMBO
Kampuni ya wananchi ya Kiliwater imeshindwa Kutoa Huduma
Dc Agnes Hokororo amesimamia mabadiliko ya kampuni hiyo iwe mamlaka rasmi ya maji ili ipate udhamini wa serikali na kukoposheka ili mpango wa kutumia maji ya ziwa chala na vyanzo vengine uwezekane

Dc tuliempata Rombo
Na DAS wake
Hawa watu ni kiboko kabisa
 
We kenge huijui rombo, rombo ndio wilaya bora mikiundombinu kuliko hata wilaya ya ubungo dsm, hospitali ya huruma ni best hispital kuliko mwananyamala ama temeke kiufupi hospitali hiyi inahadhi ya kuwa hospitali ya mkoa
 
Rombo ni sehemu nzuri sana, binafsi napapenda sana. Kuna hali ya hewa nzuri sana.
 
Duh aisee umenimbusha nbali sana yule pastor nilikua sikosi program yake Radio Sauti ya Injili kabisa nilianza kumsikia nikiwa mdogo kabisa.

. . . . . . . . . na NENOOOO litaendeleaaaaa!!!! !
Anaitwa Jacob Nyabonge Maina au nimekosea? Memory nzuri sana za home zinakuja aisee
 
Back
Top Bottom