Maajabu ya wilaya ya Rombo-Kilimanjaro

Maajabu ya wilaya ya Rombo-Kilimanjaro

Kiraeni Sec
f8488ae829fb314965e0a23667adacab.jpg
Angalau kwa majengo, hiyo shule ni bora kuliko makumi kwa makumi ya shule za sekondari zilizopo Dar es salaam! Kama ni ya serikali, Selalini atumie hata pesa zake za mfukoni kuboresha hivyo vijumba upande wa kulia manake vinaonekana ni uchafu. Na kwa jiografia hiyo ya Rombo, ningeshangaa sana ningeambiwa ni "maskini" kwa sababu haiwezekani wakati una-share mpaka na Kenya; na Tanzania ilikuwa na uhaba wa bidhaa kwa miaka nenda rudi enzi hizo; halafu bado wakazi mshindwe kutumia hiyo fursa. Watu wengi ambao walitumia fursa ya uhaba wa bidhaa Tanzania, hivi sasa ndio wenye maisha mazuri hata kwa vijijini.
 
Wilaya ya rombo ni wilaya iliompakani mwa Kenya na Tanzania iliyo na hali ya hewa nzuri huku ikizungukwa na msitu mnene wa mlima kilimanjaro zao kuu la kibiashara ni ndizi na kahawa japo kahawa imepoteza thamani.

Ni wilaya ilio karibu sana na jiji la Nairobi ni takribani masaa matatu au manne hivi kutoka wilaya ya rombo hadi Jiji la nairobi . Wakazi wake wengi hufanya biashara jiji la Nairobi kuliko miji ya Tanzania . Wakazi wake ni wa kipato cha kati sio maskini sana na wala sio matajiri sana . Wilaya ya Rombo ina miundombinu ya barabara nzuri sana.

Wananchi wake wengi wanatumia bidhaa kutoka nchini Kenya kutokana na kukosekana kwa vyombo vya habari vya kutangaza bidhaa za Tanzania Jambo la kusikitisha wilaya hii hamna station ya redio ya Tanzania inayoshika hata moja kwa hiyo wakazi wengi wa Rombo wanasikiliza sana station redio za kenya .

Hili limefanya wilaya hii kutojulikana vizuri na watu kutokuwepo na uelewa mpana wa mambo yanayoendelea nchini mwao. Wilaya ya Rombo japokuwa ni wilaya kongwe hapa nchini haina hospitali ya wilaya.

Njoo sasa kwenye majengo ya mahakama, kituo cha polisi cha wilaya pamoja na Magereza ya wilaya hazina hadhi kabisa ni zaidi ya magofu . Wilaya ya Rombo ni wilaya iliosahulika kama iko Tanzania japokuwa ina wafanyabiashara wakubwa Tanzania na kenya.

Ni vyema serikali ikayatazama hayo niliyodokeza japo matatizo ni mengi sana yalio kwenye wilaya ya Rombo
Hapo uliposema haina hospital ya wilaya ni uongo. Rombo ina hospital ya wilaya inaitwa Huruma.
 
Wilaya ya rombo ni wilaya iliompakani mwa Kenya na Tanzania iliyo na hali ya hewa nzuri huku ikizungukwa na msitu mnene wa mlima kilimanjaro zao kuu la kibiashara ni ndizi na kahawa japo kahawa imepoteza thamani.

Ni wilaya ilio karibu sana na jiji la Nairobi ni takribani masaa matatu au manne hivi kutoka wilaya ya rombo hadi Jiji la nairobi . Wakazi wake wengi hufanya biashara jiji la Nairobi kuliko miji ya Tanzania . Wakazi wake ni wa kipato cha kati sio maskini sana na wala sio matajiri sana . Wilaya ya Rombo ina miundombinu ya barabara nzuri sana.

Wananchi wake wengi wanatumia bidhaa kutoka nchini Kenya kutokana na kukosekana kwa vyombo vya habari vya kutangaza bidhaa za Tanzania Jambo la kusikitisha wilaya hii hamna station ya redio ya Tanzania inayoshika hata moja kwa hiyo wakazi wengi wa Rombo wanasikiliza sana station redio za kenya .

Hili limefanya wilaya hii kutojulikana vizuri na watu kutokuwepo na uelewa mpana wa mambo yanayoendelea nchini mwao. Wilaya ya Rombo japokuwa ni wilaya kongwe hapa nchini haina hospitali ya wilaya inayomilikiwa kiserikali bali inayotumika ni ya kanisa

Njoo sasa kwenye majengo ya mahakama, kituo cha polisi cha wilaya pamoja na Magereza ya wilaya hazina hadhi kabisa ni zaidi ya magofu . Wilaya ya Rombo ni wilaya iliosahulika kama iko Tanzania japokuwa ina wafanyabiashara wakubwa Tanzania na kenya.

Ni vyema serikali ikayatazama hayo niliyodokeza japo matatizo ni mengi sana yalio kwenye wilaya ya Rombo
 
Mheshimiwa spika, kwa kuwa radio, pombe, bidhaa nyingi na wanaume hutoka Kenya, na vijana wenyeji wamekimbilia Dar na Arusha, nashauri wilaya hii iwe chini ya Kenya. Nawakilisha
 
Wilaya ya rombo ni wilaya iliompakani mwa Kenya na Tanzania iliyo na hali ya hewa nzuri huku ikizungukwa na msitu mnene wa mlima kilimanjaro zao kuu la kibiashara ni ndizi na kahawa japo kahawa imepoteza thamani.

Ni wilaya ilio karibu sana na jiji la Nairobi ni takribani masaa matatu au manne hivi kutoka wilaya ya rombo hadi Jiji la nairobi . Wakazi wake wengi hufanya biashara jiji la Nairobi kuliko miji ya Tanzania . Wakazi wake ni wa kipato cha kati sio maskini sana na wala sio matajiri sana . Wilaya ya Rombo ina miundombinu ya barabara nzuri sana.

Wananchi wake wengi wanatumia bidhaa kutoka nchini Kenya kutokana na kukosekana kwa vyombo vya habari vya kutangaza bidhaa za Tanzania Jambo la kusikitisha wilaya hii hamna station ya redio ya Tanzania inayoshika hata moja kwa hiyo wakazi wengi wa Rombo wanasikiliza sana station redio za kenya .

Hili limefanya wilaya hii kutojulikana vizuri na watu kutokuwepo na uelewa mpana wa mambo yanayoendelea nchini mwao. Wilaya ya Rombo japokuwa ni wilaya kongwe hapa nchini haina hospitali ya wilaya. Hospital inayotumika kama ya wilaya ni ya kanisa

Njoo sasa kwenye majengo ya mahakama, kituo cha polisi cha wilaya pamoja na Magereza ya wilaya hazina hadhi kabisa ni zaidi ya magofu . Wilaya ya Rombo ni wilaya iliosahulika kama iko Tanzania japokuwa ina wafanyabiashara wakubwa Tanzania na kenya.

Ni vyema serikali ikayatazama hayo niliyodokeza japo matatizo ni mengi sana yalio kwenye wilaya ya Rombo
 
Rombo imeendelea sana ,yani mm nimetembea sana hapa tz hasa vijijini naweza kukupa ushuhuda kuwa Rombo hakuna hata nyumba yanyasi na kama ipo imeachwa kama kumbukumbu tu ya wanafamilia,sasa Rombo unayoisema wewe ni ya Kenya mana Kenya kuna Rombo pia,tatizo Rombo ni maji hasa ukanda wa mashariki ,ila shule zipo nzuri kuliko hapa dar,pia kila mtaa unapitika tena kwa gari na kila familia kuna njia ya kwenda hm kwa gari,sio dar gari inalazwa ccm
Mtoa mada haijui Rombo
 
Mtoa mada usifananishe Rombo na wilaya za ajabu ajabu.....
1. Rombo kwa elimu wamejitahidi sana hadi wazee wa miaka 90 wanajua kusoma na kuandika

2. Umeme upo vijijini tena bila kutegemea mpango wa REA

3. Barabara zinazopitika vizuri

4. Rombo imepangika bila hata kuwepo kwa mipango miji

5. Huduma ya maji safi ilikuwepo tangu miaka ya 90's

6. Ni moja ya wilaya yenye shule nyingi za msingi na sekondari
 
Arusha me huwa sioni tofauti na Moshi kabisa sababu idadi ya wachagga pale Arusha inazidi idadi ya wachagga waliopo Moshi mpaka Manyara Singida Dodoma kote huko wachagga wametapakaa niliingia visiwani ndani kwenye wilaya fulani ya Buchosa Mwanza nilipigwa na butwaa kuwakuta wachagga huko wanafanya Biashara ya Samaki na dagaa visiwa vyote.
Kilimanjaro ina eneo dogo mno pia, hili nalo linachangia, pia fursa nazo zimepungua sana
Kama ukichunguza utaona hata mji wa Moshi nao unarudi nyuma, badala ya kukua unasinyaa, watu wanaukimbia wanaenda kwingine...Dodoma ina boom labda inaweza ikawa prime destination mpya miaka inayokuja
 
Mtoa taarifa acha upotoshaji wewe,Kwamba wilaya haina Hospital ya Wilaya huu ni uongo.Ipo Hospital kubwa na yenye hadhi ya hali ya juu pengine tofauti na Wilaya nyinginezo.Sema tu hospital hiyo ni designated kwa maana ni ya Kanisa na inaendeshwa na Serikali.Kwa kifupi Hospital ipo,tena si moja bali ni Mbili zenye utaratibu huo.(Huruma na Ngoyoni).Vituo vya Afya pia vipo kila Tarafa na vyenye uwezo mzuri.Ukarabati wake umekuwa ukifanyika kila mara.
Mahakama ipo tena imekarabatiwa hivi karibuni,Magereza ipo ya kawaida na yenye hadhi kuliko Magereza mengine kama ya Korogwe,Mwanga na kwingineko,
Kituo cha Polis kipo walau hakipo vizuri sana lakini kinakidhi.
Hivyo utoe taarifa zenye uhakika.usitubabaishe.
Toa sifa pia kama shule kuwepo nyingi,na watu kujituma katika uzalishaji.
Tatizo kubwa ni Maji yasiyo ya uhakika kwa hapa Rombo na hasa wakazi wa tambarare wanataabika sana maji.
Unaingia alafu unatoka.
 
hii wilaya ina magarimengi yanayofanya safari zake kwenda mikoa mingine nadhani kuliko mikoa mingine yote
mabasi yanafanya safari zake kwenda dar ni kma
  1. Dar espress
  2. Tilisho
  3. Wakati express
  4. Saibaba
  5. Longera
  6. Meridian
  7. esther express
  8. wengine ongezeni
 
wanaume wa rombo hawana nguvu wanasaidiwa na wakenya
 
Nipo hapa rombo naipata kill fm vizuri kabisa radio one, clouds na nyingne au unaongelea rombo ya wapi??
Mtoa mada atakuwa mtani(MPARE) Kilimanjaro ni mkoa wa pili kwa utajiri/maendeleo Tz kwa mujibu bunge la bajeti 2016/2017 kupitia wizara fedha kwa takwimu zilizo wasilishwa na waziri wa fedha bwana Philip Izidor Mipango wakilinganisha miundo mbinu yani hoapitali,shule Barbara nk,pia kipato cha mtu mmoja mmoja na mambo mengine mengi.
 
Zile zilikuwa agenda ya kupendelea mikoa ya kanda ya ziwa kama hujui, Kilimanjaro ni ya pili wakati watu wanakukimbia?
 
Kubusu redio, watu wanapenda kusikiliza radio citizen ya kenya sabubu ina vipindi vizuri sana, na inapiga nyimbo saaana za tanzania
 
Kumbe ndio kupo hivyoo! Basi mim nilijua kwa hao jamaa ni Ulaya ndogo maana wengi wao wana mawe kwel kwel.
 
Back
Top Bottom