Maajabu ya Serikali yetu Maamuzi IMTU hospital

bakuza

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
492
Reaction score
104
Maamuzi ya Serikali na maajabu yake pale IMTU hospital
Kwanza nitanabaishe kuwa nilisikitishwa na kitendo kilichofanywa na Utawala wa Hospitali ya IMTU hasa wanaohusika na chuo kwa kutupa jalalani mabaki ya miili ya binadamu waliotumika katika mafunzo.Hilo jambo limeonesha kukosa utu kwa wahusika waliotakiwa kufanya taratibu za kuyateketeza mabaki hayo na kama waliona kuyateketeza ni ghalama basi wangechimba shimo na kuyafukia ili yasituletee sintofahamu kama hii iliyoletwa.

Haya maamuzi ya kufungwa kwa hospitali ya IMTU ni miongoni mwa maamuzi ya ajabu kutolewa na tunaotarajia washauliwe na kufikia maamuzi yenye tija kwa taifa lakini ajabu ni kuwa mara kwa mara wamekuwa wanatoa maamuzi ambayo hata kwa fikra ya mtu mmoja asiye na elimu kubwa hayaingii akilini hata chembe.Tumekuwa tukishuhudia maamuzi ya kishabiki na kisiasa zaidi katika mambo ya msingi na wananchi hawahoji mambo haya..hii ni ajabu kabisa.

Mtu dhaifu ama mvivu wa fikra pekee ndiye anaweza kushangilia maamuzi haya yasiyo ya busara hata chembe..Hii si adhabu kwa IMTU hospital kama wanaodhani wanajua kufikiri wanavyotaka kutuaminisha.Hii ni adhabu kwa wananchi wan nchi hii kama nitakavyoorodhesha kwa uchache hapo chini..tukitilia maanani kuwa hospitali zetu za serikali na binafsi hazitoshi na hata za umma hazina vifaa vya kitekinolojia vya kutosha kuhudumia wananchi hii hupelekea mara nyingi wagonjwa kutumwa kwenda katika hospitali hizo za binafsi kupata huduma ambayo hata Muhimbili kama hospitali ya Taifa hawana.

Wakati maamuzi haya yakitokea yamenikumbusha visa vya ajari za barabarani ambapo Serikali badala ya kuchukua hatua stahiki kwa wakosaji huishia kuifungia kampuni na huku magari yakibadilishwa majina ya kampuni na kuendelea na kazi bila shida,sikuacha kuikumbuka DECI ambayo ililiza watu wengi mpaka leo wameibiwa pesa zao sisemi wameibiwa na wajanja bali serikali yao ambayo iliiacha DECI ikafanya kazi zake miaka na kukusanya pesa nyingi wakati serikali ipo kimya na mwishowe wakaifungia na kuichukua pesa ya walalahoi wasijue wakadai kwa nani?

Hebu tafakarisha kichwa kidogo.Hivi leo tunaposhangilia kufungiwa kwa hospitali ya IMTU tumefikilia haya:-
1. Vijana wetu pale wataelekea wapi kuendelea na masomo yao,au nao ni wakosaji?

2. Wafanyakazi wa kitanzania waliopata ajira pale kujikimu maisha yao bila kuwasahau wafanya usafi na walinzi wataishi vipi? au nao wanausika katika kukosa huko.

3. Wagonjwa wanaotibiwa pale wataelekezwa wapi wakati mahospitali tuliyonayo hayatoshi unaenda Muhimbili asubuhi kurudi nyumbani usiku na wakati mwingine umepigwa kalenda utadhani na ugonjwa unasubiri..Au na hao wananchi wanaotibiwa pale ni wakosaji?

4. Je serikali inayokusanya kodi pale itapataje makusanyo tena ilihali hospitali imefungwa?

5. Je wajasiliamali walioingia mikataba ya kuisambazia huduma hospitali ile,ziwe za stationary,chakula na nyingi nyinginezo je nao wamekosa nini?na mitaji yao imewekwaje na malipo yao watapataje?

6. Na wahitimu wetu wa kidato cha sita waliotarajia kupata udahili pale ya kujiongezea maarifa wataelekea wapi ili hali vyuo vyetu havitoshi kuwadahili wenye sifa wote.

7. Na Wale wahitimu wa kada ya utabibu ambao Mungu jaria wangepata ajira pale waelekee wapi ili hali soko la ajira lipo taabani nchini kama tujuavyo?

8. ……….n.k

Tusemeje sasa sisi waonao karibu tusio na viona mbali ?kwamba serikali haijui mkosaji ni nani katika hospitali ile ili akawajibika kwa makosa yake,kama haijui wakosaji mpaka kufikia kubahatisha kwa kutoa adhabu ya jumla ya kufungia hospitali nzima ya IMTUadhabu ambayo inamkumba kila mtu Je kwa nini wakakamata hao nane waliojinasibu kututangazia?
Ngoja nipayuke bana serikali mnatukosea sana tena sana,msione wananchi tupo kimya mkadhani hatuwazi yaliyo sahihi bali hatupewi nafasi ya kuyaweka wazi,ila muda waja ambao hatutaweza kuwavumilia wenye maamuzi yasiyo na tija kwa taifa kisa ni mwanasiasa.Haiwezekani kuweka makanjanja katika kuamua hatima ya taifa eti kwa sababu tu ni mshirika katika siasa zetu au alitufadhiri katika chama au ana ushawishi wa kisiasa chamani.Hebu tuweke siasa pembeni tufikirie taifa kwanza.
Nadhani mimi mwenye akili kiduchu kwa elimu yangu ya kata nimewaza hivyo wewe jeeeeee..?????????
 
Mkuu nisawa ukumbke uhur bla mpaka ni...hataungetenda mazur ukaja kuhalb sheria haiangalii.otherwise tugefanya tuwezavyo
 
Pamoja na yoote hayo lakini kama hawafuati utaratibu FUNGIA tuu mambo mengine yatajulikana mbele kwa mbele.
Kwanza Serikali ingeitaifisha tuu.
 
Bla blaaa nyingiiiii, acha sharia ichukue mkondo wake, tena adhabu hiyo ni ndogo sana haiendani na kosa walilo fanya!
 
wanahitaji adhabu kali tu hizo zisiwe sababu za kutetea maovu...angejitokeza hata mwanafunzi kukemea uozo huo wangekuwa mahali pazuri lakini hakuna hata mmoja aliyefanya chochote.............mpaka wananchi watoe taarifa wao walikuwa wapi wakati wanafanya maamuzi hayo?
 
kwa akili kama yako tunakoelekea kila mtu atakuwa anafanya jambo analolitaka yeye bila kufuata sheria inasemaje. Kwa mtaji huu hatuwezi kufika popote. kama watu wanakuja kutupa mabaki ya miili ya binadamu mtaani na wewe unaona wameonewa ni hatari sana kwa nchi yetu. BTW kwa sababu unatetea tumbo lako siwezi kukushangaa.
 
Dar es Salaam. Serikali imeifungia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), baada ya kuifanyia ukaguzi na kubaini kasoro kadhaa za uendeshaji wake.

Ukaguzi huo ulifanywa jana na jopo la wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya IMTU kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hospitali hiyo imefungiwa wakati Kamati ya Watu 15, iliyoundwa na Serikali ikiendelea kuchunguza kashfa hiyo.

Hata hivyo, wakati taarifa za kufungiwa zikitolewa habari za ndani zinaonyesha kuwa hapakuwa na mgonjwa yeyote hospitalini hapo, ikielezwa kuwa wagonjwa wote waliondoka baada ya kuibuka kwa kashfa ya viungo IMTU ikihusishwa.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Bunini Kamba alisema kuwa wameamua kuifungia hospitali hiyo kwa muda usiojulikana, baada ya kukuta upungufu mbalimbali katika maeneo ya kutolea huduma, jambo linalohatarisha usalama wa wagonjwa.

“Maabara tumekuta dawa ambazo muda wake wa kutumika umepita na hazikuwa katika mpangilio maalumu. Wodini hakuna usimamizi maalumu, hasa kwa wagonjwa wenye majeraha,” alisema Dk Bunini.

Aliongeza: “Hakuna wauguzi wa kutosha na mashine ya kuchoma taka ngumu haifanyi kazi vilivyo. Tumeona kuwa hospitali hii haistahili kuendelea kutoa huduma kwa jamii.”

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Profesa Yasin Mgonda alisema: “Tumesikia uamuzi huo uliotolewa baada ya kufanyika ukaguzi. Tutajirekebisha na tutakapokamilisha tutawaita kuja kutukagua tena.”

Alisema kuwa pamoja na sababu nyingine, hospitali yake imefungiwa baada ya kubainika kuwa bomba la maabara limeharibika na halitoi maji.

Nyingine ni kutojaza vitabu vya wagonjwa kwa mujibu wa taratibu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, pia duka lake la dawa kuwa halijasajiliwa lakini akasema sababu hiyo imewashangaza kwani wanachojua wao duka hilo limesajiliwa.

Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia aliliambia gazeti hili kwamba anaipongeza Serikali kwa uamuzi huo akisema utanusuru maisha ya wananchi waliokuwa wakipata huduma hospitalini hapo.

BURNING QUESTIONS FROM THE ABOVE STORY
1. Is the inspection special for IMTU or they do have routine inspections for other hospitals?
2. If they have routine inspections to health centers, when was their last visit to IMTU?
3. Is the penalty imposed according to 'penalty clause in agreement' or just emotional?
 
Hiyo bi adhabu kwa wananchi wanaopata huduma Imtu,na itafunguliwa soon maana hili ni dili la kufunika Escrow na IPTL.behold.
 
Dar es Salaam. Serikali imeifungia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), baada ya kuifanyia ukaguzi na kubaini kasoro kadhaa za uendeshaji wake.

Ukaguzi huo ulifanywa jana na jopo la wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya IMTU kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ukaguzi huo ulifanywa jana na jopo la wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya IMTU kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hospitali hiyo imefungiwa wakati Kamati ya Watu 15, iliyoundwa na Serikali ikiendelea kuchunguza kashfa hiyo.

Hata hivyo, wakati taarifa za kufungiwa zikitolewa habari za ndani zinaonyesha kuwa hapakuwa na mgonjwa yeyote hospitalini hapo, ikielezwa kuwa wagonjwa wote waliondoka baada ya kuibuka kwa kashfa ya viungo IMTU ikihusishwa.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Bunini Kamba alisema kuwa wameamua kuifungia hospitali hiyo kwa muda usiojulikana, baada ya kukuta upungufu mbalimbali katika maeneo ya kutolea huduma, jambo linalohatarisha usalama wa wagonjwa.

"Maabara tumekuta dawa ambazo muda wake wa kutumika umepita na hazikuwa katika mpangilio maalumu. Wodini hakuna usimamizi maalumu, hasa kwa wagonjwa wenye majeraha," alisema Dk Bunini.

Aliongeza: "Hakuna wauguzi wa kutosha na mashine ya kuchoma taka ngumu haifanyi kazi vilivyo. Tumeona kuwa hospitali hii haistahili kuendelea kutoa huduma kwa jamii."

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Profesa Yasin Mgonda alisema: "Tumesikia uamuzi huo uliotolewa baada ya kufanyika ukaguzi. Tutajirekebisha na tutakapokamilisha tutawaita kuja kutukagua tena."

Alisema kuwa pamoja na sababu nyingine, hospitali yake imefungiwa baada ya kubainika kuwa bomba la maabara limeharibika na halitoi maji.

Nyingine ni kutojaza vitabu vya wagonjwa kwa mujibu wa taratibu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, pia duka lake la dawa kuwa halijasajiliwa lakini akasema sababu hiyo imewashangaza kwani wanachojua wao duka hilo limesajiliwa.

Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia aliliambia gazeti hili kwamba anaipongeza Serikali kwa uamuzi huo akisema utanusuru maisha ya wananchi waliokuwa wakipata huduma hospitalini hapo.

Good!!!
 
....hayo mengine yooote kwangu sio hoja ila kwasababu ni ya wahindi,funga tu manyanyasaji kweli haya majamaaa...
 
Maamuzi ya Serikali na maajabu yake pale IMTU hospital
Kwanza nitanabaishe kuwa nilisikitishwa na kitendo kilichofanywa na Utawala wa Hospitali ya IMTU hasa wanaohusika na chuo kwa kutupa jalalani mabaki ya miili ya binadamu waliotumika katika mafunzo.Hilo jambo limeonesha kukosa utu kwa wahusika waliotakiwa kufanya taratibu za kuyateketeza mabaki hayo na kama waliona kuyateketeza ni ghalama basi wangechimba shimo na kuyafukia ili yasituletee sintofahamu kama hii iliyoletwa.

Haya maamuzi ya kufungwa kwa hospitali ya IMTU ni miongoni mwa maamuzi ya ajabu kutolewa na tunaotarajia washauliwe na kufikia maamuzi yenye tija kwa taifa lakini ajabu ni kuwa mara kwa mara wamekuwa wanatoa maamuzi ambayo hata kwa fikra ya mtu mmoja asiye na elimu kubwa hayaingii akilini hata chembe.Tumekuwa tukishuhudia maamuzi ya kishabiki na kisiasa zaidi katika mambo ya msingi na wananchi hawahoji mambo haya..hii ni ajabu kabisa.

Mtu dhaifu ama mvivu wa fikra pekee ndiye anaweza kushangilia maamuzi haya yasiyo ya busara hata chembe..Hii si adhabu kwa IMTU hospital kama wanaodhani wanajua kufikiri wanavyotaka kutuaminisha.Hii ni adhabu kwa wananchi wan nchi hii kama nitakavyoorodhesha kwa uchache hapo chini..tukitilia maanani kuwa hospitali zetu za serikali na binafsi hazitoshi na hata za umma hazina vifaa vya kitekinolojia vya kutosha kuhudumia wananchi hii hupelekea mara nyingi wagonjwa kutumwa kwenda katika hospitali hizo za binafsi kupata huduma ambayo hata Muhimbili kama hospitali ya Taifa hawana.

Wakati maamuzi haya yakitokea yamenikumbusha visa vya ajari za barabarani ambapo Serikali badala ya kuchukua hatua stahiki kwa wakosaji huishia kuifungia kampuni na huku magari yakibadilishwa majina ya kampuni na kuendelea na kazi bila shida,sikuacha kuikumbuka DECI ambayo ililiza watu wengi mpaka leo wameibiwa pesa zao sisemi wameibiwa na wajanja bali serikali yao ambayo iliiacha DECI ikafanya kazi zake miaka na kukusanya pesa nyingi wakati serikali ipo kimya na mwishowe wakaifungia na kuichukua pesa ya walalahoi wasijue wakadai kwa nani?

Hebu tafakarisha kichwa kidogo.Hivi leo tunaposhangilia kufungiwa kwa hospitali ya IMTU tumefikilia haya:-
1. Vijana wetu pale wataelekea wapi kuendelea na masomo yao,au nao ni wakosaji?

2. Wafanyakazi wa kitanzania waliopata ajira pale kujikimu maisha yao bila kuwasahau wafanya usafi na walinzi wataishi vipi? au nao wanausika katika kukosa huko.

3. Wagonjwa wanaotibiwa pale wataelekezwa wapi wakati mahospitali tuliyonayo hayatoshi unaenda Muhimbili asubuhi kurudi nyumbani usiku na wakati mwingine umepigwa kalenda utadhani na ugonjwa unasubiri..Au na hao wananchi wanaotibiwa pale ni wakosaji?

4. Je serikali inayokusanya kodi pale itapataje makusanyo tena ilihali hospitali imefungwa?

5. Je wajasiliamali walioingia mikataba ya kuisambazia huduma hospitali ile,ziwe za stationary,chakula na nyingi nyinginezo je nao wamekosa nini?na mitaji yao imewekwaje na malipo yao watapataje?

6. Na wahitimu wetu wa kidato cha sita waliotarajia kupata udahili pale ya kujiongezea maarifa wataelekea wapi ili hali vyuo vyetu havitoshi kuwadahili wenye sifa wote.

7. Na Wale wahitimu wa kada ya utabibu ambao Mungu jaria wangepata ajira pale waelekee wapi ili hali soko la ajira lipo taabani nchini kama tujuavyo?

8. .n.k

Tusemeje sasa sisi waonao karibu tusio na viona mbali ?kwamba serikali haijui mkosaji ni nani katika hospitali ile ili akawajibika kwa makosa yake,kama haijui wakosaji mpaka kufikia kubahatisha kwa kutoa adhabu ya jumla ya kufungia hospitali nzima ya IMTUadhabu ambayo inamkumba kila mtu Je kwa nini wakakamata hao nane waliojinasibu kututangazia?
Ngoja nipayuke bana serikali mnatukosea sana tena sana,msione wananchi tupo kimya mkadhani hatuwazi yaliyo sahihi bali hatupewi nafasi ya kuyaweka wazi,ila muda waja ambao hatutaweza kuwavumilia wenye maamuzi yasiyo na tija kwa taifa kisa ni mwanasiasa.Haiwezekani kuweka makanjanja katika kuamua hatima ya taifa eti kwa sababu tu ni mshirika katika siasa zetu au alitufadhiri katika chama au ana ushawishi wa kisiasa chamani.Hebu tuweke siasa pembeni tufikirie taifa kwanza.
Nadhani mimi mwenye akili kiduchu kwa elimu yangu ya kata nimewaza hivyo wewe jeeeeee..?????????
acha sheria ifuate mkondo wake.
 
Pengine imefungiwa pia ili kupisha hasira kutoka kwa watanzania
kwa kile kilichoonekana, pia

Pamoja na huo uzembe wa kutupa miili ya watu jalalani;

Inasemekana pia kuwa hiyo hospital ina mapungufu ya wauguzi wa kutosha,
haina vifaa vya kutosha, kuwapa wagonjwa dawa zilizokwisha muda wake;
na hata wauguzi kufanya kazi ambazo si za kwao.
 
unapendekeza nin kifanyike , una bwabwaaajaaa,,, ! Pointles...
 
Hakuna haja ya kutetea uovu, imtu ni taasisi na co mtu binafsi kufungiwa kwake iwe kama adhabu ya mwanzo tu. Iwajibishwe kwa mujibu wa sheria
 
yani badala ya kuadhibu watendaji wameadhibu wananchi wanaohitaji huduma.
Acheni unafiki ndugu zangu. Hivi hayo mapendekezo si yalitolewa na chama cha madaktari? Mmekuwa mkilaumu serikali kuwa ama inachelewa kuchukua hatua au haichukui hatua kabisa. Sasa serikali imefanya kweli mnaleta bla blaa nyingi. Mahospitali yote hayo ya private hamyaoni mkaenda kutibiwa nyie wenye hela zenu? Maana mngesingizia kuwa walala hoi hawana pa kukimbilia. WaTz bwana........
 
Maamuzi ya Serikali na maajabu yake pale IMTU hospital
Kwanza nitanabaishe kuwa nilisikitishwa na kitendo kilichofanywa na Utawala wa Hospitali ya IMTU hasa wanaohusika na chuo kwa kutupa jalalani mabaki ya miili ya binadamu waliotumika katika mafunzo.Hilo jambo limeonesha kukosa utu kwa wahusika waliotakiwa kufanya taratibu za kuyateketeza mabaki hayo na kama waliona kuyateketeza ni ghalama basi wangechimba shimo na kuyafukia ili yasituletee sintofahamu kama hii iliyoletwa.

Haya maamuzi ya kufungwa kwa hospitali ya IMTU ni miongoni mwa maamuzi ya ajabu kutolewa na tunaotarajia washauliwe na kufikia maamuzi yenye tija kwa taifa lakini ajabu ni kuwa mara kwa mara wamekuwa wanatoa maamuzi ambayo hata kwa fikra ya mtu mmoja asiye na elimu kubwa hayaingii akilini hata chembe.Tumekuwa tukishuhudia maamuzi ya kishabiki na kisiasa zaidi katika mambo ya msingi na wananchi hawahoji mambo haya..hii ni ajabu kabisa.

Mtu dhaifu ama mvivu wa fikra pekee ndiye anaweza kushangilia maamuzi haya yasiyo ya busara hata chembe..Hii si adhabu kwa IMTU hospital kama wanaodhani wanajua kufikiri wanavyotaka kutuaminisha.Hii ni adhabu kwa wananchi wan nchi hii kama nitakavyoorodhesha kwa uchache hapo chini..tukitilia maanani kuwa hospitali zetu za serikali na binafsi hazitoshi na hata za umma hazina vifaa vya kitekinolojia vya kutosha kuhudumia wananchi hii hupelekea mara nyingi wagonjwa kutumwa kwenda katika hospitali hizo za binafsi kupata huduma ambayo hata Muhimbili kama hospitali ya Taifa hawana.

Wakati maamuzi haya yakitokea yamenikumbusha visa vya ajari za barabarani ambapo Serikali badala ya kuchukua hatua stahiki kwa wakosaji huishia kuifungia kampuni na huku magari yakibadilishwa majina ya kampuni na kuendelea na kazi bila shida,sikuacha kuikumbuka DECI ambayo ililiza watu wengi mpaka leo wameibiwa pesa zao sisemi wameibiwa na wajanja bali serikali yao ambayo iliiacha DECI ikafanya kazi zake miaka na kukusanya pesa nyingi wakati serikali ipo kimya na mwishowe wakaifungia na kuichukua pesa ya walalahoi wasijue wakadai kwa nani?

Hebu tafakarisha kichwa kidogo.Hivi leo tunaposhangilia kufungiwa kwa hospitali ya IMTU tumefikilia haya:-
1. Vijana wetu pale wataelekea wapi kuendelea na masomo yao,au nao ni wakosaji?

2. Wafanyakazi wa kitanzania waliopata ajira pale kujikimu maisha yao bila kuwasahau wafanya usafi na walinzi wataishi vipi? au nao wanausika katika kukosa huko.

3. Wagonjwa wanaotibiwa pale wataelekezwa wapi wakati mahospitali tuliyonayo hayatoshi unaenda Muhimbili asubuhi kurudi nyumbani usiku na wakati mwingine umepigwa kalenda utadhani na ugonjwa unasubiri..Au na hao wananchi wanaotibiwa pale ni wakosaji?

4. Je serikali inayokusanya kodi pale itapataje makusanyo tena ilihali hospitali imefungwa?

5. Je wajasiliamali walioingia mikataba ya kuisambazia huduma hospitali ile,ziwe za stationary,chakula na nyingi nyinginezo je nao wamekosa nini?na mitaji yao imewekwaje na malipo yao watapataje?

6. Na wahitimu wetu wa kidato cha sita waliotarajia kupata udahili pale ya kujiongezea maarifa wataelekea wapi ili hali vyuo vyetu havitoshi kuwadahili wenye sifa wote.

7. Na Wale wahitimu wa kada ya utabibu ambao Mungu jaria wangepata ajira pale waelekee wapi ili hali soko la ajira lipo taabani nchini kama tujuavyo?

8. ……….n.k

Tusemeje sasa sisi waonao karibu tusio na viona mbali ?kwamba serikali haijui mkosaji ni nani katika hospitali ile ili akawajibika kwa makosa yake,kama haijui wakosaji mpaka kufikia kubahatisha kwa kutoa adhabu ya jumla ya kufungia hospitali nzima ya IMTUadhabu ambayo inamkumba kila mtu Je kwa nini wakakamata hao nane waliojinasibu kututangazia?
Ngoja nipayuke bana serikali mnatukosea sana tena sana,msione wananchi tupo kimya mkadhani hatuwazi yaliyo sahihi bali hatupewi nafasi ya kuyaweka wazi,ila muda waja ambao hatutaweza kuwavumilia wenye maamuzi yasiyo na tija kwa taifa kisa ni mwanasiasa.Haiwezekani kuweka makanjanja katika kuamua hatima ya taifa eti kwa sababu tu ni mshirika katika siasa zetu au alitufadhiri katika chama au ana ushawishi wa kisiasa chamani.Hebu tuweke siasa pembeni tufikirie taifa kwanza.
Nadhani mimi mwenye akili kiduchu kwa elimu yangu ya kata nimewaza hivyo wewe jeeeeee..?????????

Teda yako haina soko tena mkuu??mbona kazi zipo mkuu ?Tz inaardhi kumbwa tu ? Maana inaoneka hauna point ya kuzungumza .ni upuuzi mtupu uliojaribu kuandika hapa .KWA KOSA WALIOFANYA HAWASTAIRI CYO KUFUNGIWA TU NI KUFUTWA KABISA HICHO CHUO NA KUTAIFISHWA KABISA .WANGEKUWA KWAO INDIA WANGEFANYA UPUUZI HUU??
 
Kilichofungwa pale IMTU ni hospital na sio chuo!!. Na kwa mujibu wa naibu wazir wa afya ufungaji wa hospital hauhusiani na tukio la utupaji wa mabaki ya miili ya watu ila mapungufu yaliyopi hapo hospitalin ndio sababu
 
Back
Top Bottom