Watapatatabusana
Member
- Jul 30, 2018
- 15
- 15
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Enock Koola, amekabidhi kiasi cha shilingi milioni 100 kama mchango wake na marafiki zake kwa ajili ya ukarabati wa Kliniki ya Meno pamoja na Maabara katika Hospitali ya Marangu, akisema lengo ni kurejesha hadhi ya hospitali hiyo na kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.
Koola amesema wazo la kuchangia ukarabati huo lilianza baada ya yeye na marafiki zake kujadili namna ya kusaidia kuboresha huduma za afya katika Jimbo la Vunjo, baada ya kuona hali halisi ya Hospitali ya Marangu na changamoto zilizokuwa zikiikabili.
Katika hatua nyingine, Koola amependekeza Kliniki ya Meno hiyo ipewe jina la “Engerasia Dental Unit”, kwa heshima ya mama wa mmoja wa marafiki zake waliochangia katika ukarabati huo.
Katika hafla hiyo,Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Fredrick Shoo mfano amempongeza Koola kwa mchango huo, akisema uboreshaji wa huduma za meno na maabara utakuwa na umuhimu katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo.