Na ile Meli ya Mv Bukoba, imechukuliwa na Alliens, yupo Mzamiaji mmoja alishuhudia hayo akiwa chini katika harakati za Uopoaji Maiti, alipo ibuka juu, akiwa na nia ya Kueleza/kuhadithia kile alicho kiona, ghafla alipatwa na UBUBU....!!
Tunakumbuka wote, pale Divers (Wazamiaji) kutoka nchini Afrika ya Kusini, walipo kuja kwa nia ya kusaidia zoezi hilo, inasemekana ilikuwa ni mbilinge mbilinge ya vuta nikuvute, kati ya Wazamiaji na Vinyambululu (Vibwengo) wa chini ya Bahari, Binaadamu akitaka kuchukua Mwili wa Marehemu, na hawa Alliens waking'ang'ania Maiti kwa nia ya Kunyonya Damu pamoja na kula Nyama.
Wazamiaji walishindwa zoezi, japo siri ilivuja kuwa walishauri, ili kazi ya uopoaji iweze kuendelea, waliomba watoe kafara ya kumwaga Damu na Nyama, kwa kuchinjwa Ng'ombe angalau Kumi, na Mizoga yake imwagwe sehemu ya tukio, Wazee na Serikali walilikataa hilo.
Hatimae zoezi kushindikana, na Wazamiaji (wa kigeni) kufungasha Mizigo na kurudi kwao...!!
NB: Wahenga wanalijua hili tukio vizuri.
Cc: Mshana Jr.
Sent using
Jamii Forums mobile app