Maajabu ya Kisiwa cha Bermuda

Maajabu ya Kisiwa cha Bermuda

Uko ndani ya ndege. Kukiwa na utulivu mkubwa ambapo watu wengi wanaonekana kusinzia. Umejiegemea kwenye seat yako ukitafakari hili na lile.. Ghafla unaskia sauti ya kilio cha mtoto mchanga kwa mbali.. unageuka huku na kule na unajiridhisha sauti ile unayoiskia haitoki ndani ya ndege bali nje.

Unajiuliza mara mbili mbili.. unashangaa . Ghafla unajiskia ulazima wa kwenda haja ndogo, unapokaribia mlango wa choo unaanza kuhisi mle ndani ya choo kuna nyoka kibao. Unajipa ujasiri na kufungua mlango, mlango haufunguki. Unasukuma tena kwa nguvu mlango bado haufunguki.

Unapata hisia kuna nyoka mkubwa yuko mlangoni ndio maana mlango haufunguki.Unaamua kuahirisha tukio unarudi kukaa kwenye kiti chako, ile kukaa tu unakutana na boonge la mtikisiko (turbulent). unaanza kuhisi ndege inadondoka…unaangalia saa..ni saa 5 usiku na bado kuna kama masaa matano kabla ya ndege kutua.

Unafungua dirisha kuangalia nje ni giza totoro, unachokishuhudia nje ni mvua kubwa na radi, pia sauti ya kilio cha kitoto kichanga inasikika zaidi. Isitoshe unaskia mshindo mkubwa kwa mbali. Haraka unafunga dirisha.Unaamua kupambana na hofu kwa kujiimbisha,…Mbinguni..kuna makao mazuri sana.

unaangalia pembeni unajistukia umekuwa ukiimba kwa sauti kiasi cha kuwaamsha baadhi ya abiria wenzako ambao wanakuangalia kwa jicho la kukushutumu na pia unajistukia ni kama wimbo wenyewe unakusuta vile kwa mazingira uliyonayo. Unajaribu kupotezea kwa kujichekesha lakini sauti inayotoka inakuwa ya ajabu kutokana na hofu uliyonayo.

Unaacha kuimba na kuiruhusu hofu iliyokushika itawale. Unawasha kitv unaangalia geographical location ulipo… ramani inakuonesha unapita kisiwa cha Bermuda.Kijasho chembamba kinakutiririka japo kuna AC. Unatamani ushuke.

hadithi hii inatufundisha nini?
 
nope.. its just a myth.. hizi stori nilisikia nikaamua kufanya uchukunzi kwa kusoma kwenye sites kadhaa na vitabu.. ni uwongo tu unakuzwa/unatengenezwa na watu na kuna watu/wazungu wametengeneza fedha nyingi kwa hii stori..
kwenye data za ajali za ndege na meli za marekani kuna ajali moja tu ya ndege tena ni eneo pembeni kidogo imewahi kuripotiwa na hakuna pengine popote imewahi kurekodiwa kuwa kuna ndege/meli imewahi kupotea maeneo hayo..
so ni uwongo tu..

Olele huo uchunguzi ulioufanya nina mashaka nao....Nikuhakikishie yanayosemwa kuhusu Bermuda triangle juu ya mauzauza sii uongo. Wala hulazimishwi kuamini ni kweli kwani hata usipoamini haitabadilisha ukweli uliopo. Katika ile triangle kuna uhusiano na nguvu za giza na wazungu hasa american elites (walio kwenye occultic groups) wanajua na ni moja ya sehemu zao za kazi . Sayansi iliyoko pale ni spiritual....
 
Dont let them get in your head they want to probe you, figure your thoughts so they can try and control you.
And through you control your whole crew.. Its european psychology boy
 
Olele huo uchunguzi ulioufanya nina mashaka nao....Nikuhakikishie yanayosemwa kuhusu Bermuda triangle juu ya mauzauza sii uongo. Wala hulazimishwi kuamini ni kweli kwani hata usipoamini haitabadilisha ukweli uliopo. Katika ile triangle kuna uhusiano na nguvu za giza na wazungu hasa american elites (walio kwenye occultic groups) wanajua na ni moja ya sehemu zao za kazi . Sayansi iliyoko pale ni spiritual....

ah mi wala sibishani na wewe kwamba kuna nguvu za giza au vipi.. nadhani ndo umeweka hapo video kuthibitusha.. kitu ninachopinga ni kuwa kuna ajali nyingi za ndege na meli zimetokea eneo hilo. na ninasimamia kwenye repoti za watafiti kadhaa na mmoja wapo alitafiti kwenye taasisi moja ya marekani inayorecord matukio ya ajali au (ndege na meli) yote yanayotokea au kupotea baharini tokea miaka ya 1800 akakuta hiyo ajali moja tu iliyotokea kwenye maeneo hayo na hakuna tukio/ajali lolote lilirekodiwa sehemu yoyote duniani kutokea kwenye maeneo hayo. so akawa anauliza swali hizo ajali zinazosemekana mbona hakuna sehemu yeyeto duniani zimewahi kurekodiwa/kuripotiwa.
ndio maana nina ujasiri wa kusema ni uwongo kwa sababu nina mahali nasimamia na report kadhaa nilizosoma..

so wewe unaposimamia ni hiyo video ya watu wanaotolewa mapepo hapo.. ndo ushahidi wako
 
Hizo ni american mysteries, mtoa mada amekurupuka bila kujua dhumuni lake hasa hizo mysteries school of thought. Ukizisoma bila kuwa na zako sio muda utamkataa Mungu. Mysteries school ni kati madarasa ya mwanzo kwa wale wanojiita ellites (planners/NWO).
 
Uko ndani ya ndege. Kukiwa na utulivu mkubwa ambapo watu wengi wanaonekana kusinzia. Umejiegemea kwenye seat yako ukitafakari hili na lile.. Ghafla unaskia sauti ya kilio cha mtoto mchanga kwa mbali.. unageuka huku na kule na unajiridhisha sauti ile unayoiskia haitoki ndani ya ndege bali nje.

Unajiuliza mara mbili mbili.. unashangaa . Ghafla unajiskia ulazima wa kwenda haja ndogo, unapokaribia mlango wa choo unaanza kuhisi mle ndani ya choo kuna nyoka kibao. Unajipa ujasiri na kufungua mlango, mlango haufunguki. Unasukuma tena kwa nguvu mlango bado haufunguki.

Unapata hisia kuna nyoka mkubwa yuko mlangoni ndio maana mlango haufunguki.Unaamua kuahirisha tukio unarudi kukaa kwenye kiti chako, ile kukaa tu unakutana na boonge la mtikisiko (turbulent). unaanza kuhisi ndege inadondoka…unaangalia saa..ni saa 5 usiku na bado kuna kama masaa matano kabla ya ndege kutua.

Unafungua dirisha kuangalia nje ni giza totoro, unachokishuhudia nje ni mvua kubwa na radi, pia sauti ya kilio cha kitoto kichanga inasikika zaidi. Isitoshe unaskia mshindo mkubwa kwa mbali. Haraka unafunga dirisha.Unaamua kupambana na hofu kwa kujiimbisha,…Mbinguni..kuna makao mazuri sana.

unaangalia pembeni unajistukia umekuwa ukiimba kwa sauti kiasi cha kuwaamsha baadhi ya abiria wenzako ambao wanakuangalia kwa jicho la kukushutumu na pia unajistukia ni kama wimbo wenyewe unakusuta vile kwa mazingira uliyonayo. Unajaribu kupotezea kwa kujichekesha lakini sauti inayotoka inakuwa ya ajabu kutokana na hofu uliyonayo.

Unaacha kuimba na kuiruhusu hofu iliyokushika itawale. Unawasha kitv unaangalia geographical location ulipo… ramani inakuonesha unapita kisiwa cha Bermuda.Kijasho chembamba kinakutiririka japo kuna AC. Unatamani ushuke.
Nafikiri wewe ulitaka kuzungumzia Bermuda Triangle na sio Bermuda Island.

bermuda-triangle-map.gif
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kama siyo kweli, naomba kueleweshwa, kwa nini hakuna ndege wala meli yoyote ambayo route yake inapita eneo hilo? Jaribu tuu kufanya utafiti.
 
Acha kujidanganya Kijana, Kama nataka kwenda Bahamas au Bermuda Island yenyewe, unafikiri huwa tunaendaje?
 
Story umeitunga vyema, ila scenery aiendani na ideology yake.
 
Olele huo uchunguzi ulioufanya nina mashaka nao....Nikuhakikishie yanayosemwa kuhusu Bermuda triangle juu ya mauzauza sii uongo. Wala hulazimishwi kuamini ni kweli kwani hata usipoamini haitabadilisha ukweli uliopo. Katika ile triangle kuna uhusiano na nguvu za giza na wazungu hasa american elites (walio kwenye occultic groups) wanajua na ni moja ya sehemu zao za kazi . Sayansi iliyoko pale ni spiritual....

Hamna kitu kama mauzauza au spiritual power pale hizo ni tungo, mimi nimepita mara kibao pale, mitikisiko ya ndege eneo lile husababishwa na mkondo wa hewa sawa tu na sehemu zingine zenye mikondo ya hewa, kuna uzushi mwiiiingi kuhusu Bermunda triangle.
 
Back
Top Bottom