Maajabu ya Kisiwa cha Bermuda

Socratic

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Posts
568
Reaction score
308
Uko ndani ya ndege. Kukiwa na utulivu mkubwa ambapo watu wengi wanaonekana kusinzia. Umejiegemea kwenye seat yako ukitafakari hili na lile.. Ghafla unaskia sauti ya kilio cha mtoto mchanga kwa mbali.. unageuka huku na kule na unajiridhisha sauti ile unayoiskia haitoki ndani ya ndege bali nje.

Unajiuliza mara mbili mbili.. unashangaa . Ghafla unajiskia ulazima wa kwenda haja ndogo, unapokaribia mlango wa choo unaanza kuhisi mle ndani ya choo kuna nyoka kibao. Unajipa ujasiri na kufungua mlango, mlango haufunguki. Unasukuma tena kwa nguvu mlango bado haufunguki.

Unapata hisia kuna nyoka mkubwa yuko mlangoni ndio maana mlango haufunguki.Unaamua kuahirisha tukio unarudi kukaa kwenye kiti chako, ile kukaa tu unakutana na boonge la mtikisiko (turbulent). unaanza kuhisi ndege inadondoka&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];unaangalia saa..ni saa 5 usiku na bado kuna kama masaa matano kabla ya ndege kutua.

Unafungua dirisha kuangalia nje ni giza totoro, unachokishuhudia nje ni mvua kubwa na radi, pia sauti ya kilio cha kitoto kichanga inasikika zaidi. Isitoshe unaskia mshindo mkubwa kwa mbali. Haraka unafunga dirisha.Unaamua kupambana na hofu kwa kujiimbisha,&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];Mbinguni..kuna makao mazuri sana.

unaangalia pembeni unajistukia umekuwa ukiimba kwa sauti kiasi cha kuwaamsha baadhi ya abiria wenzako ambao wanakuangalia kwa jicho la kukushutumu na pia unajistukia ni kama wimbo wenyewe unakusuta vile kwa mazingira uliyonayo. Unajaribu kupotezea kwa kujichekesha lakini sauti inayotoka inakuwa ya ajabu kutokana na hofu uliyonayo.

Unaacha kuimba na kuiruhusu hofu iliyokushika itawale. Unawasha kitv unaangalia geographical location ulipo&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; ramani inakuonesha unapita kisiwa cha Bermuda.Kijasho chembamba kinakutiririka japo kuna AC. Unatamani ushuke.
 
Kuna watoto wakali sana pale, ngoja mvua iishe niende tcra kuomba ruhusa/kibali cha kuwawekea hii video na hizi jpeg
 

nasikia ndege hazipiti hapo. Je ni kweli?
 
nasikia ndege hazipiti hapo. Je ni kweli?
nope.. its just a myth.. hizi stori nilisikia nikaamua kufanya uchukunzi kwa kusoma kwenye sites kadhaa na vitabu.. ni uwongo tu unakuzwa/unatengenezwa na watu na kuna watu/wazungu wametengeneza fedha nyingi kwa hii stori..
kwenye data za ajali za ndege na meli za marekani kuna ajali moja tu ya ndege tena ni eneo pembeni kidogo imewahi kuripotiwa na hakuna pengine popote imewahi kurekodiwa kuwa kuna ndege/meli imewahi kupotea maeneo hayo..
so ni uwongo tu..
 

Mkuu napenda sana kuckia habar ya ile triangle ambako ndege uvutwa
 
Mkuu napenda sana kuckia habar ya ile triangle ambako ndege uvutwa

ndo hiyo inaitwa bermunda triangle.. ni uzushi tu.. wazungu wameuza vitabu, wamecheza muvi nk. they make a lot of money out of that myth.. si kweli.. ni kama hadithi za nguva (samaki mtu)
 
ndo hiyo inaitwa bermunda triangle.. ni uzushi tu.. wazungu wameuza vitabu, wamecheza muvi nk. they make a lot of money out of that myth.. si kweli.. ni kama hadithi za nguva (samaki mtu)

Eti ndo kama nungwi hvi maji yanaingiia hapo
cjui mkipita ukiwa macho unapotea.
 
Sasa mbona hadithi yako haisemi kama na hao abiria wenzako hiyo hali walikuwa wanaiona au ni ww tu???????
 
Conciparancy iliyopo hapo inaaminika kuna Allien station hapo chini kwani miaka mingi iliyopita evidence inaonyesha kuna meteorite ilianguka hapo lakini mpaka leo haijapatikana so watu wanahusisha na alliens activities
 
Ila ni kweli ndege zinapotea na meli pia Nina list ya ndege na meli zilizopotea huko ngoja nikae sawa nitaziweka hapa
 

Uongo mtupu.
 
Hivi hizo mlienda kusoma ujinga?(in faiza foxy voice)
 
Kuna documentaries zinazoelezea juu ya Bermuda triangle na visiwa vyake kwa undani zaidi.
Kama ukiweza kuzipata utapata majibu yote juu ya Bermuda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…