Kwa kuongezea:
1. Kanisa Katoliki ndiyo Kanisa pekee ambalo mnyororo wake wa uongozi, tangu Mt. Petro, haujakatika mpaka leo.
2. Kanisa Katoliki ndilo the most conservative, lisilokubali kuendana na mabadiliko ya Dunia. Yesu, hakumteua mwanamke kuwa mtume, wala mitume wake hawakuwahi kumchagua mwanamke yeyote kuwa mtume, japo wakati wote walikuwepo wanawake waliojitolea maisha yako kutumikia Mungu, wao walipewa majukumu mengine, lakini siyo kuwa maaskofu au mashemasi. Ndivyo ilivyo mpaka leo.
3. Kanisa Katoliki ndiyo Kanisa pekee lenye historia a kumbukumbu zote kuhusu ukristo.
4. Kanisa Katoliki ndilo kanisa pekee ambalo watumishi/viongozi wake ndio kwa kupitia mikono na kauli zao, Mungu alitenda miujiza ya wazi, iliyothibitika kwa kila aliyekuwepo na hata na wanasayansi mashuhuri, mf. Miujiza mingi kwa mikono na kauli za Mt. Fransisco wa Aziz, Sista Fausta wa Poland, Padre Pio wa Italia, Mt. Ritha wa Kasia, Mt. Veronica, Muujiza wa Ekaristi Takatifu wa Lanciano,.
5. Kanisa Katoliki ndilo linalofuata maelekezo ya Yesu kwa vitendo, kama vile kutokuhukumu wengine, kutokupiga kelele, wala waumini wake kujionesha mbele za watu ili kutafuta sifa.
6. Kanisa Katoliki ndilo linaloshikilia nyaraka nyingi za historia ya ukristo, jinsi wakristo wa mwanzo kabisa walioishi nyakati za mitume walivyofanya katika kuuishi ukristo wao.
7. Kanisa Katoliki ndilo linalofuata liturujia ya wakristo wa mwanzo, wakifanya mabadiliko madogo sana. Kwa kadiri ya maandiko ya Askofu Ignatius, baba wa imani ni kwamba ibada ya wakristowa mwanzo ilifanyika siku ya kwanza ya Juma, liliyoitwa siku Siku ya Bwana au Siku ya kumega mikate. Ibada ilifanyika kwa utaratibu ufuatao:
a. Kuulizana na kuombana msamaha kabla ya kuingia hekaluni.
b. Kumwomba msamaha Mungu
c. Kumsifu Mungu
d. Kiapo mbele ya Mungu
e. Kumwabudu Mungu
f. Kubariki mikate
g. Kumega mikate
h. Kumshukuru Mungu.
8. Kanisa Katoliki ndilo lilitoa mwongozo kwa mifumo ya Dunia. Cannon law, ndiyo imejenga msingi wa mifumo ya sheria Duniani kote. Kanisa Katoliki chini ya uongozi wa Papa Cinstantin, ndiyo ulitoa mwongozo wa ndoa, ikiwemo kutoa tangazo wiki 3 kabla ya kufungidha ndoa. Vyuo vikuu vyote vya mwanzo vilianzishwa na Kanisa Katoliki, ndiyo sababu mpaka leo wahitimu huvaa majoho ambayo yalikuwa vazi rasmi la mamlaka ndani ya Kanisa.
NB: Kanisa Katoliki ndiyo msingi wa imani ya Kikristo, lakini pia dini ya kiislam iliiga mambo mengi toka Kanisa Katoliki.