Maajabu ya kampuni ya safe land world investment

Gidabed

JF-Expert Member
Jan 29, 2023
423
792
Wakuu natumai mpo salama otherwise poleni na majukumu.

Kuna kampuni moja inafahamika kwa jina la safe land world investment,inasadikika ni kampuni inayohusika na masuala ya uwekezaji ambapo unawekeza pesa yako na kuisubiria kwa muda wa siku takribani 170.

Kwa mujibu wa kampuni hii kiwango cha chini cha kuwekeza ni $50 sawa na Tsh 125,000/=.

Ukiwekeza;
125k kila siku utakuwa unalipwa 1875.

Ukiwekeza 200k utalipwa 3000 kila siku.

Ukiwekeza 400k utalipwa 6000
(Mathematically hapo ukifanya utagundua ni % ngapi utalipwa kulingana na uwekezaji wako).

NB: ukiwekeza pesa yako wanadai zikifika zile siku 170 unarudishiwa nusu ya ile hela yako uliyowekeza.😁

Na wanasema kampuni yao ni valid until 2027.

Hivyo nilikuwa naomba kama kuna mtu ana walau fununu kuhusu hii kampuni atusaidie.
Maana matapeli wamejaa sana mjini siku hizi
 
Mkitapeliwa msije mkasema hatukuwaambia

Make sure wanakuonyesha
Brella registration
TRA tax clearance
Registration etc
Je wanafanya baishara Gani inayowapa faida kiasi hicho amabyo inagawanywa Kwa wanachama?

Opinion are like rectum everyone got it
 
Hili nitalifanyia kazi
 
Wapelekee tupate kujua uhalisia.
Hata hivyo kuna wadau nawafahamu,wamewekeza huko na wakiingia kwenye account zao wanakuta mambo yapo kama mkataba ulivyokuwa umesainiwa.

Wameingiziwa pesa zao.

The problem ni kwamba soon watageukwa na wahusika
 
Baada ya ukimya wa muda mrefu wamekuja kwa njia nyingine watu wengine ila ni walewale tu!.
 
Daaah hii nchi vitu vingine vinafikirisha sana ok wacha tusubiri ushuhuda.

NB:kama pesa huna kazi nayo weka fixed account tu au kanunulie hisa
 
Wakuu natumai mpo salama otherwise poleni na majukumu.

Kuna kampuni moja inafahamika kwa jina la safe land world investment,inasadikika ni kampuni inayohusika na masuala ya uwekezaji ambapo unawekeza pesa yako na kuisubiria kwa muda wa siku takribani 170.

Kwa mujibu wa kampuni hii kiwango cha chini cha kuwekeza ni $50 sawa na Tsh 125,000/=.

Ukiwekeza;
125k kila siku utakuwa unalipwa 1875.

Ukiwekeza 200k utalipwa 3000 kila siku.

Ukiwekeza 400k utalipwa 6000
(Mathematically hapo ukifanya utagundua ni % ngapi utalipwa kulingana na uwekezaji wako).

NB: ukiwekeza pesa yako wanadai zikifika zile siku 170 unarudishiwa nusu ya ile hela yako uliyowekeza.😁

Na wanasema kampuni yao ni valid until 2027.

Hivyo nilikuwa naomba kama kuna mtu ana walau fununu kuhusu hii kampuni atusaidie.
Maana matapeli wamejaa sana mjini siku hizi
Watanzania Hatujifunzi tu na huu uwekezaji uchwara asee, Fanyeni kazi , Fanyeni biashara kwa maarifa , nguvu na bidii kubwa mtapata hela. hakuna hela inakukuta ukiwa umelala wake up
 
Ukiitwa kwenye fursa wewe ndo fursa yenyewe utapigwa tu. Lazima UPIGWE na kitu chenye ncha kali.

kitu kizito.jpeg
 
Hakuna deal nzuri ya hivyo DUNIANI, kaa nao mbali au kilio cha kusaga meno kinakuja
 
Back
Top Bottom