Maajabu ya daraja la Kigamboni!

Heshima mbele wakuu.... Naona mambo yamekuwa moto kweli kweli. Nadhani hapa kuna vitu tunavi overlook sababu nakumbuka mradi ulivyoanza (jamaa wa pale Ardhi Institute, panaitwaje tena sasa) walikuwa wanauangalia kama Dar es Salaam Coastline Development/Upgrading Project, daraja lilikuwa part of the mradi mzima. Sasa nadhani kuna maendeleo yametokea nakadhalika lakini haina maana kwamba tuache kuchanganua manufaa, gharama, aina ya kivuko (daraja,tunel)......

Hivyo nadhani haya ndio nionavyo mimi:
1. Aina ya kivuko (daraja au tunel):
Kwa muangalio wangu wa haraka haraka nadhani wale jamaa wa Ardhi walipendekeza daraja ili liwewe ku "FUSE-IN" na madhanri nzima ya bandari yetu ya Salama (manake ukiweka tunel hakuna kitu kitaonkana zaidi ya vijishimo pande zote mbili). Sisemi tunel halitakuwa na mvuto la hasha lakini nasema kwamba kuna uwezekano wale waliopendekeza na kutoa preliminary design waliangalia/walipendekeza daraja against tunel kutokana na sababu maradufu (inawezekana hata cost pia waliangalia). Swali ni kwamba je, inawezekana kubadilisha between the two? Jibu ni kwamba inategemea ni nini haswa ndio muhimum (Dar Coastal line development/cost)!! Hili nadhani linatakiwa kuangaliwa kwa upya sababu naona kuna more interest in this than initially thought!

2. Location ya kivuko:
Hapa ipo kazi kweli kweli. Hebu jiulize (kama tukijenga daraja) ni meli za ukubwa gani zinapita pale mahali (Linea Messina etc). Sasa kama tunataka kujenga daraja ambalo sisi wazalendo tunaweza kulitunza nadhani ni bora tuwa na kama lile la Mkapa kule Rufiji (fixed type). Sasa angalia ukubwa wa meli (headroom/height ya daraja) kwa kuzingatia urefu wa meli (high/low tide - at least 100 years history), majengo ya hapa Jijini (pale city centre, Kurasini wherever), Congestion ya Jiji pale city centre, disturbance ya wakati wa ujenzi nk.... Kisha jiulize je inahitajika ardhi kiasi gani kuweza kupata enough gradient both kwenye kupanda/kushuka (Dar na Kigamboni sides), wow... Si utani inahitajika atleast 1km on both sides, kwa daraja tu na access roads, sasa hebu liweke daraja hili pale City centre kisha jiulize vingapi vitabidi vipishe njia (BoT, State House etc)....... Do the math!

3. Kuhusu matumizi ya daraja (miguu, magari, baisskeli, etc):
Nadhani hapa kuna kuchanganya idhaa, muhimu sio nani analihitaji zaidi bali je, Daraja litajengwa na litajengwa wapi? Kwa umbali ulivyo lazima kutakuwa na njia za magari na pia wale waenda kwa miguu kama sisi. Sasa hata kama litajengwa Kurasini au City Centre still lazima kuwepo na miundombinu ya waenda kwa miguu pia. Jaribu kukaa Jangwani kuangalia kila asubuhi watu wangapi wanatembea kwa miguu kutoka Magomeni etc mpaka City Centre, itakuwa Kurasini mpaka town?

4. Swala la Pesa na Umuhimu:
Kwa mtazamo wangu ni kwamba ukizingatia Jiji linavyopanuka kwa kasi, daraja hili lilitakiwa kujengwa 5 years ago!! Kwa nini, hebu angalia idadi ya vianja tumeshapimiwa na Serikali kule Kigamboni, mahoteli, ma "bichi"......kisha geuka na angalia idadi ya meli zinapita pale feri kila siku. Wengi watasema suluhu ni kuongeza pontoon, ha ha haaaa.... "You must be joking" umeshawahi kuona madau palae feri yanavyopigwa vikumbo na "ma meli".... Sasa jiulize pale creek yenyewe ni ndogo wewe ukaongeza pantoni si utakuwa unatengeneza "death creek" leave alone delays kutokana na kupishana kati ya mitumbwi, meli, pantoni na offcourse vyote vyategemea kina cha maji (tide).....
Kuhusu pesa zitatoka wapi nadhani sio kitu cha kujiuliza saana, wote tunajua apart from Education/Afya/na mambo mengine meeengi, pia kuna swala zima la INFRASURUCTURE DEVELOPMENT!!! Hili la daraja lipo katika hilo la 3, Miundo Mbinu!!!

Sasa kama nilivyosema vyote ni vizuri lakini kikubwa ni kwamba "Je Serikali/vyombo vinavyohusika wameshafanya mchakato mzima wa nini kifanyike pale mahali kwa kuangalia current situation na mipango mizima ya kuendeleza Jiji la Dar Salaama?"... Tunaweza jenga daraja na ku create more problems than what we currently have!!

Naomba kuwakilisha!!!!!!!
 
Kunradhi.... Nikirudi kwenye mengine mawili:

1. Mkuu GT, tunangojea muziki wa kujengwa kwa darafj na mambo ya kauzibe.... Tafadhali tuambiwe ni kina nani, wapo wapi, na wanafanya nini kuzuia ujenzi wa daraja hili.........

2. Kuhusu Mhandisi/Kandarasi wa kujenga daraja hilo.... Mbona pale waJepu walipotoa pesa/kuchangia kujenga Kilwa Rodi wakamkatia pasi KONOIKE hatukupiga kelele sana, pia tuangalie Chalinze-Tanga, Dar-Mlandizi nk ambapo ni wa Denishi!! Kiutaalam Dutch wapo pina sana kwenye mambo ya Maritime Engineering manake ukiangalia kule kwao Rotterdam wamejituma kisawa sawa... Sikatai wao kujituma/kupewa tenda considered kwamba kwa vile ni mkopo lazima sisi kama walipaji tushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa kutafuta kandarasi/mhandisi, kisha mawazo yetu au kutokukubaliana na chohote katika swala hili lazima lisikilizwe kiutaalam na sio eti kwa vile hatujapewa "ka 10%" ketu.....

Hivyo, nadhani swala hili kabla sijasema tumepigwa changa la macho kuna mengi ya kuangaliwa (ukiwemo MUZIKI wa GT)............ For now, ngoja nijiwekee ka kinywaji niendelee kula wikendi taraaaatiiibuuuu!!!!
 


Masatu,

Hebu nenda ukaangalie tena hiyo sosi yako maana sidhani kama wadachi wanaweza kutoa an open ended promise ya 50%. Madaraja ni miradi mikubwa kutegemeana na design. Tunaweza jenga daraja la $50 million au la $1,000 million na 50% yake toka kwa kodi za wadachi itakuwa ni vitu 2 tofauti vya ku-discuss bungeni kwao. Hebu jaribu kudodosa zaidi ujue walichoahidi maana 50% ya anything haionekani kuwa realistic. Siku njema.
 

Nakubaliana na wewe asilimia 100. Miji mikubwa mingi kwa kutumia either main government au local government wameweza kufaidika na BOT. Toll Bridge and Toll road is very popular kwenye nchi zilizo endelea.

Tatizo la viongozi wetu upeo wao wa kufikiri ni finyu. Anaweza kusema aaahh kigambo tuspend pesa zote hizo kwa nini. Wanachosau ni kwamba Kigamboni ni beach area, maana more job will be created, jiji litapanuka na kupunguza msongamano in some extend, government itakusanya more mapato ( something which government need to do), tourism sector itaongezeka.

Sasa ukiwa na miwaziri ambayo akili zao ni 0% madhara yake ndio hayo. Wanachojua wao ni how much will it cost, and what percentage will i be able to grab. Wanashindwa kufanya long term benefit analysis.
 

DUA post inaonesha either unapenda kushindana au kukichangamsha kijiwe cha JF...
...napenda kukujibu swali laka kama ifuatavyo.
1. Ni Kweli tunahitaji Daraja Kigamboni...posts za baadhi ya member zikutoshe pia.

2. Priority its a personal judgment...on my side hio ni moja ya priority kwasasa kwa tunaoishi huko...kama unaishi Nje ya kigamboni au hujui umuhim wake...sikulaumu may be time will tell.

3. Gharama nafikiri baadhi ya Member wametaja. Pia hili jambo sio geni, Bungeni washajadili hili suala. na baadhi ya wabunge washawahi kumuuliza Mramba(enzi hizo miundo mbinu). inshort..Wadachi watatoa 50%(as per proposal iliyopelekwa huko), the remaining NSSF will cover.

Kuna economic benefits nyingi ktk Ujenzi huo, sema uwezo wako wa ku-analyse ni mdogo...
Swali lako la kulaumu eti study haijafanyika..nimekueleza kama wewe ni mtaalamu wa Civil Engineering weka proposal zako hapa JF na pia uwatumie wale wahusika...usikae kusema hakuna watu walofanya hio study au hadi wewe uwajue hao wataalamu?
 
Morani75,
Nitatofautiana nawe ktk hicho kipengele cha pili...Location unapojaribu kutumia meli kama ni sababu kwani yapo madaraja mengi sana yaliyojengwa ktk nafasi kama hiyo ama chini yake na katikati ya mji kwenye maghorofa marefu zaidi ya hayo yetu vipimbi.

Kumbuka tu kuwa tuna ufuko mrefu sana sambamba na barabara ya Ocean road nje kabisa ya Benki kuu, Ikulu na vyote ulivyovisema ambao unaweza kabisa bila ubishi kupata gradient na mapito ya meli hizo. Tatizo kubwa ni mwinuko wa tosha tokea upande huu na sii upande wa Kigamboni kisha daraja hujengwa kwa malengo ya baadaye kupunguza congestion na sio kufikiria wakati wa ujenzi hali majumba kila siku yanajengwa na congestion hiyo hutokea kwa muda...
Mkuu hapa kinachotakiwa ni kutazama solution ya Usafiri kwenda Kigamboni ambako kulingana na maelezo niliyoyapata wizara ya Utalii ina plan kuweka mahotel makubwa, viwanja vya golf na kadhalika ili kubadilisha mtazamo hali ya Utalii nchi kutotegemea zaidi mapori na Wanyama. Dubai ambayo haina wanyama wala mapori leo hii ina attract watalii wengi zaidi kuliko sisi kwa sababu Ndivyo tulivyo...Tunaendekeza fikra njozi za kufkiria kuwa Utalii ni Safari na nature hali kila nchi duniani ina nature yake, kisha tofauti ya nchi za kiafrika ni ndogo sana.
 

Pengine wewe ndio unapenda kufurahisha kijiwe.

Je, hilo faili ambalo ulikuwa unalipigia debe liko wapi?

And then again on your flip flop side ............... Priority as a nation or as an individual? I just happen to highlight to you that may be a tunnel could be appropriate, whether we obtain funding or not, that doesn't mean I support the idea or not.

Uwezo finyu ulionao kifikra na kukurupuka katika mijadala ndio unaokupeleka kusema mimi nalaumu kwamba hakuna study. Well, if there was any study (by any means) why don't you produce it for everyone to see? I don't need to be a Civil Engineer to know pumba unazoandika, or let alone to know that there wasn't any proper study subject to the matter.

Well you can be here trying to justify your comments but you should be responsible for what you write. Lete hiyo study sasa! au endelea kumsubiri GT akuletee faili mboga.
 

Nimeitoa:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=4560

Hizo ndio ndoto zetu. Upande mwingine wa sarafu tunaokataa kuuona ni huu hapa chini:


Nimeitoa kwenye link hii:
http://www.ehj-online.com/archive/2000/july2002/july4.html

Tunataka kuwa kama Dubai! tunajua ecological cost ambayo Dubai watalipa kutokana na vile visiwa walivyojenga? tunataka tunnel, tunajua gharama za ku'vent' hizo tunnels na kuhakikisha usalama wa maisha kama janga la moto likitokea? Tunazungumzia Toll bridges, tunajua watu wa Kigamboni ni wangapi wanaohangaika na hiyo sh 100 (?) ya pantoni. Let us keep it real, ndugu zangu na tusahau hizi ndoto za alinacha. Zinatuchelewesha katika safari yetu na kutukaribishia matapeli wa kitaifa. Nani anakumbuka mradi wa Jangwani?

Tukae, tutulie, tuvute pumzi na tuangalie hizi proposals kama kweli zitamsaidia raia wa kawaida wa Dar es Salaam. yule aishie Buguruni, si yule wa Masaki.
 
DUA sina Haja ya kubishana nawe...labda nikupe points 3 za ushindi...Lkna WAKATI NDIO UTAKAOKUPA MAJIBU...
alieanzisha Mada ni GT, akaahidi kuja na faili..may be hana au alikuwa anataka kuchokoza au bado yupo ktk Utafiti. So uamuzi ni mtu binafsi.. kuamini au kutoamini....Mbona MKJJ anaposema ana CD mnakaa mkao wa kula...na husemi CD mbovu...inakwaruza!!!


MCHUNDO..thanks kwa sources...na pia kwa comments zako. Kimsingi hatuna uwezo wa kuwa kama dubai, dubai yenyewe ni ndogo kuliko MKOA wa DSM...hivyo hatulinganishi in everything. Tunaangalia maeneo tu ambayo tunaweza iga. Hizo FLats 17 za [Mafuta House]!!ndio jengo moja tu tena mbwembwe nyingi hadi kufunguliwa kwake..Huko Sharjah tu ndugu zetu wanaokwenda kuchukua spear Mbovu...hizo 17 flats zipo Kibao, Kiongozi wao hana Muda kwenda kufungua hizo 17flats...so msingi wangu wa Hoja ni kuwa hatuwezi iga kila kitu kutoka kila Nchi, na pia si kweli Dubai imeendelea kuliko nchi zingine tumetolewa mfano tu.

Kimsingi Toll System kaka Mchundo si kwa watembea kwa Mguu, tena kwao wao itakuwa FREE kupita ktk hizo Daraja. Toll system kwa magari ambayo hadi mtu achukue gari, then huyo mtu hana DHIKI ya 100.
 

Nimeshindwa kukuelewa hapo kwenye nyekundu unataka kuelezea nini? Kuwa mafuta House ina flat 17 na Sharja wanazo kibao? kwa hiyo idadi ya flats ni kipimo cha maendeleo? Mbona flats ni aina moja tu ya makazi. Hizi zinapendelewa sana sehemu ambapo ardhi ni adimu ( si kuwa haipo lakini haipatikaniki kirahisi). Ulaya ( bara si visiwani) wana unatamaduni wa kuishi kwenye flats wakati marekani wanapendelea zaidi nyumba zilizosimama zenyewe. Uingereza wao nao ni row houses, semi detached n.k ndizo zinazotawala. Flats zilijengwa sana Uingereza (na marekani- huko wanaziita projects- angalia St. Louis, Chicago, New York) katika miaka ya sitini ili kujaribu kutatua tatizo la makazi kwa wale wenye kipato cha chini. Katika miaka ya themanini ilitambulika kuwa hizo flats zimekuwa ndio jaa la matatizo ya kijamii ( uuzaji wa madawa ya kulevya na uhalifu mwingine) na kuanzia hapo kwa wenzetu flats kama sehemu ya makazi zimekuwa zikiangaliwa upya. Flats zinafanikiwa zaidi pale ambapo watu wenye kipato cha juu wanamiliki ( Park Avenue, kando ya ziwa huko Chicago n.k) na sehemu kama za nchi za bara asia ambazo tatizo la eneo la kujenga ni kubwa mno na hawana choice isipokuwa kwenda juu. Sisi Dar es salaam kwa bahati mbaya tumechukua flats kama dalili ya maendeleo na hivyo kuharibu mandhari ya maeneo kama Kariakoo, Upanga, Masaki na katikati ya mji kwa kujenga ovyo ma'apartment blocks' yasiyo na mbele wala nyuma.

Point taken kwenye suala la toll bridges. Ni mara nyingi, kweli haya madaraja yanawatowaza wale wenye magari tu. Hii inawezekana kwenye nchi ambazo private car ownership ni kubwa au sehemu ambapo daraja liko strategically located kuunganisha sehemu ambazo watu wanatumia sana usafiri wa magari kwa binafsi au biashara. Kwa hali yetu, hivi sivyo. Sehemu kubwa ya wakazi wanaosafiri kati ya kigamboni na feri ni waenda kwa miguu au baiskeli. Magari ni sehemu ndogo ya traffic. Sidhani kuwa toll kutokana na haya magari peke yao yanaweza kufanya mradi ukawa sustainable. Kinachowezekana ni pengine manispaa iwekeze kwa makusudi kupanua makazi, maofisi na kadhalika upand wa pili ili idadi ya magari iongezeke. Zaidi ya hapo, bila shaka, watakaoendesha hilo daraja watakuwa hawana budi bali kujaribu kupanua wigo la mapato yao na kuwatoza pedestrians na waendesha baiskeli watakao tumia daraja leo! Cha muhimu ni kuwa solution ya hapo kiganboni si rahisi kama walioleta mada hii wanavyodhani. Inabidi uchambuzi yakinifu wa dhati uafanyike kabla ya kufanya maamuzi yeyote. Solution ni lazima ihusishe wale wanaotembea kwa miguu na sio wenye magari tu!
 

Mkandara, heshima Mkuu.... Naona hapo tunnaongelea kitu kimoja kutokea kwenye angle tofauti.... Nakubaliana nawe na ukisoma zaidi sijasema kwamba daraja halitufai wala pale mjini hapafai bali nilishauri kwamba (at the end of my first comments up there) tujaribu kuweka wahusika wote kwenye mchakato mzima... Nakumbuka mwanzoni mwa mpango huu "CONCEPT" ilikuwa ni kupendezesha Jiji letu la Salama, lakini sasa hivi ukiangalia congestion, developments (both Kigamboni na CBD) sidhani kama ule mpango wa mwanzo unaweza kuchukuliwa moja kwa moja (naona FM pia ameliweka hili hapo juu.....

Tukirudi pia kwenye swala la location nina concerns zifuatazo:
1. Construction traffic - Je tutaweza kukidhi hii traffic pale CBD incase we build it (as you are saying maeneo ya Ocean Road Hospital)?

2. Generated traffic - Ukumbuke kwamba once daraja likiisha, watu wengi waliokuwa wanatumia Kilwa Road kwende maeneo ya Mji Mwema nk wataamua kupita njia fupi na yenye uhakika.... Sasa hebu imagine current (with future growth factor) ya hapo CBD, jumlisha magari yote ambayo yataamua tu kupitia darajani yaendayo Kigamboni na hata wale wanaoenda mpaka Coast Region wote wapitie hapo CBD, unadhani patakalika hapo?? Tukumbuke pia kuwa kutakuwa na ruti za mabasi, malori etc!! Hii simaanishi kwamba daraja halifai hapo mahali lakini nasisitiza kwamba tuangalie options zetu za sasa na miaka kadhaa ya baadae

3. Kuhusu hilo la utalii na Dubai naomba nisilisemee sana lakini this does not make sense to me kwamba kujenga daraja kutaleta watalii.......

So bottom line is sipingi ujenzi wa daraja, bali nasisitiza kwamba TUNATAKIWA KUFANYA A DETAILED STUDY AMBAYO TUTAWASHIRIKISHA WATU WA KWENDA KWA MIGUU, WAPANGA ROUTE ZA DALADALA, MIPANGO YA RAPID TRANSIT SYSTEM, MIPANGO MIJI, WATUMIA MAGARI, WENYE MAOFISI, MAJUMBA, MAHOSPITALI KWENYE MAENEO HUSIKA kabla hatujaamua kuwekeza pesa.... Nadhani FM naye ameliweka hili nami naomba nisisitizie swala hili!!
 
FM...sijasema Flats ni maendeleo...ila nilitoa mfano kuwa kuna baadhi ya vitu hatuwezi kuiga ktk nchi yetu.Baadhi ya vitu nchi za watu ni vitu vidogo sana, ukiviweka TZ issue kubwa!!

Nakubaliana nawe kuwa Flats zetu hapa K/KOO zimejengwa bila Mpango. sisi TZ hatuna haja sana ya Flats...bado sehem kubwa ni Pori hivyo tunahitaji watu wanaopanga MIJI vyema.

Back to Daraja: I hope study imefanyika na Inaendelea kufanyika. kwa vyovyote iwavyo Daraja halitoweza kuwatoza Wapita kwa MIGUU...sijatembea sana duniani, ila kama una mfano wa sehem ambayo wapita kwa Mguu wanatozwa TOLL..please nijulishe!!!
 
So bottom line is sipingi ujenzi wa daraja, bali nasisitiza kwamba TUNATAKIWA KUFANYA A DETAILED STUDY AMBAYO TUTAWASHIRIKISHA WATU WA KWENDA KWA MIGUU, WAPANGA ROUTE ZA DALADALA, MIPANGO YA RAPID TRANSIT SYSTEM, MIPANGO MIJI, WATUMIA MAGARI, WENYE MAOFISI, MAJUMBA, MAHOSPITALI KWENYE MAENEO HUSIKA kabla hatujaamua kuwekeza pesa.... Nadhani FM naye ameliweka hili nami naomba nisisitizie swala hili!![/QUOTE]

Hichi kikao unachokisema kikali tusubiri!!!
 
Moran75,
Nimekuelewa mkuu ktk hoja zote na ndio maana nimesema kipengele hicho tu. Pia nimeeleza navyofahamu mimi na labda nikurudishe nyuma kidogo. Mji wa Dar es Salaam unafahamika kwa kitu kimoja kikubwa sana.. nacho ni kwamba kuna barabara moja tu toka katikati mjini kwa kila kitongoji chake. Si Ubungo, Kinondoni, Temeke, Buguruni wala Ukonga na sehemu zote hizi zilimewahi jengwa barabara mpya bila kufikiria sana matatizo ya muda (congestion) mfupi ambayo ni lazima yatakuwepo hata ikiwa ujenzi wa mtaro tu. Lakini baada ya kujengwa hizo barabara zimeweza kwa kiasi kikubwa ku handle traffic pamoja na kwamba planning ya mji wetu ni mbovu toka enzi ya Ukoloni.
Kwa hiyo ujenzi wa daraja hili uchukuliwe kama ni hatua moja ya kuondokana na tatizo la Usafiri kama vile tunavyosisitiza ujenzi wa barabara. Hizo congestion zote zitakuwepo kwa muda na baada ya ujenzi wa Daraja hilo kumbuka watu wote unaosema huenda na Kilwa road wanatokea mjini sio toka Kurasini, Mtoni ama Temeke. Hivyo basi hata kabla ya kushika njia hiyo ya Kilwa ni lazima wapitie maeneo ambayo unayazunguzia na imekuwa vigumu kwa waendesha magari na mabasi yetu kuweza kutoka mjini na pia kumbuka kuwa Kigamboni ndio sehemu pekee imebakia isiyokuwa na exit ya haraka (barabara) zaidi ya kuzungukia Mbagala.

Na kwa wale wanaodai hawaoni umuhimu wa daraja hili kwa madai ya kuwa haliwezi kuwasaidia Watanzania walio wengi... Hii inanishangaza sana kwa sababu sioni kabisa mantiki yake kwani nikitumia mfano wao naweza sema hatukuhitaji Airport ya kimataifa hata kidogo...Ni watu wangapi wanaoweza ku afford kusafiri kwa ndege licha ya jiwanja kubwa lililochukua eneo kubwa na hata kusababisha makazi ya wananchi walalahoi kuhamishwa bila matakwa yao.
Je, uwanja huo unamnufaisha nini Mtanzania maskini tunaye jaribu kumsema hapa, ikiwa mji wetu unapanuka na Kigamboni ambako mahotel makubwa yanajengwa kwa sababu ya kupanua Utalii nchini hasa ktk mji wetu mkubwa kuna kosa gani kimaendeleo. Bila shaka hatuwezi kujipima na nchi kama Dubai ama nchi yeyote ile kwa mapana ama gharama ya suti yetu hii mpya lakini haiwezi kuchusha Dar Es Salaam nayo ikavaa suti hata kama ni ya kutoka China...Hatufanyi kuiga ila ni umuhimu wa kurahisisha usafiri ktk jiji letu ambalo ni alama yetu kubwa nje na ndani.

Wakuu, huu ni wakati wa mabadiliko yale maswala ya fikra za Kijamaa ndugu zangu kidogo inabidi mwende na wakati. Miji yote duniani haifanani na kila nchi ina mji mkuu wenye maendeleo makubwa tofauti na miji mingine modogo ambayo pia ina sifa zake na pengine ujenzi wa vivutio tofauti na miji mingine. Na ndio maana leo hii tuna halmashauri za miji ambazo kazi yake kubwa ni kujaribu kuepuka ule mfumo centralization ambao kwa muda mrefu umekuwa ukitumika.
Daraja la Kigamboni ni muhimu sana pale mjini kabla ya kuwekwa vivuko vingine kwani ukitazama mji wetu wa Dar unazidi kupanuka na kuna eneno kubwa sana upande huo wa Kigamboni ambao sii wengi kati yetu ambao wanafahamu huko Kigamboni kunafanana vipi pamoja na kwamba ni karibu sana toka mjini kuliko vitongoji vinginevyo..
 

Bob need I say more? hapa nilipo napiga mluzi tu.....
 

Naona niingize senti mbili zangu.

Planning ya Dar es salaam tumeiharibu sisi wenyewe tusiwalaumu wakoloni. Master plans kwa kawaida ni dunamic na zinatakiwa ziwe updated kila wakati. Sisi hiyo hatujafanya. Building regulations, bye-laws zinazotuongoza mpaka sasa ni zile tulizorithi kutoka kwa wakoloni na kuzifanyia marekebisho kidogo. Hakuna master plan ya maana iliyotayarishwa toka ile waliotayarisha wakina Marshall Macklin Monaghan Limited kutoka canada katika miaka ya sabini. Hii master plan haikutekelezwa kama ilivyo kawaida yetu. Sasa nasikia mradi wa Sustainable Dar es Salaam project nao wanahangaika na ya kwao wanayoiita Strategic Urban Development Plan. Kwa hali hii development zinazofanyika Dar ( na kwenye miji mingine) zinafanywa on ad-hoc basis bila kuwa na malengo yaliyoainishwa katika Master Plan. Mfano ni hiyo njia ya mabasi ya kwenda kasi. Wakuu walienda Curitiba, Brazil wakaona rapid transit system yao, wakarudi nyumbani na kuwatangazia wananchi kuwa sasa mambo safi maana wataiga mfano wa wa Brazil bila kufanya feasibility studies au matayarisho mengine! Huko Curitiba, hii system imefanikiwa kwa sababu ni sehemu ya Master Plan. Hii system imelenga kumrahisishia usafiri mtu wa kawaida, kupunguza matumizi ya magari na kulinda mandhari ya mji. Kila kitu, kuanzia njia zenyewe, mabasi yatakayotumiwa, aina ya vituo vya kusimamia, urahisi wa kutumiwa na walemavu na nauli itakayofanya hayo mabasi yawe ndani ya uwezo wa watumiaji na vilevile kufanya mradi uwe sustainable viliangaliwa.

ktk Wikipedia

Vyote hivi vilichukua muda kupanga na mchango wa wataalamu wa fani mbalimbali walijumuishwa. Sasa angalia sisi tulivyo'approach' suala lenyewe. Feasibility study ilifanyika baada tu ya muwekezaji kudai, bila hiyo tusingefanya. Juhudi gani zimefanywa katika ubunifu wa vituo bora vya hayo mabasi n.k.?

Wataalamu kama wakina Morani wanapohoji haraka za kukimbilia hili daraja inatubidi tuwasikilize. Anachoshauri yeye ni kuwa tuhakikishe kuwa studies zote zimefanyika ili tutafute solution itakayotufaa zaidi. Sehemu ya hizi ni feasibility studies itakayojumuisha gharama za uendeshaji na namna ya kulipia. Kama litagharamiwa na toll, basi tuhakikishe kuwa kweli yako hayo magari ya kutosha. Kuwepo kwa mahoteli ya kitalii hakuna maana hii maana haya generate traffic kubwa kiasi hicho. Mfanyabiashara yeyote aliye makini ni lazima kwanza anahoji kama investment yake itarudi. Wenzetu ambao mnasisitiza tukurupukie solution hili ndio wenye mtizamo wa miaka ya sitini ambayo yametuachia tembo weupe kibao! Wakati huo ndio tulijenga viwanda kwa kukazania zaidi siasa na siyo biashara. Mfano wako wa kiwanja cha ndege si sahihi. Uwanja wa ndege umejengwa ili kutuunganisha na nchi nyingine pamoja na sehemu nyingine za nchi yetu. Usafiri wa anga hauwezi kuwepo bila uwanja wa ndege. Na hata wenyewe haujengwi kwa sababu ya sifa tu bali unaongozwa na mtizamo wa kibiashara. Lengo letu la kuwa na uwanja ni nini? Ni kuwa hub, kushindana na Nairobi? Kitu gani kitafanya mashirika ya ndege ya kimataifa yatumie uwanja wetu? Vivutio gani tutaweza kuweka ili wasafiri ( wa ndani na nje)hao waje? Au tuwe end destination tu na domestic hub ya hapa kwetu? Maswali kama haya ndiyo yanaongoza uamuzi wa kujenga uwanja wa ndege na sio prestige tu. Tunachokiomba sisi, ni kuwa yote haya yafanyike vile vile katika maamuzi ya kujenga daraja. Tutumie wataalamu wetu na wengine kutoka nje kuliangalia suala hili kwa undani zaidi.

Ushindani baina ya miji ni kitu cha kawaida na cha kusisitizwa. Lakini uwe ushindani unaoongozwa na mipango iliyo realistic. Tusipende platitudes. Kuita Arusha Geneva au Dar es Salaam Vancouver hakuta badili ukweli wa Unga Limited na Uwanja wa fisi. Tutumie vizuri rasilimali zetu kwa kuwekeza kwa makini. Hatuna luxury ya kufanya experiments. Tutayarishe Master Plan ituongoze katika maendelezi ya mji wetu kabla ya kujiingiza kichwa kichwa kwenye miradi kama hii. Ni hayo tu.

Bin Maryam! Kweli nilikimbia umande lakini middle school zilikuwa kiboko ndugu yangu!
 


MKuu Mkandara ulioyaweka hapo ni majibu mazuri sana...ila naona wengine wameshindwa kuelewa,ila usichoke kuwaweka sawa!!! na wengine unaweza waacha kuwajibu ONLY TIME will TELL.
 
Wizara Inawahitaji Wachina Maana Kwa Rushwa Wanajulikana Na Tena Huwa Wanatamba Wakifikiri Ni Biashara Halali Kwa Nchi Za Africa Lakini Naikumbusha Tu Wizara Iangalie Yasije Yakatokea Ya Sam Nujoma Road
 
My good Tanzania Citizens, my adorable Dar Es Salaam residents, and my Bad Government, do you really tell me that Government of Tanzania failed to build a bridge to Kigamboni? Unataka kuniambia kweli hata wameshindwa kuyapa makampuni mengine binafsi zabuni ya kujenga daraja la kuunganisha Kigamboni na Dar kweli? Au wanasubiri walete maafa tena na kuunda kamati za uchunguzi? Feri zenyewe ni mbovu kupita maelezo.. kilasiku zinakosa uelekeo... Kweli unadhani wakiingia mkataba na makapuni binafsi yajenge daraja hilo kisha yatoze ada hizohizo za feri kwa muda wa miaka 5-8 kisha serikali inalimiliki na kuwa bure itashindikana kweli? Watu hawatajitokeza? Yaani ninaoingea kwa machungiu sana, kwasababu kweli kama kungekuwa na daraja Kigamboni... nadhani ungekuwa ni mji mwingine tosha wa kitalii, kwanini Serikali halilioni hili?....
 
Hili daraja nalo limeishia wapi?

GT nimenunua server mpya kutunza dosier kama hizi. Leta vitu mkuu bado nakusubiria hapa. JF ambako kila kitu kinapitia kwanza kabla ya kuwekwa kwenye news bongo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…