MzalendoHalisi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2007
- 4,710
- 1,660
Kama ilivyozoeleka ..hao Wadachi wakitoa Grant basi hapo hakuna ulaji wa maana kwa Watz!
Kwa kifupi ni kukosa tu uzalendo na kuweka kwanza maslahi binafsi mbele!
Maana sasa miaka zaidi ya 15 kweli Tz tunashindwa kufikia maamuzi jambo dogo hivi.. je makubwa tutaweza?
Mkulu GT,
Ni kweli kuna kiwingu kikubwa kimetanda katika sakata zima la ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Last time I checked serikali ya Holland wamekubali kutoa grant ya 50% ya cost ya daraja lote. For reasons best known to themselves, wizara ya Miundo Mbinu pamoja na wizara ya Fedha wamekuwa wakikwamisha kwa makusudi juhudi za ujenzi, inasemekana wizara ya Miundo Mbinu wapo radhi daraja lijengwe na watu wengine (mbali na wadachi) na serikali igharamie in FULL.
Sasa swali ikiwa kuna 50% grant yes GRANT sio LOAN ( condition ni kuwa kampuni za kidachi tu ndio zishindanie tenda)ni vipi watu wanang'ang'ania serikali igharamie in FULL?
Kwa mara ya mwisho nilipofuatia swala la daraja hili niliambiwa kuwa serikali ilikuwa imekwisha amua litajengwa Kurasini badala ya pale Kigamboni kutokana na kwamba pale Kivukoni hakuna nafasi ya kutosha kuweza kupandisha mwinuko wa daraja.
Majuzi tu nilipata habari kuwa ujenzi huo wa Kurasini umesimamishwa baada ya kuzingatiwa kuwa daraja lilitakiwa zaidi lijengwe maeneo ya mjini pale Kivukoni na sio Kurasini kutokana na sababu nyingi za kimsingi.
Bila shaka yawezekana ikawa hii ndio sababu kubwa ya usitishaji wa mpango wa ujenzi wa daraja la Kurasini kwani kama kuna mabadiliko ya kurudisha offer ama mchoro uwe wa Kivukoni badala ya Kurasini na gharama zake. Mtakumbuka kuwa niliwahi sema kuwa daraja linaweza jengwa kabisa kwa kuitumia barabara ya Ocean road kupata mwinuko na nguzo kuu za daraja.
Binafsi sioni sababu kabisa ya kuweka kivuko cha daraja Kurasini, tutakuwa hatujatatua kabisa tatizo la usafiri na nina hakika bado wananchi wataendelea kutua usafiri wa maji (Panton) kuliko kwenda hadi Kurasini.
Dua soma thread...
kama wewe huoni priority sawa..ila sote tunajua Kigamboni Kivuko muhim....may be unaishi nje ya DSM au hujawahi kufika kigamboni...
Tumeweka Wizara kila moja ifanye kazi yake...kulala kwa idara moja ya serikali kusifanye idara zingine kulala, au kuamka kwa Idara moja kusifanye watu waone Gere/WIVU au hao wenzao watapata credits/UJIKO...Pesa wachangiaji wamesema zitatoka wapi so far hicho kivuko ninavyoelewa itakuwa TOLL kwa kipindi Fulani kurudisha pesa, then itakuwa FREE
Mie si mtaalamu wa Mambo ya Ujenzi...watu wa Civil Engineering wanaweza kusema juu ya kipi kifanywe...[tunnel or bridge]kama wewe mtaalam basi andika mchanganuo maalum kuwashauri wahusika...na pia unaweza iweke hapa JF.
Sijasema issue ya wivu as per ulivyoelewa[labda uwe mtendaji ktk wizara zilizotajwa, kama haupo basi Haumo ktk WIVU]...Nilikusudia juu ya wivu ni kati ya Idara na Idara. Kuna mambo yana tegemeana kiutendaji, NSSF wamesubmit hio proposal yao ya Ujenzi, hawezi jenga hadi Wizara ya Ujenzi ipitie, na pia Wizara ya Fedha na Wizara zingine...ukiangalia NSSF wanachoangalia ni kuwekeza, wizara zingine wanaangalia maslahi..sasa ukichunguza kwa undani kuna mgongano wa ki-Maslahi!!!
Dua kama hunijui mie si mtu wa kukurupuka kama wewe, na kama sina la kuongea huwa nakaa kimya hata wiki, kuangalia wengine wanazungumza nini..sio kujiongezea posts, then nianzishe thread ya kupengezana!!!
Tumsubiri GT kama mwanzilishi ambae anasema atatuletea Faili zima[/SIZE]