Maajabu: Manispaa Kigoma yakaimisha 'DMO' darasa la saba

Kweli umeamua kujilipua ndugu yangu...sasa kama umehisi wanatabia ya kutumia ushirikina unatuhakikishiaje kuwa hiyo wiki ijayo utakuwepo kabla hawajakushiri na wewe?
 
Wivu wa kike?

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu wewe sidhani kama ni daktari au muuguzi labda una hirizi za damu ya uganga na ushirikina maana una majungu makali sana yaani ukisoma maandiko yako walahi ukipewa sumu unaweza muua mwenzio ! Watu mliosoma kwa kuunga unga ndo mnakuwaga hivyo kwani kaharibu nini mwenzio ? Kumbe wote mlitengeneza vyeti sasa povu la nini kwa mwenzio ? Shubaaaaamiiitiii !!!! Shindwa shetani la kigoma lisilowaza maendeleo kizizi chako kime-expire karew !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa halmashauri ni kawaida tu hasa zile ambazo zpo remote area STD VII ndo wanaendesha halmashauri
 
Manispaa ya Kigoma Ujiji imemkaimisha Mganga mkuu wa manispaa mwenye elimu ya darasa la saba..Filimbi ya haki inaweza kuripoti
Mganga mkuu huyo Abigael Mika KASUMANI hana cheti cha form four,alianza kama mfagizi wa ofisi kisha akanunua cheti cha form four na kujiendeleza kimagumashi na kujipachika cheo cha AMO.

Lakini wakati wa ukaguzi wa vyeti vya form four yeye na Muuguzi mkuu wa manispaa(ARK) walijifungia katika chumba na kuchukua mafaili yao na kunyofoa vyeti vya form four(vilivyokuwa feki) na kuacha vya darasa la saba

Hata hivyo uhakiki uliwapita salama na kwa kutumia ushawishi wao wanawake hawa majabali wawili waliwahonga waheshimiwa flani wawili na kufanikiwa kumshawishi Diwani mmoja mpenda rushwa kuwapigia chapuo na kuhakikisha Kasumani anabaki kukaimu nafasi ya mganga mkuu baada ya aliyekuwepo Peter NSANYA naye kutumbuliwa na kuondolewa utumishi wa Umma kwa kughushi

Katika hali ya ajabu sana Abigael karudi kukaimu na sasa inadaiwa yeye na muuguzi mkuu huyu darasa la saba wanatumia nafasi husika kuwakomoa wabaya wao,kuhamisha wafanyakazi wanaojifanya 'wajuaji' na kuingilia mafaili ya watumishi wengine kuhakikisha hawapewi nafasi hiyo ikibidi kwa kutumia 'ushirikina' na mambo mengineyo..

Sisi wafanyakazi tulioondolewa katika utumishi wa umma kwa kukutwa na vyeti visivyo halali TUNASHANGAA SANA KWA SABABU TULINUNUA VYETI WOTE NA ABIGAEL HANA CHETI CHA FORM FOUR..ANAKUWAJE KAIMU MGANGA MKUU?

WIKI IJAYO TUTAELEZA NAMNA ALIVYOFANYA UFISADI KATIKA MANUNUZI YA IDARA KATIKA MWAKA WA FEDHA ULIOPITA NA NAKALA YA NYARAKA HUSIKA ILI UMMA UJUE NAMNA SINTOFAHAMU MANISPAA NA JINSI MKURUGENZI JJ MBOYA ALIVYOZUNGUKWA NA MAFISI..
Haya ni Majungu tujiepushe na majungu, kwani hapa ninavyokupinga ni kuwa Dr. Nsanya amesharudishwa kazini baada ya serikali kujiridhisha kuwa tuhuma iliyokuwa ikimkabili kuwa alighushi cheti cha kidato cha nne si za kweli na yupo kazini alisharipoti. Kuhusu hao wengine taarifa walizotoa ni kuwa wao ni la saba na nchi hii ilishawahi kuajiri darasa la saba na hadi leo wapo kwenye system za serikali. Kwa makala hii imeonesha wazi kuwa wewe ulinunua cheti cha kidato cha nne(4) na inaonesha wazi umeshatumbuliwa hapo ulipo na hao unawaonea wivu bado wapo kazini, pole sana kwa wizi wa kuiba cheti na nakushauri uache wivu nafasi ya kurisiti ipo wazi kwako.
 
Nashangaa ndugu zangu wa Kgm MAJUNGU!! Dr Abigael namfahamu nilisoma nae chuo, najua kuwa aliajiriwa mwaka 1984 na Halmashauri moja hapo Kgm baada ya kumaliza chuo cha waganga Maweni. Baadae alienda Musoma chuo cha Waganga na Bugando!!!!!! Lakini mkumbuke UDMO Sio kutibu tu na uongozi unakuwa ndani ya mtu, nidhamu, ukweli, uchapakazi,uwajibikaji nk. nk. Ndio maana wasomi hawakai Kgm majunguuuu!


kwa maelezo haya... nilijua wengine watakuja na taarifa zaidi...
 
Majungu hayo, anajituma, Ni mchapakazi . Anaaminika.
Mheshimiwa kaimu DMO chapa kazi. Kaza uzi mti wenyewe matunda ndio unaotupiwa mawe.
Mie Nipo Lindi siwajui ila machapisho ya majungu Ni kamahayo.
Mheshimiwa kaimu DMO huwezi kumridhisha kila mtu hata Mungu kuna wanao mlalamikia .


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom