ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,041
- 49,720
Serikali kuu haijatenda fair iweje halmashauri mpya ya Tunduma ilitaka kuanza ujenzi wa majengo ya utawala kwa pesa za vyanzo vya halmashauri zaidi ya billion moja ikazihamishia kujenga hospital wakati hawajaleta pesa za kujengea admn.block ila huko kwingine wametuma?Mleta uzi hakika amekurupuka nina mashaka na uwezo wake wa kufikiri, kwanza unapoishutumu Halmashauri kwamba kuna fedha zimeibwa au kutumiwa vibaya lazima uwe umefanya uchunguzi na kujiridhisha kwamba mradi huo umetengewa bajeti kiasi gani na zimetumika kiasi gani na je thamani ya fedha inaendana na kazi iliyofanyika? Na je umejengwa Kwa shughuli za ukumbi au matumizi mengine lakini Kwa sasa unatumika kama ukumbi Kwa muda?
Huwezi kuanza kuwashutumu viongozi kabla ya kufanya uchunguzi wa kina na unao Uhuru wa kuwauliza endapo Una mashaka na jambo lolote unaless otherwise utwambie kwamba uliwahoji viongozi na hawakukupatia ushirikiano, najua hukufanya hivyo ukaamua kukurupuka kuja kuweka upupu wako hapa.
Kwanza unaweza kukuta wewe unawashutumu viongozi wa Halmashauri lakini wanaoujua ukweli wanawapongeza viongozi Kwa kujenga hata hilo jengo uliloliona si kitu kuliko baadhi ya taasisi ambazo hadi sasa zinakodi kumbi za mikutano Kwa gharama kubwa Kwa siku(zaidi ya laki 5 Kwa siku)
Kwa faida yako kama ulivyoambiwa na mmoja wa wachangiaji hapo juu Linajengwa jengo la Utawala la Halmashauri lenye hadhi ya nyota 5 na ndani yake lina ukumbi wa kisasa.
Ninakushauri kabla ya kupost chochote JF fanya Kwanza uchunguzi sio kupost upuuzi wako na kuwapotosha watu.Kwa faida yako ukumbi wa jengo la Utawala la Halmashauri na ukumbi wa Halmashauri angalia picha, na ujenzi unaendelea tatizo lako umeona kwamba habari inayokufurahisha ni huo uliouita ukumbi lakini sio ujenzi wa jengo. View attachment 835929
Pesa zinazolipwa kama pango ya jengo la kukodi ni karibu robo tatu ya hizo huoni hii ni hasara?