KING KIGODA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2018
- 3,756
- 2,999
Nimekuwepo kwenye utumishi wa umma huu mwaka 4 sasa katika halmashauri moja huku mkoani Morogoro.Tangu nilipofika katika halmashauri hii 2020 nilimkuta mkurugenzi ambaye tayari alikuwepo hapa tangu 2018.
Kwa muda huu wa miaka 3 ambao nimekuwepo hapa,nimeona na kusikia dili nyingi za kifisadi zikifanyika kupitia mtandao wa maafsa waliotengenezwa na mkurugenzi huyo ili kupitisha dili chafu. Mbinu anayotumia kuwateka maafsa hao ni pamoja na kuwatengenezea mazingara magumu ya kiutendaji na kimaslahi, huku akiwajengea uoga kwa kuwakaripia na wengine kutowapa majukumu yao ya kiofisi kabisa.Haya mambo aliyafanya kwa muda wa kati ya mwaka 1 hadi 2 kwa mujbu wa watumishi niliowakuta hapo,na kwa wale waliojishusha na kukubali kupelekwapelekwa kwa matakwa yake,ndiyo baadae walikuja kuwa njia ya kupitisha dili zake chafu mpaka leo.
Mimi kwa ushuhuda wangu mwenyewe nimethibitisha kupitia Afsa usafirisha wa halmashauri ambaye yeye alibaki na msimamo wa kufuata kanuni na taratibu za kazi yake,akiewekwa pembeni na na nafasi yake kupewa Afisa mmoja wa elimu msingi,yeye mwenye taaluma yake amekuwa msoma magazeti ofisini bila ya jukumu lolote mwaka wa 2 huu sasa.
Kwa kupitia TO wa mchongo,pesa kuanzia za matengenezo ya gari,mafuta,vipuri n.k zinapigwa na magari ni mabovu siku zote.Utaratibu wa kisheria wa ukaguzi wa magonjwa ya gari na matengenezo haufuatwi tena na gari zinatengenezwa mitaani kwa gharama ndogo huku zimetolewa pesa nyingi.
Wito wangu ni kwa Rais Samia, asijiamini kwamba huku chini pako vizuri na kumbe ndiyo kunaufisadi mkubwa unaosababishwa na hawa wakurugenzi kwa kukaa halmashauri moja muda mrefu na kupelekea kutengeneza cheni za upigaji.
Kifupi ufisadi ni janga kubwa kwa sasa.