Maagizo ya Waziri Mkuu kwa Ma DC na Ma DED Nchi Nzima

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI WOTE NCHINI, AMPONGEZA MKUU WA WILAYA MSTAAFU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametoa Maagizo Kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Wote nchini kwenye Halmashauri zao Kusimamia Kutokuwepo kwa Michango Holela inayo kera Wananchi na kushindwa kufanya Shughuli nyingine hali inayopelekea Wanafunzi kuondolewa mashuleni.

Mhe. Majaliwa Ameyasema hayo Jun 1, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Mhe. Ally Kasinge alilotaka kujua “Je Serikali haioni Umuhimu wa kupitia sera ya Elimu bila malipo ili michango ya Ulinzi, Shajala pamoja na michango ya Chakula iwe ni jukumu la serikali kwa dhana ile ile ya kuwapunguzia gharama wazazi au walezi” Mhe. Kasinge

Majaliwa amesema serikali inaendelea kutekeleza Sera ya Elimu bila Malipo (bila Ada) kwa lengo la kuwapunguzia wazazi michango mingi ambayo ni holela na kuleta usumbufu ambapo amesema serikali hupeleka fedha kwenye Kila Halmashauri kwaajili ya kuwezesha shule.

“Serikali inapeleka fedha kila Mwenzi kwenye kila Halmashauri kwaajili ya kuwezesha shule zetu za sekondari, Wakuu wa shule na uongozi wa shule kuweza kutumia kwenye maeneo ambayo walitarajia sana kupata michango kutoka kwa Wazazi” Mhe. Majaliwa
 
Attachments

  • IMG-20230601-WA0156.jpg
    IMG-20230601-WA0156.jpg
    34.5 KB · Views: 2
  • IMG-20230601-WA0157.jpg
    IMG-20230601-WA0157.jpg
    43.9 KB · Views: 2

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI WOTE NCHINI, AMPONGEZA MKUU WA WILAYA MSTAAFU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametoa Maagizo Kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Wote nchini kwenye Halmashauri zao Kusimamia Kutokuwepo kwa Michango Holela inayo kera Wananchi na kushindwa kufanya Shughuli nyingine hali inayopelekea Wanafunzi kuondolewa mashuleni.

Mhe. Majaliwa Ameyasema hayo Jun 1, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Mhe. Ally Kasinge alilotaka kujua “Je Serikali haioni Umuhimu wa kupitia sera ya Elimu bila malipo ili michango ya Ulinzi, Shajala pamoja na michango ya Chakula iwe ni jukumu la serikali kwa dhana ile ile ya kuwapunguzia gharama wazazi au walezi” Mhe. Kasinge

Majaliwa amesema serikali inaendelea kutekeleza Sera ya Elimu bila Malipo (bila Ada) kwa lengo la kuwapunguzia wazazi michango mingi ambayo ni holela na kuleta usumbufu ambapo amesema serikali hupeleka fedha kwenye Kila Halmashauri kwaajili ya kuwezesha shule.

“Serikali inapeleka fedha kila Mwenzi kwenye kila Halmashauri kwaajili ya kuwezesha shule zetu za sekondari, Wakuu wa shule na uongozi wa shule kuweza kutumia kwenye maeneo ambayo walitarajia sana kupata michango kutoka kwa Wazazi” Mhe. Majaliwa
Nikajua ameagiza Waalimu walipwe posho ya vipindi na maudhurio darasani kama Wabunge wanavyolipwa posho ya kikao Bungeni.
 
Sidhani kama serikali utaweza kuleta hela ya chakula kila mtoto .....labda gharama zingine sio chakula ....wazazi tujipinde kwa hilo
 
Shule ya serikali inachangisha wazazi pesa ya mlinzi, rim,ya kujenga uzio ya kulipa walimu waliojitolea.
HII elimu Bure ni Sanaa tu
 
Back
Top Bottom