Maagizo 9 aliyotoa Rais Samia kwenye ziara yake Mkoa wa Manyara

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa maagizo tisa katika ziara yake mkoani Manyara ikiwemo kusisitiza kwamba

1. Serikali itaendelea kukopa kwa lengo la kuchochea maendeleo ya haraka. na alisema kuwa maendeleo ni gharama na kuyafikia kunahitaji njia mbili ambazo ni kodi na mikopo hivyo alitutaka wananchi kulipa kodi maana mikopo hiyo lazima irejeshe.

2. Wananchi waendelee na kilimo serikali itaboresha umwagiliaji na mbegu.

3. wananchi wa Mayara waache vitendo vya ukatili kwani vimekithiti.

4. wakulima na wafugaji watakiwa kuacha migogoro.

5. wananchi waagizwa kutunza mazingira kupanda miti badala ya kuikata.

6. wanasiasa wasichochee wananchi kuvamia ardhi kwa nia ya kupata kura.

7. hakuna ukweli wowote wananchi wakisajiliwa TRA itawadai kodi.

8. Mabwawa na maziwa mkoani Manyara tathmini ya mazingira.

9. Serikali kutioa huduma ya maji kulingana na fedha atakayolipa mtumiaji.

Ukisoma kwa umakini utagundua Rais Samia Suluhu ndiye yule kiongozi watanzania wengi tulitamani kua nae maana maendeleo yote haya yanamgusa mwananchi moja kwa moja acha nisema Rais Samia Suluhu ni kiongozi bora zaidi haijawai tokea
 
Tatizo la Tanzania walipa kodi ni 10pc. Hapo nimeweka wafanyakazi na wafanyabiashara.

Msiongelee VAT maana hiyo haikwepeki
Maendeleo yanaitaji pesa lazima tulipe kodi ili tuishi katika miundombinu iliyobora na tupate huduma zote muhimu katika ubora kama ilivyo sasa
 
Kwa kuwa wananchi wametakiwa kutekeleza maagizo aliyoacha Rais, ambayo kimsingi serikali inaenda kusimamia. Wananchi wa Manyara tuone wao wataanzia wapi!!!!!
 
Ukisoma kwa umakini utagundua Rais Samia Suluhu ndiye yule kiongozi watanzania wengi tulitamani kua nae maana maendeleo yote haya yanamgusa mwananchi moja kwa moja acha nisema Rais Samia Suluhu ni kiongozi bora zaidi haijawai tokea

Kama kawaida kusifia Rais
Kuna mmoja aliitwa hadi mkombozi mungu

Hii nchi inahitaji watu wakusifia kama nyie wapungue
 
Back
Top Bottom