Maafisa 90 wa magereza wahitimu shahada ya uzamili Chuo cha Uhasibu Arusha

Maafisa 90 wa magereza wahitimu shahada ya uzamili Chuo cha Uhasibu Arusha

Joined
Feb 4, 2026
Posts
11
Reaction score
9
Simple blog post Instagram Post_20260207_142256_0000.png
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Lusetula (Mbunge), amewatunuku shahada ya uzamili wahitimu 2,250 wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakiwemo maafisa na askari 90 wa Jeshi la Magereza, waliosajiliwa katika mwaka wa masomo 2024/2025 katika fani mbalimbali zikiwemo amani na usalama pamoja na uongozi na utawala. Mahafali hayo yamefanyika Februari 06, 2026, katika ukumbi wa Ngurudoto jijini Arusha.

Akizungumza katika mahafali hayo, Mhe. Lusetula amewataka wahitimu wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutumia elimu waliyoipata kama chachu ya kuleta maendeleo ya taifa.

“Nendeni mkaitumie vyema elimu na maarifa mliyoyapata ili kuchochea maendeleo ya taifa, zingatieni misingi ya amani na muwe wazalendo,” alisema Mhe. Lusetula.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa Eliamani Sedoyeka, alimshukuru Mkuu wa Jeshi la Magereza kwa ushirikiano wa dhati uliopo kati ya chuo hicho na Jeshi la Magereza kupitia programu mbalimbali zinazowawezesha maafisa na askari kupata elimu itakayowasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao, hususan katika shughuli za urekebishaji wa wafungwa na mahabusu.

Aidha, Mrakibu wa Jeshi la Magereza (SP) Amos Atanas Maheri, ambaye ni miongoni mwa wahitimu wa shahada ya uzamili katika Chuo cha Uhasibu Arusha, ametunukiwa zawadi maalum baada ya kufanya vizuri zaidi katika masomo ya uongozi na utawala.
 
Hizi ajira za serikali unaingia ukiwa flat, masomo ya juu utayapata ukiwa ndani ya ajira. Ni na ajira ni ngumu kusoma hadi kufikia ngazi za juu, na kwa kawaida kadri unavyopanda juu kielimu ndivyo na masomo yanavyokuwa rahisi, digri unapata huku unaiona kirahisi tu, hakuna kufeli juu. Ngoma nzito iko kidato cha nne kuvuka kwenda cha tano
 
Kwa kuzingatia zile 48 Laws of Power hapo ni Fitina Mode Activated

Maboss wanawaona threat kwa vyeo vyao!!
 
Back
Top Bottom