Maadili za siku hizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maadili za siku hizi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Roulette, Nov 4, 2011.

 1. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  wazazi wa siku hizi tuna mtihani mkubwa sana wa fuwafunza watoto wetu maadili (nimetafsiri maadili kama values).
  Zamani ilikua rahisi sababu jamii nzima ilikua na maadili sawa na mzazi anampa mtoto yale yale maadili alipokea kutoka kwa zazazi wake mwenyewe, na mtoto akileta ubishi anarudishwa nafasi yake kwa adhabu kali sana. Ila leo tunaishi katika tamaduni nyingi sana ambapo unashindwa kumbana mtoto kama tulivyo banwa sisi. Upande mngine pia bila kumuandaa mtoto atashindwa kushirikiana na wenzie, na waalimu au na watu wasio wa familia yake.
  Dunia ya leo ina mambo mengi sana na saa zingine hatujui tuchukue nini tuache nini. Mwalim akimchapa mtoto fimbo anashtakiwa polisi. Ukishangaa mtoto wa jirani anamvalia baba yake bikini waende swiming pool unaonekana mshamba etc. Nini sahihi na ni kipi cha kufanya?
  Nimegawa maadili katika kundi nne na nimejaribu kuonesha ni kundi zipi zinaruhusiwa kubadilika, kwa kiwango gani, na nani anaruhusa ya kubadilisha.
  1. Kwanza kuna maadili yanao kubalika na walimwengu wote, kama uaminifu, umoja, upendo, imani nakadhalika. Mwambie mtoto kua anatakiwa kutumia maadili haya kama nguzo ya maisha na kila atakapo kua katika changamoto atafute jibu litakalo husisha maadili haya.
  2. Pili kuna maadili ya Dini na imani zetu. Hizi zinaweza kua tofauti na maadili ya dini zingine. Mwambie mtoto aheshimu sana maadili ya dini yake ila aheshimu pia dini za wengine sababu ndio njia pekee ya watu wa dini zingine kuheshimu dini yake. Hapa sitaki kuweka mfano kama mnao naomba mnichangie. Maadili haya kwa kawaida hayabadiliki ila yanaweza kutafsiriwa na wachungaji (sheikh, paster au father)
  3. Tatu Kuna maadili ya nchi zetu. Mwambie mtoto kuhusu historia ya nchi yake na msaidie kuipenda nchi yake na maadili ya raia mzuri. Tofautisha propaganda za siasa au za serikali na maadili ya nchi. Maadili haya ni yale yale kwa raia wote, wanawake kama wanaume, wazee kama vijana, magamba kama manyoa... Mfano: Sisi kama raia hatutakiwi kuchoma bendera. Bendera letu ni mali na lina thamani kubwa sababu kuna mashujaa wengi walimwaga damu kwa kulilinda. Pia kama raia tunatakiwa kulipenda taifa letu na kulitetea kila tuendapo etc.
  4. Nne, kuna maadili ya mila, kabila na familia zetu. Haya ni maadili tuliorithi toka kwa wazee. Mwambie mtoto kua maadili haya yalisaidia ukoo kufika hapa tulipo na yalizaliwa kutokana na mazingira mbali mbali. Hivo, ikiwa atataka kujua matumizi ya maadili hayo katika mazingira fulani, asome kwanza mazingira na afanye mwenyewe tafsiri ya maadili kutokana na mazingira. Anaweza pia kuongea na wazee wa familia kwa kupata mwanga zaidi. Mfano: Babu yake alikua na wake 5, baba yake akawa na wake 2, je yeye anaweza pia kuoa mke zaidi ya mmoja? Au Mama yake alikeketwa, na dada zake pia. Je akiacha kukeketwa ni makosa?
  5. Alafu kuna mchanganyiko wa maadili ya nyumbani (hapo kwenu). Mzazi lazima umwambie mtoto wewe mwenyewe unatumia nguzo gani, kanuni gani, desturi gani na maadili gani kuiongoza familia yako? Katika viwango vyote hivyo chukua 2 au 3 kwenye kila daraja zinazo kuongoza zaidi kuliko zingine na zifanyie kazi. Ni muhimu sana mtoto aone kua mzazi unachukulia maadili ya familia kwa kiwango cha juu sana. Na ikiwa kwa sababu moja au nyingine unahitajika kumkaripia au kumuadhibu mwanao, kumbuka kumwambia ni adili gani la familia amevunja. Na mwambie kua akiwa mkubwa, atajenga zakwake mwenyewe (mfano wazazi wanapo mwambia mtoto kua hapo nyumbani hakuna kurudi baada ya saa 2 usiku, na kama hutaki tafuta nyumba yako. adili linalo husika hapa ni heshima na limeunda kanuni la saa ya kurudi nyumbani)
  Kwa kumaliza, nitatoa mfano wangu binafsi: Nakumbuka Baba yangu alitwambia nyumbani kua wakubwa wanapewa kipaumbele juu ya wadogo. Shule nikafundishwa 'women and children first'. Nilipofika nyumbani nikataka kujifanya najua zaidi ila baba alinipa kiti na akanieleza kua hayo sio maadili yetu kama waafrica, na kama wanafamilia yake. Kwetu sisi ni muhimu heshima iuwiane na miaka na akanipa sababu nyingi zikiwemo uzowefu wa maisha, heshima na kadhalika. Nikamuuliza kama mwalimu alikosea na kama naweza kumwambia mwalimu kua sisi waafrika tunawapa wazee kipaumbele. ndio kama hapana sababu adili lingine la familia yetu ni uvumilivu wa maadili ya wengine. Alisema naweza kabisa kumwambia kuhusu adili zetu na kutoa sababu ila nisimkosoi katika adili zao. Kama atapendezwa na zetu, atabadili mwenyewe.
  Kwa wale wenye mifano ya maadili haya, au wenye aina zingine nawakaribisheni kunichangia au kunikosoa. Asanteni.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mmomonyoko wa maadili ni janga lingne hli
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kuendelea na hoja iliyopo tunaomba maana(definition) ya zamani

  Zamani ni lini?

  Pia "jamii nzima" ina mipaka gani?
   
 4. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hi Gaijin. Nikisema zamani namaanisha one generation ago (kama miaka 20, 30 hivi, kwenda nyuma). Na nikisema jamii nzima namaanisha 'community'. Sio scientific article, ni maongezi tu. Kama kuna mushkil hapo we kosoa tu na twambie neno gani lingefaa zaidi.
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ni katika kuelewa tu ili tuweze kuchangia.

  Hapo umesema

  lakini ukatoa mifano mingi sana ya kuwa kulikuwa na values tofauti hata enzi za ulivyolelewa (dini tofauti, imani tofauti, na kisa cha mwalimu wako na baba) kiasi cha kuwa tunashindwa kuelewa hiyo "jamii nzima" basi inamaanisha nini?
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Anyway

  Kwa zamani ya miaka 20-30 nyuma, upande wangu sioni tofauti yoyote na wakati huu wa sasa

  Nimelelewa mjini kulikokuwa na watu kutoka makabila tofauti wenye mila na tamaduni tofauti. Nimefungua macho kwetu kuna TV na Video player ambayo ilinikutanisha na tamaduni za nje tokea nikiwa mtoto. Baadhi ya wanafamilia na jirani walikuwa wakisoma nje ya nchi, na wakirudi likizo kila mwaka au nusu mwaka na "mambo" kutoka huko nje

  Jirani yetu wa nyumba ya pili, kuliko na mtoto ambae unaweza kusema amezaliwa "homosexual". Familia zetu ni marafiki wa karibu kwa sababu mdogo wake wa kike (mwenye umri sawa na mimi) ana sickle cell na alihitaji damu (O negative) takriban kila mwezi kutoka kwa kaka yangu (na kwangu). Huyo kaka homosexual (na wadogo zake) hadi leo tunawasiliana na huko nchi za nje aliko inasadikiwa "ameolewa".

  Shule nako kuna waliokuwa hawaji wiki nzima, kisa wanachezwa na kanga moja tu. Kuna wengine walikuwa wanakeketwa/kutahiriwa (wanawake).


  Kwa hiyo kwa upande wangu sioni kipya baina ya enzi za miaka 20-30 nyuma na sasa. Wala hakukuwa na jamii nusu seuze nzima iliyokuwa na maadili sawa.

  Kwenye malezi nnachokumbuka kikubwa ni kufundishwa ama kuelekezwa kwa reasoning na sababu zenye ushahidi kuwa "hiki ni chema" na "hiki ni kibaya". Kwangu sababu ya "sio maadili yetu" pekee hainitoshelezi.

  NB: Nna dada yangu aliyetoga masikia sehemu 3 kila moja, miaka 15 nyuma. Kwa sababu alitaka kufanya hivyo na wazazi walishindwa kumpa ushahidi kuwa kufanya hivyo ni "kubaya".
   
 7. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  What I meant ni kwamba familia mbali mbali zinazohishi sehem moja (in the same community) zilikua na maadili ya kufanana. Ila leo watu mnaweza kua na undugu wa karibu, au mnaweza kua na same socio-economic background ila maadili yakapishana. Sijui naeleweka...
   
 8. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Thread nzuri sante..

  kweli waweza mfundisha mwanao maadili, maarifa na mifano mema ya maisha
  wakati wa udogo. ila jinsi akuavyo naye anagundua njia zingine au anaishi maisha
  ayatakayo au ayapendayo. Na katika hayo mafarakano ya maisha anaweza kutoka nje
  ya ulicho mfunza....

  Dunia ni nyumba ya kila mtu siku hizi..
  Nikimaanisha maadili, tamaduni , maarifa na vingine vingi
  vimechanganyikana. Hope for the best ...
   
 9. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Pia unatandawazi na teknolijia vimechangia kwa kiasi kikubwa kubomoa maadili yetu
   
 10. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  u .com umewaharibu vijana
   
 11. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  nafikiri si kumfunza maadili bali mjengee uwezo imara wa upima kila afanyapo maamuzi; nadhani itasaidia katika makuzi yake.........kujua hasara na faida kabala hajajitumbukiza kweny e kitu chochote kiwe chema ama kibaya
   
 12. JICHO LA 3

  JICHO LA 3 JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utandawazi unachangia sana
   
 13. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160


  3. Tatu Kuna maadili ya nchi zetu. Mwambie mtoto kuhusu historia ya nchi yake na msaidie kuipenda nchi yake na maadili ya raia mzuri.

  Kwa sasa hili halipo na wala halitakuwepo, historia ya nchi yenyewe haieleweki, kuipenda nchi ambayo wachache wananufaika na wachache hawajui watakula nini, utamwambiaje mtoto aipende nchi wakati yeye mwenye wala hajui future yake? nchi ambayo tabaka la walicho nacho na wasionacho ni kubwa.

  Tuliipenda tanzania wakati wa miaka ya sabini, tukiimba ( Tanzania na kupenda kwa moyo wangu) the song was real coming from the moyo, hapakuwa na tofauti kubwa kwa walicho nacho na wasio na kitu. tulikuwa tukiheshimu hata bendera ya taifa na wimbo wa taifa, sasa hivi wimbo wa taifa hauna tofauti na mdundiko na hiyo bendera ni kama pazia la mlangoni tu.

  Nne, kuna maadili ya mila, kabila na familia zetu.
  Hii nayo shida tu.
  Watoto wanazaliwa wanawasikia baba na mama wakisalimiana goodmorning, januari mpka januari hakuna safari za kijijini, likizo watoto wanapelekwa kuona wanyama au kupumzika comorro na nairobi, asilimia karibu 60 ya watoto wa kitanzania hawajui kuzungumza kikabila, bibi au babu wakiwana shida wanaambia waje mjini, wao inawalazimu kuongea kiswahili ili watoto wawaelewe.

  5.
  Alafu kuna mchanganyiko wa maadili ya nyumbani (hapo kwenu).

  Hili nalo mzozo
  kutokana na ugumu wa maisha, baba anatoka nyumbani asubuhi sana na mama naye vile vile, muda wa kuridi ni usiku, hakuna mwenye muda wa kuangalia watoto wana ishi vipi kiamaadili, watoto inabidi wajifunze kwa kuona mtaani na kusikia ya mtaani. ukipakia dala dala utakuta mwanafuzi kakaa kwenye siti, wewe mtu mzima umesimama yeye wala hashituki.   
 14. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Umesema kweli kabisa ila nchi yetu au familia zetu kua mbali na maadili ya mwanzi sio sababu ya kuishi bila maadili. Nchi kama nchi haijaharibika chochote, Tanzania bado ni ile ile, ila muongozo na mazingira ndio yameharibika. Hivi unadhani improvement itatoka wapi kama sio kwa wananchi? Na wananchi hao lazima waipende nchi yao na walipende taifa lao.
  The same applies to maadili ya mila. Concept ya modernity inataka kila kitu cha kitamaduni kitupiliwe mbali ila ukweli ni kwamba utamaduni huu ulisaidia traditional societies zetu kusurvive as a civilisation toka karne ya kwanza. Sijasema modernity ni mbaya moja kwa moja au traditional values ni nzuri zote ila kuna traditional values nyingi zinaweza kusaidia katika maisha na zitamsaidia mwanao ikiwa atazitumia.
  Pamoja na ugumu wa maisha au kutokua na wakati mwingi wa kuongea na watoto lazima kuna rules and regulations hapo nyumbani, Umeziunda vipi? what are the core values that govern you and your family? Lazima utakua umezichota toka maadili in general hapo juu na kujitengenezea 'core list' ya values zako. tumia mfano wako kumwelewesha mtoto namna gani values zinasaidia katika maisha ya kila siku. katika wakati huo mdogo mkiwa pamoja jioni onea nae. Mweleze kuhusu uaminifu. Mweleze kuhusu uwajibikaji, uvumilivu na kadhalika...
   
 15. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante Gaijin kwa kutupa mfano wako binafsi. Umeongea zaidi kuhusu familia yenu na kwa kweli mnaonekana mlikua na values nzuri kama tolerance, compassion, wazazi waliheshimu view points ya watoto na kadhalika. Swali langu hili hapa: ni familia yako yote (upande wa aunts na uncles) ambayo ilikua hivo? Sijui kama 30 years ago ulikua nchini au nje ya nchi ila naweza kukwambia kua homosexuality ilikua haikubaliki kirahisi iwe kwa madili za mila, za dini au za kifamilia. Hata leo bado ni tabu ila kuna watu wengi zaidi wamekua tolerant. Huwezi kusema the way citizen related to their country then ni sawa na the way they relate to it today... kuna mabadiliko kiasi na mzazi wa leo anatakiwa kua a bit more critic in selecting maadili kuliko yule wa 30 years ago ambae alikua more or less na a default set of values.
  Kitu kingine ninachoamini mimi (ila kila mtu yuko huru kuamini vinginevyo) ni kwamba kuna vitu unaweza kumwachia mtoto afikirie mwenyewe kipi kizuri na kipi kibaya ila katika miaka ya mwanzo lazima um-inculcate 'core values of humanity' na ikiwa ataenda kinyume na hizo ni muhim kumkaripia na kumpa adhabu.
   
 16. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unamaana hakuna values unatakiwa kumfunza mtoto? Nadhani uzuri wa binadam ni kwamba tunaweza jenga wisdom on other people's experience, na ndio utajiri wa mtu mwenye maadili. Unataka mtoto wako ajaribu kuishi bila kuwasaidia bonadam wenzie hata akiwa na uweze, hadi pale ataona ubaya wa tabia yake alafu ndio aje arekebishe na kuanza ku-apply compassion?
  Nadhani pamoja na kumsaidia kujenga uwezo wake wa ku-assess situation ni muhimu awe na value kadhaa za msingi. NImesema hapo mwisho 9maadili ya familia) kua ni set ya maadili kila mtu anajijengea kwa kutumia maadili za realms zingine na ni lazima uongee kuhusu choice zako na mwanao ili akija kutoka chini ya amri yako ajue pia namna ya kutumia maadili yalio kutwa na namna ya kujiundia list ya maadili yatakayo msaidia maishani.
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,177
  Trophy Points: 280
  ufafanuzi wa msamiati wa maadili bado ninauhitaji..........
   
 18. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Makuzi tu hayo.
   
 19. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nilisema hapo mwanzo tunazungumzia maadili kwa maana ya 'values'
   
 20. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kuna mada iliyofanana na hii na nakumbuka niliweka maangalizo haya:
  [Kila zama ina "watoto wake wa siku hizi". Mimi leo ninalalamika watoto wangu hawafati ninayotaka, ninagomba, "watoto wa siku hizi". Baba yangu alikuwa ananigomba na kulalamika "watoto wa siku hizi", na yeye pia alilalamikiwa na baba yake "watoto wa siku hizi"].

  Kuna kisa kilitokea kwa jamaa zangu wa karibu. Binamu yangu alipachikwa mimba. Shangazi yangu alichofanya nikulivumilia lile, aliwaunga mkono mpaka wakamaliza masomo yao, ndio badae wakaoana (mpaka leo wako pamoja). Walipata mtoto wa kike, akiwa kidato cha nne naye akapachikwa mimba. Baba na mama yake wakaja juu kuona mtoto wao amewaaibisha, wakataka kumfukuza nyumbani. Shangazi aliwaita na kuwakumbusha kile ambacho "pengine walikuwa wamekisahau", kuwa na wao walifanya hivyo hivyo lakini yeye (Shangazi hakuwafukuza) badala yake aliwaunga mkono mpaka wakamaliza masomo.

  Ninachotaka kusema ni kuwa mara nyingi yule aliye baba au mama anaweza kuona watoto wake wanapotoka, iwe generation yoyote ile. Ktu cha kufanya nafikiri, ni kujaribu kuwalea watoto wetu katika mazingira tuliyonayo sasa. Tuwe flexible kidogo kwa kuangalia ulimwengu tunaoishi. Tuwalee watoto wetu zaidi kwa maadili ya ndani ya nyumba bila ya kutumia Mkono wa Chuma. Na zaidi, tuwalee kwa reasoning, kwa majadiliano na mawasiliano. Tusing'ang'anie tu HAPANA wala kwa NDIO kwa sababu MIMI NIMESHASEMA IWE HIVYO. Ikiwa HAPANA au NDIO mweleze mtoto kwa nini, msikilize, jadiliana naye, anaweza kuona na kukubali sabau zako au wewe kukubali zake.
   
Loading...