Maadili za siku hizi

Asante Gaijin kwa kutupa mfano wako binafsi. Umeongea zaidi kuhusu familia yenu na kwa kweli mnaonekana mlikua na values nzuri kama tolerance, compassion, wazazi waliheshimu view points ya watoto na kadhalika. Swali langu hili hapa: ni familia yako yote (upande wa aunts na uncles) ambayo ilikua hivo? Sijui kama 30 years ago ulikua nchini au nje ya nchi ila naweza kukwambia kua homosexuality ilikua haikubaliki kirahisi iwe kwa madili za mila, za dini au za kifamilia. Hata leo bado ni tabu ila kuna watu wengi zaidi wamekua tolerant. Huwezi kusema the way citizen related to their country then ni sawa na the way they relate to it today... kuna mabadiliko kiasi na mzazi wa leo anatakiwa kua a bit more critic in selecting maadili kuliko yule wa 30 years ago ambae alikua more or less na a default set of values.
Kitu kingine ninachoamini mimi (ila kila mtu yuko huru kuamini vinginevyo) ni kwamba kuna vitu unaweza kumwachia mtoto afikirie mwenyewe kipi kizuri na kipi kibaya ila katika miaka ya mwanzo lazima um-inculcate 'core values of humanity' na ikiwa ataenda kinyume na hizo ni muhim kumkaripia na kumpa adhabu.

1. Familia yangu ilikuwa hivyo na shangazi na wajomba wengine walikuwa kama hivyo wengine tofauti na hivyo (hii ina maanisha kuwa hakukuwa na default values wakati huo pia).

Enzi hizo kuna watu waliamini wasichana wasisome na wengine walitaka wasome ila kidogo, na wengine walitaka wasome sawa na wanaume. Wapo waliowaozesha watoto wao kwa vizee vya miaka mingi wake wa pili, wengine waliamini kuwa wasichana wana haki ya kuishi vile wanavyopenda.
Wapo waliopiga bakora watoto wao kwa makosa wafanyayo wapo waliokuwa hawaijui bakora ni nini maishani mwao

2. Sina kumbukumbu ya hali ilivyokuwa zamani zaidi ya miaka 30. Ila zamani ya miaka 20 nyuma ndio hiyo kuliko na "shoga" na sikumuona kuwa persecuted in any way. Unapozungumzia ku relate na nchi hata sielewi unazungumzia kitu gani hasa.


Kilichobadilika ni kuwa enzi hizo ulikuwa wewe mtoto na sasa wewe ni mlezi kwa hiyo tunataka kujifariji kuwa sisi ulezi wetu mgumu kwa kuwa hakuna default set of values. Hata zamani hazikuwepo
 
Back
Top Bottom