Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,436
- 4,151
Toka lini mashekhe wakaunga mkono maaskofu? mara nyingi hizi huwa ni pande mbili zinazokinzana, sijui ni kwa nini. Lakini mwisho wa wote ukweli utajulikana whether ni hao mashekhe au maaskofu
Kuna wakati nimetokea habari za viongozi hawa wakifanya kazi pamoja km katika kufuatilia athari za mazingira katika migodi, mapambano dhidi ya ukimwi, mauaji ya albino, ukeketaji, kuombea taifa amani, n.k. Hivyo ndugu zangu tujihadhari sana na wanasiasa waliofilisika hasa wa nyakati hizi ambao wakisaidiwa na mafisadi wananunua viongozi wa dini kuimarisha ajenda zao muflisi zinazoelekeza taifa kwenye hatari kubwa.
Hakuna ubishi kwamba hivi sasa kuna kitu kimeharibika sana ndani ya chama tawala kinachopelekea kukumbatiwa na kuenezwa kwa hoja ya udini katika kila suala muhimu kwa maisha ya watanzania. Nasikitika zaidi kwamba inawezekana hata UwT wanatumika kupepea cheche za moto huo ili kutuondoa kwenye mantiki na umakini wa kushughulikia matatizo yetu kistaarabu. Baadhi ya viongozi wa dini (zote) wanatumika kama mamluki. Tuamke kulipinga hili kwa nguvu zote.