CCM yawataka Maaskofu wavue majoho... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yawataka Maaskofu wavue majoho...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 9, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  CCM: Maaskofu vueni majoho

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu,
  Arusha;
  Tarehe: 8th January 2011


  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha kimewataka maaskofu wote na viongozi wengine wa dini mkoani hapa, kuvua majoho ya kazi yao na kutangaza kuingia katika siasa.

  Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema hayo jana mbele ya waandishi wa habari wa Jiji la Arusha na kuwataka maaskofu hao kuacha kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.

  Chatanda alisema, kitendo cha maaskofu kusema hawamtambui Meya wa CCM Arusha, Gaudence Lyimo kimewashtua na hakiwezi kuachwa hivi hivi.

  Alisema viongozi wa dini wanapoingilia masuala ya siasa ni ukiukwaji wa majukumu yao hivyo bora wavue majoho yao na kuingia kwenye ulingo wa siasa kama alivyofanya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

  Chatanda ambaye ndiye anatajwa kuwa chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha, hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa kama Mbunge mkoani Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa wenyewe.

  Chatanda ambaye alikuwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole alisema kazi ya maaskofu ni kuelekeza njia za imani na kuwataka waumini kuwa wacha Mungu na si kushabikia siasa.

  "Sisi kama viongozi wa CCM wa Mkoa wa Arusha tumesikitishwa na kauli za maaskofu hao na tulitegemea kabla ya kutoa tamko lao wangetuita sote na tukatoa maelezo yetu na hapo ukweli wangeupata lakini kusema uchaguzi haukuwa halali si sawa."

  Hata hivyo, alisema yeye kama Mbunge, alipangiwa na chama chake kuwa Arusha na hivyo, ataendelea kuwa diwani wa CCM Arusha hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo na chama chake.

  Akizungumzia makundi ndani ya CCM ambayo pia yanampinga hasa kutokana na kumtuhumu kusababisha CCM kushindwa Jimbo la Arusha, alisema wanaCCM hao hawajui wanalosema hivyo wanapaswa kusamehewa.

  Juzi Maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba hawatampa ushirikiano meya huyo.

  Walitoa tamko hilo wakati walipokuwa wanalaani hatua ya Polisi mkoani Arusha, kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano ya amani ya Chadema na hivyo kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 20.

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  CCM waache unafiki....................Maaskofu hao hao baadhi yao waliposema JK ni chaguo la Mungu walitukenulia meno.............mbona CCM hawakusema Maaskofu wavue majoho na kujiunga na siasa?
   
 3. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ni jambo la ajabu kidogo, Mkeo hata kama ananuka kikwapa huko chini bado wewe hutahisi na kuuona uvundo huo
   
 4. k

  kipupwe Member

  #4
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walichokifanya Maasko wa Arusha ni sahihi. Ya Mary Chatanda ni maneno ya kisiasa ambayo ni porojo.

  Hebu ajiulize, Waziri mkuu alipoenda kuongea na viongozi wa Dini ilikua ni siasa? Au Rais JK alipoenda luongea na Papa ilikua ni Siasa?
   
 5. G

  Godwine JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  nadhani naomba na maaskofu waitishe maandamano ya amani nchi nzima kupinga unyanyasaji huu wa arusha
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huyu Mama anajiona ana nguvu sana?
  Anadhani kauli yake inatiliwa maanani na watu wangapi?...she is just a click, na sauti yake inaishia Magomeni!:-*.
  Ni katika viumbe ambao Arusha inajutia kuwahi kuwapata!
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Anamtegemea EL.

  Amesahau yaliyomkuta mama yetu wa kambo.
   
 8. A

  August JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Naona baba yake Makamba kaona akae kimya yeye sasa anataka kuvaa hilo joho, anataka kumpa tabu pinda ya kwenda kuomba radhi kwa maaskofu wa Arusha sasa.

  Naona huyu mtoto/bibi ana radhi ya wakubwa wake, maana yeye na maaskofu ni watu mbalimbali ni sawa sawa mbingu na ardhi. Asione kuwa na hiyo nafasi akajio yuko sawa nao, na hili suala sio la kisiasa, bali ni la kibaradhuli. Madiwani wa CHADEMA ni wengi kuliko wa CCM, halafu unafanya uchaguzi kinyemela, halafu unafikiri hili ni jambo la kisiasa, infact hata hao CCM ili kutuliza amani inabidi wamuhamishe huyo mama mara moja. Na huyo mkurugenzi wa jiji ambaye ndio msimamizi wa uchaguzi.

  NB: ikiwa kitu cha wazi kama hiki kina chakachuliwa, je uchaguzi mkuu ambao waliondikishwa, waliopiga nk vina kuwa nyuma ya pazia, uchachuliwa wake si utakuwa mkubwa?
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  maaaskofu wameingia hapo kwa kuwa kuna watu waliopoteza maisha..tulitegemea CCM mkoa iongelee namna ya kuzika wafu ...au kupekeka rambirambi na kuudumia majeruhi..........
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  (nilimskiliza uyo mama).

  CCM wala hawana uzuni kuna watu wamekufa. wanachojua wao uchaguzi umekwisha anayeona kulikuwa na kasoro aende maakamani.

  kwenye notebook yake akuna ata seemu aligusia abari za watu kupoteza maisha au ata kuonesha masikitiko kwamba kuna watu wamekufa. akili yake imajaa ccm = ulaji; ulaji = ccm.
   
 11. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Acheni upuuzi, kwani hii ni mara ya kwanza polisi kuuwa kwenye mitafaruku ya kisiasa hapa TZ? Hao watu wawili mlio watoa sadaka ni makelele chungu mzima! Mi naona CDM ni taasisi ya kanisa au vice-versa!
   
 12. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashauri CCM wampe Ulinzi huyo Mama maana mimi watu wa Arusha na wajua sana namna wanavyowathaimini Viongozi wao wa Dini halafu mtu mwingine tu anakuja na kuwabeza hadharani itakula kwake. Na zaidi watu wa Arusha ni wacha Mungu na wapole sana lakini wakigeuka hawasikiagila mnadi swala wala la Mhadhini Huyo Mama akae akijua hilo.
  Lakini hebu wan JF nipeni CV ya huyo Mama tusijekuwa tunmhukumu bure kumbe sio yeye.
   
 13. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha kimewataka maaskofu wote na viongozi wengine wa dini mkoani hapa, kuvua majoho ya kazi yao na kutangaza kuingia katika siasa.

  Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema hayo jana mbele ya waandishi wa habari wa Jiji la Arusha na kuwataka maaskofu hao kuacha kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.

  Chatanda alisema, kitendo cha maaskofu kusema hawamtambui Meya wa CCM Arusha, Gaudence Lyimo kimewashtua na hakiwezi kuachwa hivi hivi.

  Alisema viongozi wa dini wanapoingilia masuala ya siasa ni ukiukwaji wa majukumu yao hivyo bora wavue majoho yao na kuingia kwenye ulingo wa siasa kama alivyofanya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

  Chatanda ambaye ndiye anatajwa kuwa chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha, hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa kama Mbunge mkoani Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa wenyewe.

  Chatanda ambaye alikuwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole alisema kazi ya maaskofu ni kuelekeza njia za imani na kuwataka waumini kuwa wacha Mungu na si kushabikia siasa.

  “Sisi kama viongozi wa CCM wa Mkoa wa Arusha tumesikitishwa na kauli za maaskofu hao na tulitegemea kabla ya kutoa tamko lao wangetuita sote na tukatoa maelezo yetu na hapo ukweli wangeupata lakini kusema uchaguzi haukuwa halali si sawa.”

  Hata hivyo, alisema yeye kama Mbunge, alipangiwa na chama chake kuwa Arusha na hivyo, ataendelea kuwa diwani wa CCM Arusha hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo na chama chake.

  Akizungumzia makundi ndani ya CCM ambayo pia yanampinga hasa kutokana na kumtuhumu kusababisha CCM kushindwa Jimbo la Arusha, alisema wanaCCM hao hawajui wanalosema hivyo wanapaswa kusamehewa.

  Juzi Maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba hawatampa ushirikiano meya huyo.

  Walitoa tamko hilo wakati walipokuwa wanalaani hatua ya Polisi mkoani Arusha, kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano ya amani ya Chadema na hivyo kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 20.
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  Adhabu ya anayeuwa mtu mmoja na aliyeuwa mia au zaidi uzito wake ni ule ule duniani na hata kwa Mungu......sijui inakuwaje wewe unabeza vifo vya wanaadamu wenzako [eti wawili]....bila kuongelea wale 40 ambao wanaendelea kuugulia na risasi kwenye miili yao.........unasema ni kelele!!!!!
  unaonaje ungekufa wewe......au angekufa mtu wako wa karibu kabisa ....pia bado ingemfaa mtu kubeza.......!!!...usishangilie kifo cha mwanaadamu hata akiwa mmoja
   
 15. kagumyamuheto

  kagumyamuheto JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Tuzingatie maneno ya busara hapa chini kabla ya kutoa misimamo yetu. nimenukuu ktk thread ya jana.
  Kadogoo said
  Re: Maaskofu watoa tamko la kumkataa meya Arusha
  Kanisa heri linyamaze na kufunga mdomo maana kila nikikumbuka mauaji ya kimbari Rwanda huwa nasikitika sana Kanisa linapoongelea juu ya haki! kila nikikumbuka mauaji ya Mwembechai Dar, na kauli alieitoa Padri Lwambano kuwa Serikali iwashugulikie Waislamu wa Msikiti wa Mwembechai na siku ya pili Polisi waliitikia wito huo na kuuwa wananchi wenzetu! nasikitika tena Kanisa kuhubiri haki!

  Kila nikikumbuka mauaji ya raia huko visiwani na kauli ya Muadhama Kardinali
  Pengo kuwa waliouliwa na Polisi huko Zenji ndio wabebe lawama kwa kutokutii amri ya Serikali ya kutokuandamana!!

  Sasa, leo Kanisa na Baraza la Maaskofu watakuwa na ubavu gani wa kujitokeza na kulaani mauaji ya Arusha?

  Kuna watu wengine wapumbavu watakao fikiri kuwa mimi nafurahia mauaji ya Arusha lakini kwa hakika kila binaadamu mwenye hisia hatafurahia kitendo hicho cha Askari wetu kufyatua risasi za moto na kuua wananchi! ni tendo la kulaaniwa lakini sio Maaskofu wajitokeze leo ghafla na kutoa kilio cha kinafiki! kwanza waombe msamaha kwa maovu waliofanya huko nyuma kwa kuunga mkono maamuzi ya Serikali ya Benjamin Mkapa ya kuuwa raia wa nchi hii na ndipo wafungue ukurasa mpya wa kudai haki za wananchi kinyume chake itakuwa vigumu kuelewa lengo la Kanisa ni nini!

  Anko Sam said
  Re: maaskofu watoa tamko la kumkataa meya Arusha
  Originally Posted by zomba
  Hawa maaskofu ndio kiini cha chokochoko, fitna na uzabizabina. Kuna zaidi wanachokijuwa?

  Haya, wamkatae meya, sasa wamkatae ana chaguo la mungu. Si walioteshwa?
  "Zomba mimi nakushangaa sana, maana siku hizi UMEHARIBIKA KABISA, kwani huko nyuma haukuwa hivyo"
  George Jinasa said
  Re: Maaskofu wamkataa meya wa CCM Arusha
  kwa kulaani vurugu na mauwaji yaliyotokea Arusha mimi ninawapongeza mababa Askofu kwa dhati. Ili hili la kutomtambua Meya mimi nakuwa mgumu kukubaliana nao kwa sababu nyingi. Kwanza, ninauhakika kwamba Maaskofu hawakushiriki katika uchaguzi wa Meya. CCM wanadai Meya wao alishinda. Chadema wanadai Kura zilichakachuliwa. Msimamizi wa uchaguzi alimtangaza mgombea wa CCM kuwa mshindi. Sasa kama Chadema anasema ukweli au CCM anasema ukweli sijua Maaskofu wametumia kigezo gani kubaini. Naamini hawawezi kusema kwa mgombea wa Chaedema alipata kura ngapi na wa CCM alipata kura ngapi tofauti na alivyotangaza msimamizi. Maana, kumbukumbu za kura bado ziko mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi.Sababu ya pili ni kwamba usahihi na uhalali wa matekeo umezua mgogoro kati ya CCM na CHADEMA. Maaskofu ni wetu sote. Wanasikiliza maungamo kwa waumini wao walio CCM, CHADEMA, CUF na vyama vingine. Ingekuwa ni busara zaidi kwao kama wangetaka uhalali wa matokeo hayo uchunguzwe na vyombo venye mamlaka ya kufanya hivyo kuliko kuunga mkono upande mmoja kati ya pande zinazogombana.

  Makanisa na taasisi nyingine katika sehemu nyingine duniani zinachukua nafasi ya usuluhishi, Kristo anasema "Heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu". Kanisa linapoteza sifa hii ya upatanishi kwa kuchukua nafasi katika pande zinazogombana. Tunaelewa pia kwamba taasisi za kidini ni kama wazazi. Wanaweza mara nyingine kutoa sauti ya kukosoa. Lakini hilo linahitaji kufanyika kwa hekima na busara sana hasa pale pana pande mbili zenye ushawishi mkubwa zinapovutana.
  Ningewashauri mababa Askofu na viongozi wa dini zingine siku nyingine tujitahidi kuepuka kuchukua nafasi fulani katika pande zinazovutana. Safari bado ni ndefu kwa hali inavyoonesha na mchango wa taasisi za dini unategemewa sana katika kuiweka nchi yetu katika amani. Watanzania bado tunaheshimu sana dini zetu na viongozi wetu wa dini.


  kagumyamuheto said
  Re: Maaskofu wamkataa meya wa CCM Arusha
  Pengine ile dhana ya UDINI ndipo inapoonekana hapa. Mbuni kaficha kichwa kwa muda mrefu huku kiwiliwili chote kikiwa nje sasa kaamua kutokeza kichwa hadharani. Mbona hawakutoa tamko pale dereva wa ccm pale maswa alipouawa na chadema?? Au pale hakuna haki ya kuishi?? Na je, uchaguzi wa meya umefanyika januari??? Why now??
  Nasikia harufu ya kumwagika damu kama ile ya rwanda!! Unapoona maaskofu nao wanachanganya dini na siasa ujue ni hatari. Kwani nafasi ya umeya ni ya kuhubiri kanisani???. Au kuwa meya lazima uthibitishwe na kanisa??. Ni kweli taratibu zilikiukwa katika kumpata meya kwani mahakama hazipo?? Taratibu zipi zimefuatwa??
  Nasikia harufu ya damu!. Jk andaa jeshi liwe tayari tayari! Nasi pia tupo tayari.

  MSAUZI said
  Re: Maaskofu wamkataa meya wa CCM Arusha
  Hawa Maaskofu wenu ni wanafiki,si ndo hawa waliowahi kusema Kikwete kachaguliwa na Mungu?
  Anonymous said
  Re: Maaskofu watoa tamko la kumkataa meya Arusha
  Originally Posted by Kadogoo
  “Kanisa heri linyamaze na kufunga mdomo maana kila nikikumbuka mauaji ya kimbari Rwanda huwa nasikitika sana Kanisa linapoongelea juu ya haki! kila nikikumbuka mauaji ya Mwembechai Dar, na kauli alieitoa Padri Lwambano kuwa Serikali iwashugulikie Waislamu wa Msikiti wa Mwembechai na siku ya pili Polisi waliitikia wito huo na kuuwa wananchi wenzetu! nasikitika tena Kanisa kuhubiri haki!
  Kila nikikumbuka mauaji ya raia huko visiwani na kauli ya Muadhama Kardinali Pengo kuwa waliouliwa na Polisi huko Zenji ndio wabebe lawama kwa kutokutii amri ya Serikali ya kutokuandamana!!
  Sasa, leo Kanisa na Baraza la Maaskofu watakuwa na ubavu gani wa kujitokeza na kulaani mauaji ya Arusha?

  Kuna watu wengine wapumbavu watakao fikiri kuwa mimi nafurahia mauaji ya Arusha lakini kwa hakika kila binaadamu mwenye hisia hatafurahia kitendo hicho cha Askari wetu kufyatua risasi za moto na kuua wananchi! ni tendo la kulaaniwa lakini sio Maaskofu wajitokeze leo ghafla na kutoa kilio cha kinafiki! kwanza waombe msamaha kwa maovu waliofanya huko nyuma kwa kuunga mkono maamuzi ya Serikali ya Benjamin Mkapa ya kuuwa raia wa nchi hii na ndipo wafungue ukurasa mpya wa kudai haki za wananchi kinyume chake itakuwa vigumu kuelewa lengo la Kanisa ni nini!”

  Mkuu asante sana namie nakumbuka hilo tamko na siku mauaji ya mwembechai yalipotokea hakuna Tamko hata moja la maaskofu lilitokea kulaani leo hii wanaleta unafiki wao wa kulaani mauaji ya Arusha. Hakuna mtu anayeyafurahia haya ila tunakemea unafiki wa maaskofu kwa vile kuna muislamu pale juu leo wanajitia vimbembele kukosoa wajiangalie kwanza kabla ya kusema otherwise jamii hasa ya waislamu haijasahau makovu waliyoyaacha kipindi kile cha mwembechai.....

   
 16. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mary chatanda shut up,,,,,,,,,,,,,,,,,,wewe ni mamluki ulisababisha vifo vya wasiokuwa na hatia,,,ndiwe ulieharibu uchaguzi,na damu zote ziwe juu ya kichwa chako
   
 17. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Wataachaje kuzungumza wakati mmewauwa waumini wao! Mkiwamaliza wote watawaongoza akina nani kwenye hiyo imani. Kama hamna uchungu na binadamu, wao wanao na wanajua wapo kwa ajili ya wananchi wengi wakiwemo mliowauwa/kuwajeruhi.
   
 18. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Kweli ccm hamna vichwa vya maana, hivi membe, warioba, sitta, mwakyembe, selelii, pinda, anne malecela etc design yenu mbona hamuongei kuhusu yaliyotokea arusha? Halaf mnataka tuwajue nyiye ni wapambanaji! Kivipi? Kama mambo ya msingi ya watu kuuawa nanyi mko kimya.
   
 19. kagumyamuheto

  kagumyamuheto JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani haya mauaji ya arusha ni MALIPO ya ile DHAMBI ya CHADEMA kuuwa MTU pale MASWA kipindi cha KAMPENI. Twende mbele turudi nyuma ukweli ndio huo.

  MAASKOFU WANAENDELEA KUJIUMBUA - KANISA = CHADEMA = MAUAJI YA KIMBARI.
   
 20. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanapokuwa wamevaa magwanda ya kijani (siku hizi haya wekwi alama ya jembe na nyundo baada ya mafisadi kupora chama) wanakuwa nguvu, mamlaka na majasiri ajabu. Hata binadamu mwenzao akiuwawa kwa kosa walilosababisha wao, wenyewe ushangilia. KUMBUKA mambo ya SUMBAWANGA mjini wakati wa matokeo ya uchaguzi mkuu 2010 walifikia kubeba jeneza na msalaba kuingia nalo kanisani kuendesha misa ya kuzika viongozi wa dini na mgombea wa CDM na wakaenda kuzika kuku ASKARI wa MWEMA wakishuhudia ubabe huo na udhalilishaji wa wavaa nguo za KIJANI hao( huku wakijuwa wazi kuwa wamechakachua).

  PINDI wazivuapo na kurudi ktk maisha ya kawaida utawaonea huruma jinsi wengi wao walivyopigika kimaisha, WALE WASUMBAWANGA WALIPORUDI URAIANI BAADA YA KUVUA NGUO ZAO ZA KIJANI, wakakuta KANISA KATOLIKI limetangaza kuwa TENGA KUPATA HUDUMA ZOTE ZA KIROHO KIFUPI WAMETENGWA KUWA WAUMINI WA KANISA uwezi kuamini wanavyo lalama na kuomba HURUMA maana MAvazi ya kijani wameyavua sasa wana uface UKWELI wa maisha halisi. Kma kawaida wakamtuma PINDA kuwaombea MSAMAHA lakini KANISA limewaambia suala walilofanya kulidhalilisha kanisa si la kisiasa hivyo hata haje JK na Baraza lake la Mawaziri msimamo wa kanisa ni uleule. Taratibu za kusamehewa na kurudishwa kundini zipo hivyo wasitegemee Viongozi wao wakija na Mavazi ya KIJANI ndio suluhu itapatikana, KWA MUNGU hakuna kuombeana toba ya DHAMBI kila mtu na mzigo wao WAMEAMBIWA WAZI kama wanatubu waomboleze wao wenyewe na kutubu na si kumtegemea PINDA KUWAOMBEA msamaha.

  SASA HUYO MARY CHITANDA ujasiri anaupata kwa kuwa anaMAVAZI ya kijani ngoja ayavue ndipo atauface ukweli, MAMA HAWA NGULUME hadi kaja kuokolewa na GAZETI LA MWANANCHI baada ya kuugua muda mrefu na CCM wenzake kutojali akawa anasaidiwa na ndugu, jamaa, na marafiki. MWANANCHI ikaweka hadharani kuwa huyu mama tusipoangalia RIP hivyo CCM wasitupe jongoo na mti wake ndio salama ya MAMA ngulume. SASA CHITANDA aangalie ataenda kutafute huduma kwa hao anaowaambia wavue majoho watamuelekeza kwenda kwa ROSTAM au MAKAMBA, na akivua hayo mavazi ya kijani uraiani atatukuta ndipo atakapo jua UMUHIMU WETU . MAANA MAVAZI YA KIJANI YANA POFUSHA NA YANAWEHUSHA.
   
Loading...