Ma sheikh arusha wamtambua meya wa arusha

masheiks wengi hawana shule! sio watu wa kutilia maanani sana. hivi kwanini wakisema wanasema kwa niaba ya waislamu wote. je huwa wanafanya mkutano na waislamu wote kupata maoni yao. ina maana mawazo na msimamo wa masheik ndo ya waislamu wote?
 
kwa mtazamo wangu hawa mashekhe ni kama wale wazee wa dar es salaam.. wanaona tatizo kwa macho yao ya nyama lakini bado wanapiga vigelegele so they have benefits behind this matter

I agree wanaweza kuwa na benefits kwa kuunga mkono Meya wa arusha ambaye tunakubali uchaguzi uliompa hiyo nafasi ulikiuka taratibu....Benefits si za kichama kwa maoni yangu,zaweza kuwa zile za uanzishwaji wa mahakama ya kadhi ambayo ni kwa ajili ya waislamu wote bila kujali itikadi zao au benefits nyingine tusizozijua....wanaojua waseme,labda twaweza pata majibu kwa nini waliunga mkono Meya????
 
Tatizo wanaokataa kuwa bakwata iliundwa kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya ccm na serikali yake tuu na ndio maan taasisi nyingine za kiislamu zinapigwa vita na ndio maana ukijaribu kuangalia matamko karibu yote yanayotolewa na bakwata huwa yapo upande wa aidha serikali au ccm. Kwa muislamu wa kweli analijua hili na ndio maana mpaka sasa huwa waislamu tunaswali eid siku tofauti tofauti ingawa sherehe ilitakikana kuwa ni moja. Bakwata wana masilahi yao kwenye ccm na serikali
 
Bakwata wasitegemee kupata mahakama ya kadhi kwa kuunga mkono udhalimu wa wazi. Michele hiyo ni ndoto ya mchana kweupe kabisa
 
Naona mengi yameandikwa hapo na Wachangiaji mbalimbali!
Nevertheless,haijalishi mtu ni wa Imani gani lakini inapotokea Viongozi wa dini kubwa kama Uislamu halafu wana Muunga Mkono Meya wanayejua fika kwamba amechaguliwa kwa mizengwe is disappointing!
Unfortunately siamini kama huu ni msimamo wa Waislamu wa Arusha,nadhani huu ni msimamo wao viongozi wenyewe coz naamni katika maandamano yale na Waislamu walikuwepo na walipata madhara kama watu wengine!!

Ni udhalimu wa hao Viongozi wa Kiislamu kuunga mkono Meya aliyechaguliwa na Ubabe,sielewi wanasukumwa na nini but it is Immoral of them!
Shame on them!!!
 
masheiks wengi hawana shule! sio watu wa kutilia maanani sana. hivi kwanini wakisema wanasema kwa niaba ya waislamu wote. je huwa wanafanya mkutano na waislamu wote kupata maoni yao. ina maana mawazo na msimamo wa masheik ndo ya waislamu wote?

Una uhakika na unachokisema? Unajua title ya sheikh ni kama Dr wenu wa divinity bwana Slaa acha kudharau wewe!!
 
I agree wanaweza kuwa na benefits kwa kuunga mkono Meya wa arusha ambaye tunakubali uchaguzi uliompa hiyo nafasi ulikiuka taratibu....Benefits si za kichama kwa maoni yangu,zaweza kuwa zile za uanzishwaji wa mahakama ya kadhi ambayo ni kwa ajili ya waislamu wote bila kujali itikadi zao au benefits nyingine tusizozijua....wanaojua waseme,labda twaweza pata majibu kwa nini waliunga mkono Meya????

Nakubaliana na wewe kuwa yawezekana kama kweli hizo benefits zipo kama walivyokuwa maaskofu wakisisitiza watu wengine wafuate sheria wakati wa Mkapa but nadhani huyu mletaji wa hii mada si mkweli ingelikuwa vizuri angelileta evidence kwanza na sio kutoa mawazo yake finyu yaliyojaa chuki za kidini.
 
Haijalishi tamko litolewe na masheikh au serikali, wampe ushirikano wasimpe hoja ya msingi ni kuwa uchaguzi ni batili (uliomweka meya madarakani) kwa kuwa sheria haijakidhiwa tena makusudi huku CCM wakichekelea, Chadema tutadai haki hiyo kutumia sauti ya watu sio kusubiri masheikh waseme (afterall uelewa wao si mkubwa katika mambo ya sheria na elimu zao ni finyu) Nawasilisha!!1
 
Haijalishi tamko litolewe na masheikh au serikali, wampe ushirikano wasimpe hoja ya msingi ni kuwa uchaguzi ni batili (uliomweka meya madarakani) kwa kuwa sheria haijakidhiwa tena makusudi huku CCM wakichekelea, Chadema tutadai haki hiyo kutumia sauti ya watu sio kusubiri masheikh waseme (afterall uelewa wao si mkubwa katika mambo ya sheria na elimu zao ni finyu) Nawasilisha!!1

Pathetic wewe uelewa wako mkubwa??? Endeleeni kudai haki yenu
 
Mkiambiwa udini upo mnang'aka, haya sasa kazi kwenu!

Kwa hili nampa tano Chitanda, wavue tu majoho yao waingie CHADEMA! Hamna mswalie mtume hapa, ebooo!!!!
 
Mary Chitanda alikosea lakini na wewe hujatumia busara maana ya maaskofu yalikua ya Mary. lakini wewe kuwatukana masheikh ni ujinga wako unauonyesha na chuki za kidini.
Yawezekana mary aliona kosa na akikiri hata rudia lakini safari hii unamshawishi aendelee kufanya ujinga

Hujatumia busara kusuluhisha tatizo vinginevyo useme hayo ni maneno umeamua kuwatukana masheikh
Sijaona tusi langu kwa Mshekh Mkuu,Mbona unamtete huyo Mama hivyo,kwenye kikao chake na waandishi unajua aliyosema ilhali yeye ndo chanzo cha yote, je na Mashekh walikuwa wanasubiri nn kutoa tamko hadi waliposikia la Maaskofu,maana tamko lao limekaa opposite na lile la Maaskofu,haihitaj kuwa hata na Certificate kung'amua hilo.
Ki msingi sijatukana mtu wala kada ya watu,kama umenitafsiri vibaya pole na samahann
 
Mleta mada ni mchukia uislam habari yake haina source na uislamu umekataa kuuwa/kudhulum nafsi hao mashekh watakaohalalisha mauaji yale ya Arusha watakuwa si mashekh ni mashehena.

{{Wala msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza (kuiua) isipokuwa kwa haki (Akahuhumu hakimu kuwa mtu huyo anastahiki kuuawa na akatoa amri ya kuuawa). Na mwenye kuuawa kwa kudhulumiwa, basi Tumempa nguvu mrithi wake (juu ya muuaji huyo, akitaka ataomba kwa hakimu kuwa amuuwe kama alivyomuuwa mtu wake na akitaka atamsamehe, na akitaka atamtoza kitu). Basi (huyo mrithi asifanye fujo katika kuua kwa ajili ya huyo mtu wake aliyeuliwa). Hakika yeye atasaidiwa (na Sharia maadamu anayo haki).}} [17:33]
Tukiegemea kwenye aya hii, hairuhusiki kwa Uislamu kuua mtu yeyote asiye na kosa kwa baadhi ya makosa ya jinai. Ni vyema tukakumbuka katika nukta hii, tofauti iliyofanywa hapo juu baina ya Qur-aan na Sunnah, na Waislamu; ni Qur-aan na Sunnah pekee ndizo zilizoafikiwa kuwa zinaendana pamoja na matakwa ya Muumba, wakati Waislamu wanaweza sana kutetereka. Hivyo, kama Muislamu yeyote ataua mtu asiye na hatia, Muislamu huyo ametenda dhambi mbaya kabisa, na hakika tendo hilo haliwezi kudaiwa kuwa limefanywa “kwa jina la Uislamu”.

Sichukii Uislam, Ukristo n.k inshort sichukii imani ya mtu yeyote ila nachukizwa na kukerwa na matendo ya wana imani,wawe wakristo eg Jaji Werema, Mary Chitanda, Kamanda Ande n.k waislam eg Makamba nk.
Nadhani post yangu sijaitunga na ndivyo walivyofanya Viongozi wa KIISLAM wa Arusha,sasa mie kuchukia kwangu UISLAM kunakujaje, unless uniambie kuwa haya niliyoyasema siyo ya kweli
 
Siwezi kukataa ila ukweli utabaki paleplae hao masheikh ni wale wa jumuia ya Kiislam ya CCM inaitwa BAKWATA. Wao wapo kwa ajili ya maslahi ya chama zaidi.

Du Kumbe CCM inatumia WAISLAM kutuvuruga Wa Tanzania, Hii ni hatar kwa ustawi wa Jamii yetu,tuwapuuze WAISLAM WA CCM = BAKWATA
 
Kama ni kweli viongozi wa kiislam watakuwa hawafanyi vema??? Naona kama wanasababisha tu mambo kuzidi kuwa shaghalabaghala. Wangeanza wao kutoa kauli ya kumtambua huyo meya ningesema labda wana sababu za msingi!!!! Lakini kwa hapa naona wanachemsha tu.... Kwanini wasubiri kilichosemwa na maaskofu ndo waende kinyume nacho.... huu ni udini...Mimi ningeshauri kama wenzao wametoa kauli waangalie ni kwa nini ikiwezekana wajadiliane nao kwanza kupata sababu na malengo kabla hawajaenda against.. otherwise wanyamaze tu itawapa heshima zaidi kuliko hii ya kupinga tu ili mradi na wao wasikike!!!

Ni hayo tu.:A S 27::A S 27::A S 27:
...kwani toka lini wakawa na busara ama kutaka amani!!
 
MUONGO MKUBWA,fanya utafiti acha kueleza uongo mradi utetee hoja yako.Masheikh wa BAKWATA si wote wako CCM na BAKWATA si organization ya kisiasa,kwahiyo tuseme maaskofu wako CHADEMA kwakuwa wali-condemn mauaji ya Arusha,wao walikuwa wanatimiza wajibu wao na BAKWATA imetimiza wajibu wake......Kwakuwa wametofautiana kauli kwenye hili la meya ndo unaanza kuwasema kwa kejeli???Lini na wapi imeandikwa kwamba BAKWATA na MAASKOFU wakubaliane kwenye kauli zao.......i call this cheap arguments,thats demorcracy and there is freedom which allow us to differ in our opinions for God's sake.Eti wako kumaslahi ya chama zaidi?????kama wewe ulivyo kwa maslahi ya chama zaidi na ndo maana unasema uongo kutetea hoja ya chama fulani iliyoungwa mkono na maaskofu.
Hapa hakuna kumung'unya maneno wala kusema kwa Mafumbo,kwenda kwao kinyume na tamko la Maaskofu,sio kweli kwamba wame exercise Democracy au freedom of speech,uhuru wa kuongea upo,ila sio kuongea VITU VYA AJABU kama walivyofanya Mashekh ARUSHA,chanzo cha vurugu ni uchaguzi wa Mayor,na Mayor hakupatikana kwa Uchaguzi wa huru na haki (Kama Muungwana),wao kusema wanamtambua ni haki yao lakini kwa undani ZAID ni kama wamebariki Mauaji ya ARUSHA ambayo kimsingi chanzo chake ni huyo Mayor wanayempigia Chapuo,suala la maaskofu Kuunga mkono hoja ambayo CDM ni haki yao pia,tujiulize je Madai ya CDM katika uchaguzi wa Mayor Arusha hayana Msingi
 
kwa upande wangu naona hoja ya msingi ya kujiuliza kama MAASKOFU wamelaani na kutomtambua meya huyo na MASHEHE wanamkubali basically wameona kila kitu kimeenda shwari???!!!????!???! HILO NDO TATIZO KUBWA SANA HAPA!!!! kwa jinsi nionavyo..kweli kabisa is it legit kukubaliana na uchaguzi huo na madhara yaliojitokeza?? jamani BADILIKENI wenzangu.... KHAA
 
Una uhakika na unachokisema? Unajua title ya sheikh ni kama Dr wenu wa divinity bwana Slaa acha kudharau wewe!!

Sasa hapo Dr Slaa anaingiaje jaman,Hiyo ni indication kuwa Dr Slaa ni tishio kwako na watu wa kada yako kwa ujumla.
Mwalimu wangu wa Chekechea aliniambia kuwa "Waache wajifananishe na wewe wala usisumbuke kujifananisha nao"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom