Ma-bodyguard wa club muwe mnapiga kwa ustaarabu au kumtoa mtu tu nje

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wakuu habari za uzima?

Ndugu zangu wana JF kwa wale watu ambao wanaendaga club kupooza stress za wiki nzima nadhani watakuwa wameshakutana na hizi vurugu za watu wakibondwa na walinzi wa club kwa kusababisha vurugu.

Ndugu zangu mimi si mtu wa viwanja ila nina mashine zangu za kutengeneza popcorn(bisi) kwenye club mbili.

Kwa kweli wikiendi hiyo iliyoisha nilienda kuangalia maana nimemuweka kijana. Nilipofika mida ya saa nne usiku nilikuwa nyuma kabisa nikiangalia kijana akiwa anaendelea kupiga kazi yake.

Ikabidi nimuite muhudumu nimwambie aniitie jamaa anayetengeneza chipsi akaenda kumuita, jamaa kuja nikamuagiza chipsi huku nikiendelea kununua muda pale. Nikamuomba yule muhudumu aniitie kijana yule wa popcorn kule nyuma. Kwa kweli kijana hakujua kama nipo mule ndani akaja.

Kufika pale nikaongea nae nikamwambia vipi biashara akasema safi, basi ikabidi aulize kwa kushangaa. Nimeshangaa sana kukuona hapa kaka mkubwa leo, nikamwambia nimekuja tu kukuona.

Basi akawa anaitwa nikamuacha akaenda, kama dakika 15 baadae nikaona watu watatu wamemnyanyua jamaa juu akivuja damu, walipopita nae karibu na nje kutokea walimshusha na kuanza kumshushia kipondo. Aiseeeeh!!!

Yule jamaa alipigwa sana huku walinzi wakisema “wewe ukilewa unajifanya msenge huna akili kupanda juu ya meza na kuanza kugombana na watu”

Kwa kweli ilibidi nimuite aliyenihudumia chakula changu kulipa bili na kuondoka.

Nyinyi wamiliki wa ma club na ma bar makubwa embu muwafundishe hawa walinzi wasipige watu kwa namna ile.

Mlinzi kazi yake ni kutuliza ghasia na kama mtu anakuwa kirusi kwa kuondoa amani ya watu ndani humo inabidi atolewe nje na mara moja apelekwe polisi.

Kwa kile kipigo ni hatari sana, wamiliki wa ma club muwe makini na kujua hawa walinzi wanafanya nini wasije wakawaingiza kwenye matatizo.
 
Hii nimecheka na kukumbuka mbali sana .
Nimekumbuka wiki iliyopita vile rafiki yangu Daudi mwasongwe alivyoniokoa kwa hawa jamaa la sivyo wangeniua japo miguu yangu haikunisaliti pia .

Kiukweli ukijua unakunywa pombe na pia ukilewa unataka mademu wa hapo bar wote wawe wako basi uwe na washikaji wenye nguvu kampani yako bila hivyo hawa walinzi wanakuuwa kimasiala kabisa

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Mkuu,
Pole sana uliwakimbia?
 
Nyinyi wamiliki wa ma club na ma bar makubwa embu muwafundishe hawa walinzi wasipige watu kwa namna ile.
Mlinzi kazi yake ni kutuliza ghasia na kama mtu anakuwa kirusi kwa kuondoa amani ya watu ndani humo inabidi atolewe nje na mara moja apelekwe polisi.

Kwa kile kipigo ni hatari sana, wamiliki wa ma club muwe makini na kujua hawa walinzi wanafanya nini wasije wakawaingiza kwenye matatizo.
Polisi hawaruhusiwi kupiga mhalifu, sembuse hao ma bouncer? Wakikupiga, hata kama una kosa, wewe nenda polisi kuripoti na kufungua kesi ya madai. Waambie polisi ukishinda watapata 5%, na mwanasheria 15%. Tena tafuta doctor muahidi 5% aseme wamekupiga sehemu za siri na kuharibu vyombo, dai kama bilioni moja hivi. Mtaji wa masikini mara nyingine ni akii zake mwenyewe. Tena kama unarekodi video ndio unawapata kirahisi kabisa.
 
Mkuu unafikiri hili linawezekana?

Mimi nimesema kama mabaunsa wanaweza wawatoe nje na watoe taarifa polisi na si kupiga mtu.

Hawa mabaunsa wanPiga sana
 
Mkuu unafikiri hili linawezekana?

Mimi nimesema kama mabaunsa wanaweza wawatoe nje na watoe taarifa polisi na si kupiga mtu.

Hawa mabaunsa wanPiga sana
Hakuna mtu anaruhusiwa kupiga mtu mwingine kwa kosa lolote lile, hata walimu siku hizi wanakatazwa kupiga wanafunzi!
 
Nilishawahi kushuhudia hii kitu Geita mwaka juzi, baada ya kumdup jamaa nje nilimuita incharge kimbinu wa wale mabaunsa nikamuelekeza kiustaarabu akawa kama kaelewa flani hivi.
 
Ni kwanini wanapiga vile mkuu?
Kwa maelezo yake alisema watu wa huko ni wakorofi sana ukiwachekea wanaweza kufunga bar. Ila baada ya kumwambia hilo halitoshi kumfanyia vile alielewa na kuahidi kuwapa maelekezo wa chini yake. Kwa bahati mbaya sikuwahi kupata nafasi ya kurudi kule.
 
Polisi hawaruhusiwi kupiga mhalifu, sembuse hao ma bouncer? Wakikupiga, hata kama una kosa, wewe nenda polisi kuripoti na kufungua kesi ya madai. Waambie polisi ukishinda watapata 5%, na mwanasheria 15%. Tena tafuta doctor muahidi 5% aseme wamekupiga sehemu za siri na kuharibu vyombo, dai kama bilioni moja hivi. Mtaji wa masikini mara nyingine ni akii zake mwenyewe. Tena kama unarekodi video ndio unawapata kirahisi kabisa.
Rushwa, uongo udongo, wizi! Tz itatoka?!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom