Kumbe bado upo upo kwanza kama mwana FA dada
Sky Eclat , nimeipenda hiyo ukisikia pooh jua limempata, ila upande wa pili wa shilingi pia nikupe pole nawe maana naamini pia nawe lilikupata ndio maana umelianzishia uzi maalumu na huenda mara nyingi tu.
Kuna watu hawahitaji hizo kitu kitu kabisa, yaani usafi wa kawaida tu kwao inatosha, yaani kuoga kwa sabuni ya kawaida na kujipaka mafuta tena ya mgando let say vestline nk. Lakini wengine walivyoumbwa wakifanya hivyo ni kituko, harufu ya jasho nk haviwaachi salama. Kumbe kuna uwezekano ulipata bahati mbaya ya kukutana na hili kundi la pili ambalo wao kuwa safe lazima watumie hizo additives/perfumes, deodorant nk unazosema ili kubalance mambo.
Lakini ulipaswakumweleza huyo mtu wako kuliko kusepa mazima, unajua kwa nini yeye sio rahisi sana kwake kufahamu kuwa anakuwa na hali ambayo ni chukizo kwa mwingine, anaweza kuwa anajiona/anaji feel kuwa yupo normal kumbe ni tofauti. Wengi wanaojifahamu huwa wanafikia hatua hiyo aidha kwa kuambiwa ama baada ya hali hiyo kuwa imekuwa critical.
Mimi ni mpitaji tu, ahsante