Ma Bachela wenzangu, Usawa huu wa Magu Kuna kuoa kweli?

hiden

JF-Expert Member
Sep 28, 2015
376
691
Wanaume, wale ma bachela,
Mpaka sasa siusomi usawa kwa kweli, hali mbaya, vyuma vimekaza.
Nimemaliza chuo, ajira hamna mwaka sasa,
Nimeanzisha vibiashara zaidi ya vitatu vyote vimekufa.

Sasa kuna kibiashara cha chakula nakiendesha hapa, lkn mambo hayaeleweki, leo unauza sana kesho hola.

Wateja wangu wengi ni watumishi wa halmashauri, hali zao hovyo, mikopo mingi kiasi kwamba hupiga milo miwili.kwa siku, akipiga mitatu jua kuna dokezo limekubali siku hiyo

Sasa nilipanga nikifika 27yrs nioe, lkn naona ngoma inaisha na usawa siusomi. Maza na Mzee wanauliza, kijana mbona hatukuelewi?
Unaoa lini? Au unaendekeza Uhuni?

Nikiwaambia hali haisomeki hawaelewi.

Mwanamke anahitaji matunzo aisee, sio yeye tu hata mtoto atakae zaliwa. Naogopa nikishindwa majukumu nitasaidiwa.

Sasa sielewei Mabachela wenzangu, vipi hali zenu huko?
Kuna kuoa kweli Awamu hii ya Bwana Mkubwaa?

Embu njooni tushauriane....!!
 
Mimi ngoja nitangaze nia hapa kabisa, mdada ambaye ni hasler ukuje huku tuanze life serious..!
 
Back
Top Bottom