M23 rebels have 48 hours to surrender: UN

M23 rebels have 48 hours to surrender: UN

Koba kama upo maeneo ya Goma rudi kwenu Rwanda. Kama bodaboda zipo chukua urudi kwenu. Mwambie Dereva nauli atalipa Kagame. JWTZ piga hao Watutsi warudi kwao.
 
Dear jf members?tusifurahie vita ya drc na tanzania na m23!
 
Koba,

..utawala wa Kinshasa unawatambua M23 kama raia wa DRC.

..M23 walikuwa sehemu ya jeshi la DRC ila waka-defect baada ya baadhi yao kuambiwa watakuwa deployed maeneo tofauti na eastern Congo.

..kwa msingi huo utaona kwamba ni M23 ndiyo wanaojitenga na ndugu zao wa maeneo mengine ya DRC.

..lakini hawa M23 siyo kikundi cha kwanza kuleta vurugu zisizokuwa na msingi DRC. sijui kama unawakumbuka wakina Bizima Karaha[alikuwa anaungwa mkono na Kagame] na wenzake ambao walidai wanapigania Congo na wanaungwa mkono wa wananchi waliowengi. Baada ya kufanyika uchaguzi, matokeo yameonyesha kwamba wananchi wa Congo wamewakataa.

nafikiri iwe international policy ukipata mtu ni mgeni mkaazi basi ni vizuri ukamuweka mbali na mpaka wa kule anakotoka, kama hawa jamaa ni vizuri wakapewa mashamba magharibi mwa nchi au kusini mwa nchi ya congo
 

Wanajeshi wa Brigedi Maalum wakiwa katika mazoezi makali yaliyofanyika hivi karibuni huko Goma Mashariki ya Demokrasia ya Kongo..
Mmoja wa walinda amani kupitia Brigedi Maalum inayoundwa na wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi akiwa katika moja ya mazoezi yaliyofanyika hivi karibu huko Goma.


Kamanda Mkuu wa Misheni ya Kulinda Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ( MONUSCO ) Luteni Jenerali Carlos Albeto dos Santos Cruz ametakanza jana jumanne akiwa Goma kwamba MONUSCO itaanza rasmi kuitumia Brigedi Maalum na ametoa saa 48 kuanzia saa kumi jioni kwa saa za Goma jana siku ya Jumanne waasi wote kusalimisha silaha zao, na kwamba ifikapo saa kumi jioni kwa saa za Goma siku ya Alhamisi Agosti Mosi wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio la usalama kwa wananchi na MONUSCO italazimika kuwapokonya ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kwa mujibu wa Mamlaka iliyopewa na Sheria zinazowaruhusu kufanya hivyo.
----------------

Misheni ya Kutuliza Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO) imetangaza kwamba kwa mara ya kwanza itaanza kuitumia Brigedi Maalum ( Force Intervention Brigade) katika kudhibiti eneo maalum la usalama ( security zone ) kuzunguka mji wa Goma ulioko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na imewapa saa 48 waasi kusalimisha silaha zao.


Taarifa iliyotolewa na MONUSCO na kusambazwa na Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa jana jumanne, inaeleza kwamba watu binafsi katika eneo la Kivu ya Magharibi ambalo linajumisha Goma na Sake na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama watapewa saa 48 kuanzia saa kumi jana kwa saa za Goma ( Jumanne ) kuzisalimisha silaha zao katika Misheni hiyo na kujiunga na mchakato wa DDR/RR unaoratibu upokonyaji, usambaratishaji, urejeshwaji makwao, kuwaunganisha na jamii na kuwapatia makazi.


Baada ya saa kumi jioni ya Alhamisi, Agosti Mosi. Taarifa hiyo inasema. Wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio kwa usalama wa wananchi na MONUSCO itachukua hatua zote muhimu kuwapokonya silaha hizo ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kama ilivyoainishwa katika Mamlaka na sheria za ushiriki za MONOSCO.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo zaidi ya wananchi milioni moja wanaishi katika eneo dogo la Goma na Sake na kando kando ya barabara ambayo inawaunganisha na kambi ya wakimbizi ya Mugungu ambayo ni makazi ya muda ya watu karibu 70, 000 ambao wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano.


Kwa mujibu wa MONUSCO, tangu kati kati ya mwezi Mei eneo hilo limeshuhudia mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa kundi la M23 dhidi ya majeshi ya Serikali ya FARDC ikiwa ni jaribio la wazi la kutaka kusonga mbele kuelekea Goma na Sake.


“ Katika mashambulizi hayo, likiwamo la hivi karibuni la Julai 14, M23 walitumia kiholela silaha zao za moto zikiwamo silaha nzito ambazo zimesababisha wananchi kujeruhiwa” .

Taarifa hiyo imeongeza kwamba kundi hilo la M23 katika mashambulizi hayo limelenga pia Vituo vya Umoja wa Mataifa.

Aidha taarifa hiyo inabainisha kwamba eneo hilo maalum la usalama ( security zone) litasaidia kudhibiti tishio la moja kwa moja mbali na eneo la nje ya Goma na pengine eneo hilo linaweza kupanuliwa na kurudiwa sehemu nyingine kutakako hitajika.

Tamko hilo la kutoa saa 48 kwa waasi kusalimisha silaha zao linafuatia kuwasili katika eneo la Goma kwa Kamanda Mkuu wa MONUSCO, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz, ambaye alitangaza kwamba Misheni ya MONUSCO itaunga mkono jeshi la Serikali ( FARDC) katika kuanzisha eneo la usalama kuzunguma eneo la Goma na vitongoji vyake.

Taarifa hiyo inamkariri Kamanda Mkuu wa MONUSCO akiyapongeza majeshi ya serikali kwa kazi nzuri iliyofanya wiki iliyopita ya kuwadhibiti M23. Ingawa anasema eneo la Goma na Sake bado limo katika mazingira magumu sana na kwamba ni wajibu wa wahusika wote kuhakikisha wahalifu wote hawaendelei kuhatarisha raia wa eneo hilo.

Kwa mwaka uliopitia , kundi la M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha yamekuwa yakipambana mara kwa mara na majeshi ya serikali katika Mashariki ya Kongo, huku makundi hayo yenye silaha mwezi Novemba mwaka jana yakiikalia Goma kwa muda.

Aidha mapingano ya hivi karibuni ambayo safari hii yalihusisha pia kundi jingine la wanagambo wenye silaha lenye asili yake nchini Uganda, yamesababisha zaidi ya wananchi 100,000 kuyakimbia makazi yao na hivyo kuongeza mgogoro wa kibinadamu katika eneo hilo linalohusisha watu wengine 2.6 milioni ambao wameyakimbia makazi yao huku wengine 6.4 milioni wakihitaji chakula na huduma za dharura.

Wakati huo huo, Kaimu Mkuu wa MONUSCO Bw. Moustapha Soumare katika taarifa yake ametoa wito kwa pande zote kutafuta suluhu ya kisiasa kwa matatizo ya DRC kupitia Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani, usalama na ushirikiano wa maendeleo katika DRC na eneo la Maziwa Makuu uliopitisha mwezi wa Februari na viongozi 11 wa Afrika na Taasisi nne za Kikanda na Kimataifa.

Aidha akasema katika kipindi hiki ambacho suluhu la kisiasa linatafutwa MONUSCO itatumia nguvu iliyonayo kuwalinda wananchi dhidi ya hatari zitokanazo na makundi ya waasi.


WAASI WA M23 WAPEWA MASAA 48 YA KUSALIMISHA SILAHA ZAO.....VINGINEVYO NI BALAA TUPU - MPEKUZI HURU
 
MONUSCO sio wajinga kujiingiza kwenye guerilla warfare na hawa rebels and they will never attack or force to disarm anybody,the only thing they will do ni kuweka buffer zone na kusimamia kama kutakuwa kuna makubaliano yeyote btn hizi factions,Congolese hakuna mtu atapigana vita yenu ni nyie wenyewe ndio mtaleta peace, MONUSCO wako pale kusimamia amani and disarm kama kutakuwa na makubaliano yeyote.
Koba look, hiyo ingeweza kutekelezwa siku za nyuma, lakini sasa hivi kuna kila dalili za kuonyesha kwamba kibao kimewagehukia wakina PK,M7, M23 na factions nyingine nchini DRC. Kitu kingine M23 sio hit and run ragtag army, wako well organised na sio siri tena kwamba wanakuwa funded/trained na watu ambao hawataki pawepo AMANI ya kudumu nchini Congo, defectors ndio wame-spill the beans(ebishimbo) ingawa hiyo ilikuwa inajulika siku nyingi tu kwamba M23 are not a lone RANGER. In short International Community imekuwa fedup na an open ended mazungumzo ambayo tukiwa wakweli yalikuwa hayana tija yoyote zaidi ya wahusika kufaidika kulala kwenye a five star hotels huko Kampala na kupata posho!! Oh yes, mbinu za key players kutaka ku-buy time ili waendeleze uporaji wao wa rasilimali za DRC. Nakubaliana nawe kwamba wa Kongomani ndio wanapashwa kuleta amani ya kudumu nchini mwao - lakini kumbuka amani haiwezi kupatikana wakiwa wanaingiliwa na mataifa ya nje mara kwa mara kwa kisingizio chochote kile.
 
Koba look, hiyo ingeweza kutekelezwa siku za nyuma, lakini sasa hivi kuna kila dalili za kuonyesha kwamba kibao kimewagehukia wakina PK,M7, M23 na factions nyingine nchini DRC. Kitu kingine M23 sio hit and run ragtag army, wako well organised na sio siri tena kwamba wanakuwa funded/trained na watu ambao hawataki pawepo AMANI ya kudumu nchini Congo, defectors ndio wame-spill the beans(ebishimbo) ingawa hiyo ilikuwa inajulika siku nyingi tu kwamba M23 are not a lone RANGER. In short International Community imekuwa fedup na an open ended mazungumzo ambayo tukiwa wakweli yalikuwa hayana tija yoyote zaidi ya wahusika kufaidika kulala kwenye a five star hotels huko Kampala na kupata posho!! Oh yes, mbinu za key players kutaka ku-buy time ili waendeleze uporaji wao wa rasilimali za DRC. Nakubaliana nawe kwamba wa Kongomani ndio wanapashwa kuleta amani ya kudumu nchini mwao - lakini kumbuka amani haiwezi kupatikana wakiwa wanaingiliwa na mataifa ya nje mara kwa mara kwa kisingizio chochote kile.
Koba anatakiwa aelelawe wakongomani ni kikundi cha mai mai, hawa wengine akina bosco ntaganda, laurent nkunda, sultan makenga ni biashara ya nchi jirani, vikundi vya wakongomani kwa sasa vimetulia. baada ya baba lao kupelekwa ze hegi (The Hague)
 
Koba anatakiwa aelelawe wakongomani ni kikundi cha mai mai, hawa wengine akina bosco ntaganda, laurent nkunda, sultan makenga ni biashara ya nchi jirani, vikundi vya wakongomani kwa sasa vimetulia. baada ya baba lao kupelekwa ze hegi (The Hague)
Ni kweli mkuu kundi la MAI MAI ambao ni Wakongomani asili walikuwepo toka ENZI za Mobutu, factions nyingine ni za kuchonga tu na viongozi wenye agenda zao za siri kuhusu DRC, alafu walivyo waongo na wanafiki wanafikili DUNIA haijui historia ya kweli kuhusu Taifa la DRC.
 
Back
Top Bottom