M-Pesa sio salama

Sasa wewe unataka wakusaidie vipi endapo utatuma pesa kimakosa, na unawasiliana na kampuni, wao wanakuambia ulipotuma pesa tayari imeshatolewa
Hapana huo ni usumbufu.
hela zangu bado nisumbuke.
 
Kunatakiwa angalau kuwepo na mfumo wa kuzuia kutoa pesa mara tu uipokeapo kwa angalau dakika 10, ili kuwezesha mtumaji kama amekosea aweze kuwasiliana huduma kwa wateja na pesa irudishwe

Hii itakua nzuri zaidi kwa kweli, au wapige simu ku confirm kwa mtumaji ela kama aliyetumiwa atataka kuitoa kabla ya hiyo time limit. Pole sana mkuu uliye tuma kimakosa.
 
Kunatakiwa angalau kuwepo na mfumo wa kuzuia kutoa pesa mara tu uipokeapo kwa angalau dakika 10, ili kuwezesha mtumaji kama amekosea aweze kuwasiliana huduma kwa wateja na pesa irudishwe
Umeshawahi kuuguwa kichaa? Unafahamu maana ya mtu anapokuwa na dharura na anatuma pesa sehemu? Usubiri dakika 10 ili iweje wakati kabla ya kutuma unaoneshwa mpaka jina la unayemtumia?
 
Kwanza pole kwa usumbufu

Pili wewe umekosa umakini

Tatu jiulize wewe ukiwa Wakala mteja ametoa hela halafu ukamatwe wakati unatoa Huduma kwa Wateja kiusahihi

Hapa nazungumzia watakapo fika polisi kukamata ofini kwako hawatasema kuna mteja mwizi ila watasema unashirikiana na wezi wa kimtandao

NNE unatakiwa kujua kuwa kwa muda wa dakika kumi ni nyingi sana hasa unapo mtumia mtu ambae si mwaminifu

Na ukiweka namba ya siri kuna jina la unae mtumia na onyo lipo iweje uwalaumu wao kwa uzembe wako


Tanzania ukipata watu watakao kuwa tayari kupambana bila kumpataia mwingine lawama inaweza kusogea mbele zaidi ila tunapo endelea kulaumu ndio tunakwama
 
Kuna muda binaadam husongwa na wimbi la mawazo kiasi kwamba anashindwa hata kujua ama kufikiria kile anachokifanya muda huo.. na kujikuta anaruhusu makosa kama hayo kutokea... Na si kwamba mtu anafanya makusudi...

Na suala la kuchelewesha shughuli nyingine kwa hatua hizo si tatizo kwasababu, litachukuliwa kama dharura... dharura zipo na haziepukiki
 
Na siku hizi kwa mpesa hatua ya mwisho ni kuhakiki jina la mtu unayemtumia pesa. Nafikiri ni ngumu kwa jina la mtumiwa kimakosa kufanana na lile sahihi lililokusudiwa.
Asante sana, Kuna la kujifunza!
 
Walichoniambia MPESA nimwombe mwizi arudishe hela zangu na ameamua kukaa kimya.
Jina la mwizi ni SAMWELI DEU MWENYE NAMBA 0759548421 na anaolafudhi ya kisukuma yet wanajidai hawawezi kumpata
Umemtumia shilling ngapi?
 
Umeshawahi kuuguwa kichaa? Unafahamu maana ya mtu anapokuwa na dharura na anatuma pesa sehemu? Usubiri dakika 10 ili iweje wakati kabla ya kutuma unaoneshwa mpaka jina la unayemtumia?
Nikuulize... wewe ni binaadam ama ni malaika..??
 
Vodacom wapuuzi sana. Wameshindwa hata kuweka withdraw code ambazo angekuwa anatumiwa anayetuma pesa naye anamtumia aliyemtumia pesa kwa msg ya kawaida.
Upuuzi na ujinga sana
Kwa akili zako ndogo kama za kuku ulitaka iwe mtu anakuuzia bidhaa kwa Mpesa halafu ukiondoka unawithdraw pesa yako?
 
Nadhani huwa unapata Ujumbe kuwa Hakikisha Namba Kabla ya kutuma Fedha zako, Makosa ni yako hapo sio yao!
Voda wako ovyo kwenye huduma kwa wateja especially ukiwa na shida... kama hayajawahi kukukuta unaweza ukabisha....
 
Nakushauri nenda kwenye ofisi zao kama upo maeneo ambayo ni mjini.... unaweza ukapata msaada
 
Voda wako ovyo kwenye huduma kwa wateja especially ukiwa na shida... kama hayajawahi kukukuta unaweza ukabisha....
Hilo lawezekana, ila kwa case ya Mtoa post.. sioni shutuma inayowastahili Vodacom!
 
Utaratibu uko hivyo, ila maranyingi kama mtu amechukua hela nyingi anatupa kabisa simcard
 
Mkuu Hapo usiwablame Voda hata kidogo hata Mimi niliwahi kukosea Japo ka elfu hamsini ila ikapotea kwa sababu Muhusika aliitoa, ni sawa na wewe udondoshe Fedha kisha useme kwanini Polisi wasimtafute aliyeziokota!
Mifano yako haifanani mkuu... je ni kwanini tunasajili line za simu????
 
Polisi pia wanataka pesa.
 
Tunatumia pia Paypal kuagiza vitu nje kwa mtu usiyemfahamu kabisa na kama akichukua fedha zako bila kutuma item anafuatiliwa popote alipo duniani na atakamatwa
PayPal inafanya kazi Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…