M-Pesa sio salama

Hawa wanaowatetea na kukejeli ipo siku itawakuta ndipo watakapokumbuka hii thread
 
Makosa yako mwenyewe unalaumu Voda. Umeingiza namba mwenyewe. Voda wakakuuliza tena hakiki au ghairi,wewe ukasema yes. Sasa kosa la voda nini hapo?Voda sio polisi ujue,nenda polisi
 
Vodacom wapuuzi sana. Wameshindwa hata kuweka withdraw code ambazo angekuwa anatumiwa anayetuma pesa naye anamtumia aliyemtumia pesa kwa msg ya kawaida.
Upuuzi na ujinga sana
Haka ka security mechanisma katam
 
Anachosema ni kuwa kosa la kutumia MPESA ni irreversible?. Mtandao aliotumia kutuma hela ni MPESA wa VODACOM, Mteja aliyetuma ni wa VODA na aliyechukua hela ni wa VODA. Aliwapigia voda kama mteja wao. ili wamsaidie. Hela imetolewa ila VODA sio dhambi kumpigia aliyechukua hela kumwambia awe muungwana kurudisha hela. Inawzekana hujasoma vizuri.
 
Hivi mtoto anapokosea kunywa mafuta ya taa badala ya maji uunabaki ukimhukumu au unatafuta jinsi ya kumsaidia kwanza? Vibao vya barabarani viko kila mahali na bado ajali zinatokea!! hoja yako ni redundant
Unatumia mfano mfu. Ni sawa na kusema mtoto kanywa mafuta unalaumu mafuta badala ya mtoto. Badala ya kwenda hospitali(Polisi) wewe unalaumu mafuta. Haaaaa haaaa
 
Voda wamejitahidi sana kuweka mechanism ya kumuuliza mteja aconfirm kabla transaction haijafanyika. Kama unalijua jina la unayemtumia (hata wale wa mitandao mingine) ni "rahisi" kucheck kabla hujatuma. Anyway, accidents happen na utakuwa na bahato sana kama VODA wataweza kukusaidia
 
japo voda wana mapungufu ila na ww hauko makini maana now wanakuketea jina la umtumiaye kama siyo una hairisha muamala ww ulizembea hapo.

mie nimewahi kosea kuwapigia wakanambia jamaa ametoa kiasi imebaki kiasi flani wakanirudishia kidogo
 
Nashauri badala ya kuushia kulalamikia jf tufatilie sheria inasemaje!
 
Nimesoma vzr na nimemuelewa, lakini hicho mnacholazimsha hakiwezekani, ndo mana kwenye kutuma kuna hatua wamekuwekea ili kuepusha makosa ambayo mwisho wa siku mtawapa lawama kama hizi
 
Hujaibiwa ila umekosea kwa uzembe wako mwenyewe..unaambiwa hakikisha jina kabla hujaweka namba ya siri wewe unaweka tu...pole sana
 
Vodacom wapuuzi sana. Wameshindwa hata kuweka withdraw code ambazo angekuwa anatumiwa anayetuma pesa naye anamtumia aliyemtumia pesa kwa msg ya kawaida.
Upuuzi na ujinga sana
hili wazo liko vyema
 
Kunatakiwa angalau kuwepo na mfumo wa kuzuia kutoa pesa mara tu uipokeapo kwa angalau dakika 10, ili kuwezesha mtumaji kama amekosea aweze kuwasiliana huduma kwa wateja na pesa irudishwe
Hapana huo ni usumbufu.
hela zangu bado nisumbuke.
 
Suppose namba zangu ni 075423678 na niliyokosea inasoma 0754233978 . sometime ni ngumu kuona hiyo namba hapo katikati haswa ukizingatia mazingira niliyotumia hela yalikuwa kwenye gari linalotembea.
Umekosea namba hapo sawa... sasa hata jina nalo ulikosea wakati una confirm mhamala?
 
Uzembe hapo ni wa mtumaji na voda hawana uhakika kama kweli ulituma kimakosa. Lakini mitandao nayo isitoe majibu kirahisi, kama wakiwa na ka utaratibu ka kumtafuta aliyepokea hizo pesa na kujaribu kumisihi azirudishe kama zimetumwa kweli kimakosa kidogo italeta uzito kuliko wateja kutafutana wenyewe kwa wenyewe, wakumbuke kwamba watumiaje hatupo sawa mwingine utakosea atakuwa na busara atukurudishia pesa yako mwingine ndo inakuwa imekula kwako wala hajali!
 


Pole sana siku nyingine jifunze kuperuzi mpesa yako. Ni hivi sasa unaweza kuzuia mwamala wako uliofanya kimakosa kwa mpesa. Fuata maelekezo yafuatayo.

1. Bonyeza *150*00#
2. Chagua namba 7 (my account/akaunti yangu)
3. Halafu chagugua namba 1 (self reversal)
4. Halafu chagua namba 1 (zuia muamala)
5. Halafu cahgua namba 1 au 2
 
Oooh naona ume ambiwa uende police ila wewe umekuja JF
na data zote umeleta JF subri ndani ya dk 10..JF wata kurudishia pesa zako sawa eeeh
 
Mkuu kwani ilikuwa tsh ngap mimi mwenyewe nilisamehe elf30 mshikaji kazila.
 
Kunatakiwa angalau kuwepo na mfumo wa kuzuia kutoa pesa mara tu uipokeapo kwa angalau dakika 10, ili kuwezesha mtumaji kama amekosea aweze kuwasiliana huduma kwa wateja na pesa irudishwe
Hii nmeipenda nadhani mirandao ya cm yote inabidi iichukue mtu akitiwa hera iweze kutoka mpaka angalau ipite dakika kadha kama nusu saa ivi... Cha kufanya hapa tuwatafute hao watu wanatoa hizi huduma yaani makampuni kila wanakopatikana labda wanaweza kuuchukua huu ushaur mzuri sana ila tukiendeleq kukaa nao sisi wenuewe haitasaidia kabisa.
 
Unamvunjia heshima mwenzio bure tu... Sijaona sababu ya kumwita mwizi sanasana wewe ndo tukuite mnyang'anyi mana unataka kumnyang'anya hela yake iliyo kihalali kwenye M.pesa yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…