Filipo
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 9,342
- 5,536
Diwani wa ccm wilayani Mbinga ambaye pia ni mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo amehukumiwa kwenda jela miaka 36 na kutakiwa kurudisha fedha kiasi cha mil 80 alichoiba katika kampuni ya kubangua kahawa aliyokuwa anafanya kazi wilayani humo. Alikutwa na hatia katika makosa 13 aliyostakiwa na moja aliachiwa huru katika hukumu iliyosomwa na hakimu mfawidhi wa wilaya hiyo!