Simiyu: Mwenyekiti wa Kitongoji ahukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kumbaka Msichana wa miaka 13

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Makama ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, imemhukumu kifungo cha kwenda jela miaka 30 Mambo John (30) mkulima na mkazi wa kijiji cha Isengwa kwa kosa la kubaka.
Simiyu.jpg
John ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwanginde ilidaiwa kuwa katika nyakati tofauti kati ya Mwezi January na May 2023 huko Kijiji cha Isengwa ndani ya wilaya Itilima alimbaka mtoto wa kike (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 13 na kumsababishia ujauzito.

Kwa Mujibu wa mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya taifa ya mashtaka wilaya hiyo Mkaguzi msaidizi wa Polisi Jaston Mhule alielezea mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kinyume na kifungu cha 130(1)(2)e na 131(1) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2022.

Jumla ya mashahidi wanne na vielelezo viwili vilitolewa na upande wa mashtaka baada ya ushahidi huo mshtakiwa alijitetea mwenyewe na Makama kumkuta na hatia kwa kosa la kubaka.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Roberth Kaanwa, Mwendesha Mashtaka aliomba Mshtakiwa apewe adhabu Kali ili iwe funzo kwake na kwa jamii ili wazee wenye umri kama yeye waache kuwarubuni watoto na kuwafanyia vitendo hivyo.

Mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na anafamilia inamtegemea, na ndipo Hakimu akamhukumu kifungo cha miaka 30 jela na fidia ya Sh. 500,000 kwa mhanga.

Katika hatua nyingine Mahakama hiyo pia imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Emmanuel Kuyi mkazi wa kijiji cha Mwamapalala Wilayani humo kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike (8).

Kabla ya hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Roberth Kaanwa, Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya taifa ya mashtaka wilaya hiyo Mkaguzi msaidizi wa Polisi Jaston Mhule alielezea mahakama kuwa Mshitakiwa akiwa ni baba mlezi wa mtoto huyo mnamo tarehe 5/5/2023 majira ya mchana huko Kijiji cha mwamapalala ndani ya Wilaya Itilima alimbaka.

Mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na anafamilia inamtegemea, ndipo Hakimu alipomhuku kifungo cha miaka 30 jela.
 
Dah! Mheshimiwa Mwenyekiti katika hili, umezingua. Wewe kwa kweli nenda tu ukapambane na maisha yako mapya ya jela.
 
Kama mtuhumiwa amekiri kosa, bado tu una mashaka kuwa hujauzito sio wake? Aliyekutwa na ngozi ndio kaiba mbuzi mzee
Sasa alikuwa anajitetea mwenyewe, utasemaje amekiri kosa?, sijaona mahali amekiri kosa, zaidi tu ya kuomba apunguziwe adhabu baada ya kukutwa na hatia. Sasa wamedhibitishaje hiyo hatia?
 
Sasa alikuwa anajitetea mwenyewe, utasemaje amekiri kosa?, sijaona mahali amekiri kosa, zaidi tu ya kuomba apunguziwe adhabu baada ya kukutwa na hatia. Sasa wamedhibitishaje hiyo hatia?
Soma hapa mzee "Mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na anafamilia inamtegemea...."

Kuhusu wamethibitisha vipi, hiyo ndio kazi ya Mahakama
 
Soma hapa mzee "Mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na anafamilia inamtegemea...."

Kuhusu wamethibitisha vipi, hiyo ndio kazi ya Mahakama
Ukishajitetea na kukutwa nanhatia, tayari wewe ni mkosaji, na ndio dhima ya yeye kuomba kupunguziwa adhabu, maana defence phase ikioita kinachofuata ni sentencing.., ila alijijitetea
 
Soma hapa mzee "Mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na anafamilia inamtegemea...."

Kuhusu wamethibitisha vipi, hiyo ndio kazi ya Mahakama
Viini vya makosa kwa mujibu wa CPA vime tally hakuna mtuhumiwa ambaye hukiri makosa popote duniani sema viini vya makosa humuumbua
 
Back
Top Bottom