M/kiti UVCCM, Mh Diwani wa CCM ahukumiwa miaka 36 jela

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,342
5,536
Diwani wa ccm wilayani Mbinga ambaye pia ni mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo amehukumiwa kwenda jela miaka 36 na kutakiwa kurudisha fedha kiasi cha mil 80 alichoiba katika kampuni ya kubangua kahawa aliyokuwa anafanya kazi wilayani humo. Alikutwa na hatia katika makosa 13 aliyostakiwa na moja aliachiwa huru katika hukumu iliyosomwa na hakimu mfawidhi wa wilaya hiyo!
 
Pole zake na hongera kwa hatua hzo lakini mbona wale wakubwa zake wanaokula nyingi wapo mtaani 2,are they above the law?
 
hii ilibidi iwafike wakina lowassa rostam mkapa na wengineo kwani wao wamesababisha hasara ya mabilioni ya shilingi
tatizo la nchi yetu ni selective justice kutafuta samaki wadogo na kuwaacha wale wakubwa ambao wizi wao unatingisha uchumi wa nchi yetu.
 
Source ni kipindi cha Habari na Matukio, Radio Free Arfica
 
Acha afungwe tu. Jamaa alikuwa kajirundikia vyeo utadhani hakuna watz wengine wanaoweza kushika nyadhifa alizokuwa nazo.
Manake 1) Diwani
2) M/kiti uvccm
3) Katibu wa mbunge Komba a.k.a mlalaji wa mjengoni.
4) Usikute alikuwa pia balozi wa nyumba 10, au M/kiti kitongoji
Aende sasa akagombee na unyapara kule lupango.
 
Diwani wa ccm wilayani Mbinga ambaye pia ni mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo amehukumiwa kwenda jela miaka 36 na kutakiwa kurudisha fedha kiasi cha mil 80 alichoiba katika kampuni ya kubangua kahawa aliyokuwa anafanya kazi wilayani humo. Alikutwa na hatia katika makosa 13 aliyostakiwa na moja aliachiwa huru katika hukumu iliyosomwa na hakimu mfawidhi wa wilaya hiyo!

Kumbe hata mapacha watatu watakuwa walianzia mbalin sana, huko uvccm ndo wanakofundishwa kufisadi mali za umma.

Bahati mbaya kwa huyu diwani ameshindwa kujinusuru na mkonon wa sheria.
 
hawa mbona ni kawaida yao ila mmoja mmoja ndiye hukamatwa na sijui kwa nini wanapewa nafasi za kutumikia umma hali ni wachafu Mungu irehemu nchi yangu Tanzania
 
Back
Top Bottom