Lyrics za nyimbo za kiswahili

Wasanii wa sasa wamekalia kuimba mapenzi wakati nchi imejaa matatizo kama ya ufisadi lakini hakuna hata mmoja anatunga nyimbo za kupinga maovu
 
Na huyu nani? Bendi gani?

Baba Anna eee

Ni lini utarudia nyumbani

Uje uwaone watoto wako

Uje uwaone baba na mama kwenu.......

(repeat)

[Lead]

Najua kazi nyingi zimekuzonga...

Huko uliko nako ni mbali sana baba Anna eeeee

Hata hivyo ufanye kila njia.....kwani kuna matatizo matatizo matatizo kwenu eeee

(Chorus)

[Wote]

Watoto wako wanakukumbuka...kila siku haweshi kukuuliza

Na mama naye ananung'unika....kwani miaka mingi imepita

Baba amekuwa mtu mzima...hawezi kuhangaika huku na kule

Kwa hiyo bwana ufanye haraka...matatizo yametuzidi mno yooooo

Fanya uje eeee

[Lead]

Leo nasema aaa......mimi naomba.....niko peke yangu.....

Maisha ya tabu.....kila kitu ni pesa.....chakula ni pesa....

Mavazi ni pesa.....ufanye haraka...bwana naomba eee

[Wote]Fanya uje eeee

Marijan Rajab akiwa na Dar International'
 
Mapenzi ni kuvuliana, nami mpenzi nimekuvulia...
Mapenzi ni kujamiiana, nami mpenzi nimekuamini.....
Mapenzi ni kuhushumiana, nami mpenzi nimekuheshimu...

Kama nyota na mwezi vilo mwanana angani, tung'arishe penzi letu sote..
Tupeane penzi bila choyo chochote na bila hiyana kwetu sote...
Elewa mapenzi ni chombo kinachotuunganisha....
Elewa mapenzi ni chombo kinachosafiri kati ya mioyo yetu ilo thabiti.
Tulizana mpenzi tutondane, tulizana mpenzi, tupembane.

Mpenzi wangu naahidi kuwa kama mto unaomwaga maji kwenye bahari bila kukinahi.....
 
hivi wapi nitapata lyrics za nyimbo za kiswahili kama Siwema,Kifo by Dr Remmy Ongala,Jojina na zile nyimbo za sikinde pleaseeeee!.

xoxo
Kelly01

we si mswahili? nilidhani utahitaji tungo za kingreza (kingereza)
 
Hapo najua kuna sehemu sehemu nitakuwa nimechapia, si unajua nyimbo hazina CD yenye booklet ya lyrics wala website ya fanbase, kwa hiyo unakumbuka ulivyosikia tu.

Halafu miaka kibao imepita.

- Kaulimtu mkuu acha hizi za kuchapia chapia katika zero tolerance nation, bwa! ha! ha! ha!

Es!
 
hivi wapi nitapata lyrics za nyimbo za kiswahili kama Siwema,Kifo by Dr Remmy Ongala,Jojina na zile nyimbo za sikinde pleaseeeee!.

xoxo
Kelly01

Kelly, ebu bembea na link hii...it brings the memory back...[ame="http://www.imeem.com/people/EoDdzIm/playlist/2W6RC-Z0/zilipendwa-music-playlist/"]ZILIPENDWA - MP3 Music Streams on IMEEM@@AMEPARAM@@http://media.imeem.com/pl/ITlyL9fZmN/aus=false/@@AMEPARAM@@ITlyL9fZmN[/ame]
 
Maria eeh,
Mary eeh

Kwa kweliii sasa nimepatwaa eeeh, Sina ujanja eeeeeh eeeh
Kupendaaa sawa na ajaliiii, haina kingaa eeeen
Nilivyomuhusudu mtoto Mary, sijapata kupenda toka nizaliweee
Na wala sintopenda mpaka kufa, mpaka kufa, Mama Mary oooh

Nasonoonekaaa ah mamaah, nasononekaaa eeeeh
Na nimezama kwenye dimbwii oooh la mapenzi.....

Huyu nani? bendi gani?
 
Mwanamema alimchanganya akili bwana Musa, hadi akiona unyasi anashtuka akifikiri ni NYOKA. Huyo alikuwa ni jabari la Muziki Marijan Shaaban (RIP). Nilifanikiwa kumuona huyu mzee LIVE pale Dar na kibendi mshenzi, machozi yalinitoka kwa furaha na majonzi. Sikuamini kuja siku moja kumuona live tena hata watu hawana time naye ila majonzi yalikuwa kumuona akiwa na kibendi mshenzi Kunduchi beach hotel..... Na hobby yangu kubwa ya muziki, milele nitamuenzi huyu mzee. Ule wimbo wa Mkuki Moyoni na Hanifa (Bamping style) zilinifanya nimuone kama nyota ya Tanzania baada ya sallum Abdallah...
 
Kelly na wengine wote mliochangia nawashukuru kwa kutupeleka miaka ile ambapo muziki ulikuwa muziki.
Nitashukuru sana kama kuna atakayeweza kuniwekea maneno ya wimbo uliowahi kuimbwa na Fresh Jumbe enzi hizo ( nadhani late 80s) akiwa na Mlimani Park unaitwa " "Conjesta" - wimbo huu unaimbwa siku hizi na In Afrika Band ( kina Roy, Bob Rudala, Biz man na wengineo ) na wanaupiga vizuri mno kama kopi.
ninakumbuka baadhi ya maneno kama ifuatavyo:
Nimetembea, pande za dunia, mashariki na magharibi,
Sijapata kumpata mwingine mwenye mapenzi ya kweli....
Na sasa kwako mpenzi, nimefikia ukingoni ....

nitashukuru sana kama mwenye maneno yote atuwekee hapa.
 
Sitegemei kupenda mwingine tena zaidi yako wee Konjestaaaa...

Mtoto mwenye imani, ooh jesta nimeamua kukupenda wee pekee duniani
mtoto mwenye imani, ooh jesta nimeamua kukupenda wee pekee duniani.

Mapenzi mazito, sioni mwingine,wala sisikii la yeyote yule

Haya kazi kwako
 
Mkuu Ye
Ubarikiwe sana.
 
"Sabah al Kheri Mpenzi"
I remember someone inquiring about this Old Taarab song found the Lyric by chanceon the Web:
An old Taarab/Swahili song by Culture Musical Club Zanzibar. (Lyrics)
-Sabah al kheir mpenzi waonaje hali yako
-sabah an nur Aziz hali yangu kama yako
-Wa'waonaje wazazi nyumbani utokeapo
-kawanusuru mwenyezi hofu yao juu yako
ebu nitoe majonzi unijuze shida yako
shida yangu sijiwezi dawa yangu sura yako
(mwenginewe hachomozi nakupenda peke yako)
(daima n'takuenzi silitupi pendo lako)
-usi'ingie simanzi sura yangu mali yako
-na kuikosa siwezi sikia langu tamko
-mwenginewe hachomozi nakupenda peke yako
-nimefanya uchunguzi nakiri maneno yako
naiyona waziwazi ishara ya pendo lako
-milele n'takuenzi natoa ahadi kwako
(mwenginewe hachomozi nakupenda peke yako)
(daima n'takuenzi silitupi pendo lako)
-kibaya sikivumbui ndani ya maungo yako
-na mimi simtambui mwenye sifa kama zako
-rangi yako ya samawi kama sufi ngozi yako
-na kuzikosa haiwi cheko na bashasha zako
wallahi sijichukuwi mgonjwa kwa raha zako
-ukaidi siujui mimi mar'dhia kwako
(mwenginewe hachomozi nakupenda peke yako)
(daima n'takuenzi silitupi pendo lako)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom