Lyrics za nyimbo za kiswahili

Tupeane michoro basi dadangu kama hizo mission town zinalipa.

Zinalipa vibaya sana!na uchumi mbaya lakini bado nadunda tuu can you imagine that?...hahahahahaha..anyways miye sichezi dili na wabongo ndugu yangu wasije niharibia bure maana ni wana roho za kwanini....wataniliza bure.
 
Zinalipa vibaya sana!na uchumi mbaya lakini bado nadunda tuu can you imagine that?...hahahahahaha..anyways miye sichezi dili na wabongo ndugu yangu wasije niharibia bure maana ni wana roho za kwanini....wataniliza bure.


Nipe hint basi lakini asiniambie Primerica or Meleleuca or life insurance tell me something different please.
 
Nipe hint basi lakini asiniambie Primerica or Meleleuca or life insurance tell me something different please.

hahahaah i did life insurance a while back in 2002......hahaha sasa nikikupa si ndiyo manake nimeshakwambia what it do you know....But not close to Ben madoff....yule ni classic mission town aisee!...But mostly niko based kwenye investment.
 
hahahaah i did life insurance a while back in 2002......hahaha sasa nikikupa si ndiyo manake nimeshakwambia what it do you know....But not close to Ben madoff....yule ni classic mission town aisee!...But mostly niko based kwenye investment.


Is it morgage or real Estate or Stocks what is it ?
 
Yule wa DC siyo mwizi bana..isitoshe mission town zangu ni legit......muda wote natumia G1(goole phone)


Hii imekaaje yule wa DC siyo mwizi lakini mission zako ni legit hivyo zake hazikuwa legit lakini siyo mwizi.
 
Sikonge umeijuaje hii site...i had no clue aisee ipo very alright.thank you aisee.Kumbe saa nyingine ina make sense kuuliza eeeh.

Jamaa kapewa ki-web space tu na mahost, lakini naona kakitumia ipasavyo.... I really liked the way how simplified the site is not forgetting the quality and quantity provided. Amejitahidi sana... anahitaji support kwa kweli. Thanks to Sikonge kwa kiunganishi kile na nikushukuru wewe pia kwa kuuliza swali hapo juu.

SteveD.
 
Tulipo toka ni mbali sana,
mapenzi yetu, yalianza na vikwazo vingi..
Polisi tumeenda mahakamani tumefika hata hivyo kwa nguvu za moola tumeshinda......................

Nakusifu sana..
Kwa kuweza vyema...
Kukabiliana na wimbi la wafitini.....
Na leo hii, tuko pamoja pia....
Tukiwa tumetuilia bila wasiwasi wowote
 
Jamaa kapewa ki-web space tu na mahost, lakini naona kakitumia ipasavyo.... I really liked the way how simplified the site is not forgetting the quality and quantity provided. Amejitahidi sana... anahitaji support kwa kweli. Thanks to Sikonge kwa kiunganishi kile na nikushukuru wewe pia kwa kuuliza swali hapo juu.

SteveD.


SteveD,
Nafurahi umeliona hilo. Nafikiri kama jamaa kapewa space ndogo basi ingelikuwa heri aandikiwe na aje apewe space kubwa hapa ndani ya jamii forum na jina lake libaki hilohilo. Jamaa hata mie alinifurahisha maana ni siku nyingi sana nilikuwa sijaingia hadi hiyo jana. Ikiwezekana basi kuwe na uwezekano wa kuunganisha nyimbo na hizo lyric yaani unaona wimbo unaamua kuchagua kusikiliza au kusoma maneno au vyote pamoja.
 
Kelly wala sikumbuki nilianzia wapi kuijua. Ila nakumbuka kupata ujumbe tuwe tuanachangia kuweka maneno. Nafikiri kama sikosei ni miaka ya 90 wakati nikiwa member wa Tanzanet forum. Ila naona kwa sasa wana nyimbo nyingi sana. Huwa nikitaka kufika huko naandika wimbo wa Tx Moshi akiwa POLISI JAZZ wa "unalewa bila kipimo". Huu wimbo kwa kweli naupenda sana na hamna sehemu unaweza kusikiliza. Ukiandika kwenye google zinatokea kama site mbili, moja ni humu JF na ya pili ni hiyo.
Inabidi HONGERA zimfikiei Tizedboy na wote waliochangia. Kama ikiwezekana, basi JF waisaidie hii site na kuiwekea LINK moja kwa moja kutoka humu JF. Nafikiri hiyo tumuachie Tizedboy mwenyewe. Vinginevyo JF itaanza kuwa kama Microsoft, ikipita na kuuwa au kununua vikampuni vidogovidogo. Na hii siyo nzuri sana.
Mwanzo niliandika kwa kufikiri jamaa kaweka nyimbo chache tu. Ila nilipoingia MAINPAGE duu, nimekubali. Mod's yale maneno yangu ya kwanza ya kutengeneza sehemu ya Lyrics za Kiswahili, muachane nayo. Ila kibidi kuisaidia hiyo site basi itakuwa vizuri maana ni nzuri na jamaa kajitahidi ila ndiyo haijulikani.


..Mkuu Sikonge, Nadhani baada ya kutoka huko Tanzanet Tizedboy alianzisha forum kwa ajili ya lyrics za nyimbo za kiswajhili kwenye DarHotwire ya mwanzo ambayo ilipata mushkeli wakati fulani na kupoteza kumbukumbu zote ndipo wakaunda iliyopo sasa. Hii ilikuwa kama miaka mitano/sita hivi iliyopita. Nadhani Tzboy aliweza kutunza baadhi ya nyimbo ambazo ndio unaziona kwenye anuani uliyoweka hapo. Mimi ni miongoni mwa tuliochangia sana kuubandika maneno ya nyimbo hizo kama utakavyoona mwenyewe. kama ulivyoshauri, sio vibaya iwapo JF itaweka link ya kwenda huko, hii yote ikiwa ni katika kuenzi muziki wetu wa nyumbani. Naunga mkono hoja kwa asilimia 100!
 
Sikonge umeijuaje hii site...i had no clue aisee ipo very alright.thank you aisee.Kumbe saa nyingine ina make sense kuuliza eeeh.
Kuuliza inasaidia sana aisee....unawasaidia hata wale wasiojua waulize nini.
 
Kelly,
Samahani hiyo anwani niliyokupa nimeanzia ndani. Ukianzia main page ndiyo unaona nyimbo zote na Watz walijitahidi kwani wameandika wengi sana.
Angalia huo ukurasa kwa kuanzia hapa:-

Mziki kutoka Tanzania

Sikonge, asante kwa hii link. Pia asante kwa muanzishaji wa thread Kelly. Yani nimepata wimbo wa marehemu Niko Zengekala. Wakati nakua nilielezewa huyu jamaa alikuwa kipofu, sasa katika huu wimbo kuna sehemu analalamika kuwa "Kumbe ulikua ndani ukichungulia dirishani...". Sasa nilimuuliza aliyenieleza alionaje?, ndio akaniambia kuwa alisindikizwa na rafiki yake ndio alimwambia, ama kuna mtu alitoa siri. Nilikuwa nikiusikia huu wimbo enzi za utoto wangu ilikuwa naumia sana, kwanini mtu amdanganye kipofu?. Kupitia huu wimbo ndio ukapatikana usemi "kuachwa Solemba". Soma huu ubeti:-

Nilichomwa na jua toka asubuhi,

mpaka saa nane Solemba sababu ya kukungoja wewe

Kumbe ulikua ndani ukichungulia dirishani

Nimeshituka Solemba ,

Nimeshituka Solemba
 
Nauliza nani anajua wimbo wa Mariam na selemani uliimbwa na bendi gani? nitaupata wapi .Nakumbuka majibu mariam akiuliza ' yapata mwaka na nusu hajasikia lolote kutoka kwa mchumba selemani aliyekwenda mjini kutafuta kazi.selemani alimjibu Mariam" kusema kweli nimekutwa na mambo ya mjini"
 
Mpenzi Luta nasikitika sherii!ehee!
Yoyoyo kuishi tena na wewe
Mama yo vituko vyako vimezidi !
Vimenichosha oo mupenzi!
Nashindwa hata la kufanya

Nilikuwa nikikukuonya hukutaka kunisikia!
Najuta yoyoyoo! Kuishi nawe
Masikini miye mamaaaa kwa kweli sina raha



Sasa umeipatapata iyo mama Luta !
Tazama sasa maisha yako yamebadilika!
Ubishi wako mpenzi wangu ukweli umekuponza
Hukutaka kusikia cha mume!
Sasa yamekukuta
Dunia ya leo Luta! nenda pole pole ..............
 
Kama wewe ulinipenda
Kwa nini kunidanganya bwana wee
Kujibandika madaraka siyo yako bwana wee we

Unadhurura mchana kutwa
Kupita kuranda randa mitaani
Kumbe hukuwa na uwezo kwa nini kunidanganya
Nikuelewe vipi?
Babu eee uaminifu wako uko wapi ?mamaaa

(Chorus)

Usinione bwege mamaaa.....Kalubandika eee
Kwa kukubali mwito wako Kalubandika ee
Hayo yote ni matatizo ya dunia mama aa


Akiingia kwenye baa kazi yake kuomba bia
Hana hata aibu sigara pia anaomba
Mitaani na kwenye masoko
Hujitangazia kuwa yeye ni kmkurugenzi wa kampuni fulani
Kumbe sio hivyooooo


Usinione bwege mamaaa.....Kalubandika eee
Kwa kukubali mwito wako Kalubandika ee
Hayo yote ni matatizo ya dunia mama aa


Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto ee mama
Kumbe bwana yule hana kitanda wala shuka
Pa kulala hana, analala kwenye stendi ya Basi!
Pa kulala hana, analala kwenye kituo cha uda Kalubandika yeyeee
Wacha vituko we bwana


Usinione bwege mamaaa.....Kalubandika eee.........
 
gal frendi wa shemeji yangu mistari kama hii eti....

Tamu kama asali Ndefu kama mpini
Urefu nchi ishirini lazma uchoke ulimi
Wengi wanajiuliza unanipendea nini?
Hiyo ni siri yetu tu wewe na mimi
Hawajui pipi ya kijiti ndio inajenga shepu
Masugar daddy kila siku wanabugi stepu
Raha ya pipi ya kijiti kula bila maganda
Pata raha halisi usisikilize propaganda
Pipi nzuri inanukia hata siku moja hainuki
Ndio maana inafichwa haiachwi uchi
Pipi ya demu wangu mtu mwingine simpi
Ni hatari kama serikali kubinafsisha nchi

aaaaaah......unanisoma?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom