Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,923
- 31,167
huyo lazima aondoke, amecheza na Maalim Seif. Yeye alitarajia apige kelele za CUF kutumia fedha nyingi kujijenga Zanzibar pekee badala ya bara halafu wamuache. Ndio maana pamoja na wajumbe wa bara kumpa kura nyingi na kumfanya aongoze kati ya waliopigiwa kura kwenye baraza la uongozi na kumzidi hata Haji Duni bado ametoswa!. Maalim Seif alimwambia wazi Lipumba asipendekeze jina lake. Huyu hakugombea akashindwa bali jina lake halijapendekezwa kabisa na mwenyekiti wao kwa kushauriana na katibu mkuu. Kimbelembele chake cha kupinga upemba ndani ya CUF ndio kimemponza. Kila siku ilikuwa kulilia tu chama hicho kijijenge bara kumbe wenzake wana ajenda nyingine kabisa
...........ndiyohiyo
Naweza kukubaliana na wewe katika hili Mkuu Habarindiyohiyo.
Ajenda za CUF ni Zanzibar tu ukija na mkakati mwingine tofauti na maalim Seif & co wa kutaka kujitanua huku bara lazima watakukimbiza.Bwana Lwakatare kajimaliza mwenyewe kukimbilia chama cha wapemba angemwuliza James Mapalala yaliyomkuta.