Mkuu hapa tunaongelea shujaa kuhamisha viwanja, hayo yagenereta yana nafasi yake!
Tangiapo kuwa chama kimoja haina maana kila mtu hana ubongo wake wa kufikiria na kutoa maoni yake! Na kuwa kiongozi haina maana wewe ni
SI unitT ya unao waongoza, lazima uwasikilize maoni yao ndo gurudumu litasonga, huwezi ukawa good leader kwa mtindo wa 'one man show', and for CUF's case 3 man show, never!'
Hamna cha kuhamisha viwanja CUF haiongozwi na watu watatu kama unavyotaka tuamini,kile ni Chama Cha Wananchi ,wao ndio wadau ,sasa kama kulikuwa na wafuasi wa Lwakatare ndio hao umeona wamemfuata ila kama kulikuwa na wapambanaji wanaokiunga mkono Chama Chao wao watabakia na kuendeleza mapambano hadi kieleweke,hawatobabaika na kiongozi kuhama Chama ,hata Seifu au Lipumba wakibwaga manyanga basi wapo watakaozuka na kusimamisha bendera ya CUF ,maana Lwakatare huwezi kumpambanisha na Shaibu Akwilombe kwa wanaomfahamu ameondoka CUF kumezuka wepya.
Hata hivyo CUF kama Chama haina nafasi na wanaotetereka ambao utendaji wao unawalakin kama huyo Lwakatale ,na zaidi ni kwa wananchi wa upande wa bara (Tanganyika) msimamo wao unaeleweka vizuri sana na WaZanzibari wanawaelewa wenzao wa Tanganyika ,kwa hivyo nataka unielewe kuwa msimamo wa wananchi wa Zanzibar si kwa viongozi bali ni kuikataa CCM ,kama huelewi wananchi waZanzibar wanawaelewa viongozi wao na wanawafuatilia ,inawezekana huelewi kinachoendelea ,kwa kukukatiza tu kuna viongozi wengi wa CUF upande wa Pemba (Wawakilishi na wabunge)wameshanunuliwa na habari zimeshafika makao makuu na zinafanyiwa kazi,haina haja ya kumwaga mtama hapa .dont play with CUF security ni hatari sana,kuna yule muwakilishi wa Magogoni ,kesi yake sijui kama uliisikia ,yule aliitwa na Karume Ikulu ,aliporudi tu akelezwa yote aliyopatana ,ila CUF wanajua kuplay political games international wakamuachia kwani lengo lao sio kushinda kile kiti bali walitazama mbele zaidi ya kitakachojiri ambacho kimewaangusha CCM japo hilo jimbo walishinda.Na hivyo kilichomuondoa Lwakatare kinajulikana na kosa alilolifanya linajulikana na yeye mwenyewe analijua ,sasa huko Chadema ndio amekwenda na ameondoka na wengine pamoja na wafuasi,unaweza kuona kama CUF imepata hasara lakini kwa interest za Chama hakuna hasara ila ni faida katika kukijenga Chama ,sasa nakupa mtihani katafute Lwakatare alifanya nini na ni kipi kilichomuangusha katika siasa za CUF.
Na pia uelewe kuwa CUF bado ni Chama kichanga ambacho kimo katika kujijenga na CCM wanakielewa sana ,na zaidi CCM wanaitolea salute security ya CUF na wanaiogopa sana,usalama wa Taifa umegonga mwamba katika kuifuatilia Core system ya security ya CUF.Hivyo usishangilie sana ,mambo ya siasa hayataki papo kwa papo,weka masikio wazi baada ya miezi sita,kwa kukumegea tu Pemba inatutoka ?