Hizi habari hazina ukweli kwani hajafungwa ila kapewa onyo na mahakama.
Hajafungwa nimezungumza naye kwa simu sasa hivi na anarudi Dar keshokutwa jumamosi jioni .
Mjadala ufungwe kwani hakuna kitu kama hicho.
ukweli zinazo na hii hapoa news kwenye majira
Lwakatare wa CUF afungwa miezi 15
Habari Zinazoshabihiana
Lwakatare (CUF) vs Kagasheki (CCM) kortini kesho 09.10.2007 [Soma]
Pingamizi la Kagasheki dhidi ya Lwakatare kusikilizwa leo 17.10.2007 [Soma]
Jaji apiga marufuku wanasiasa 10.10.2007 [Soma]
Na Theonestina Juma, Bukoba
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa Kagera, imemhukumu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Wilfred Lwakatare (45) kifungo cha miezi 15 baada ya kupatikana na kosa la kumtishia Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu na kufanya fujo baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo mwaka juzi.
Hata hivyo, kifungo hicho cha miezi 15 ni cha nje, ambapo kwa kipindi hicho, Naibu Katibu huyo ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini, kwa kipindi hicho hatatakiwa kutenda kosa lolote kuanzia jana, baada ya hukumu hiyo kutolewa.
Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Wilbard Mashauri, baada ya kuridhika na upande wa ushahidi wa mlalamikaji, na hata hivyo kutokana na wananchi kutojua kuwapo kwa kesi hiyo jana wengi hawakuwa mahakamani hapo.
Katika kesi hiyo namba 455 ya mwaka juzi, ambayo Mwendesha Mashitaka wake alikuwa ni Mkaguzi wa Polisi, Shaweji Alawi, ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 15 mwaka juzi saa 5.15 asubuhi katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu Bukoba Mjini.
Katika kesi hiyo, mlalamikaji ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu katika Jimbo la Bukoba Mjini, Bw. Faustine Fissoo, aliwasilisha madai mawili ambayo yalikuwa ni pamoja na Bw. Lwakatare kumtishia kwa kumwambia kuwa "nitakuonesha cha mtema kuni au niingie msituni," pamoja na kutumia lugha chafu dhidi yake.
Lugha chafu hiyo aliibainisha kuwa ni pamoja na Msimamizi kula njama na polisi na Rais Mtaafu wa Awamu wa Tatu, Bw. Benjamini Mkapa kutaka kuwaangusha katika uchaguzi huo.
Hata hivyo, kati ya madai hayo mawili, madai ya kwanza ndiyo Mahakama iliyatumia katika kumtia hatiani mwanasiasa huyo ya kumtishia Msimaizi na kufanya fujo ambayo kwa upande wa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa mlalamikaji, ilithibitika.
Aidha, madai ya pili ya kutumia lugha chafu yalitupiliwa mbali na Mahakama kutokana na upande wa mlalamikaji kushindwa kuthibitisha.
Kwa upande wa mlalamikaji ambao ulikuwa na mashahidi wawili ambaye ni pamoja na Katibu Muhtasi wa Msimamizi huyo, Bibi Alice Mugomba na Msimamizi wa Uchaguzi huo, Bw. Fissoo. Mlalamikiwa alikuwa na mashahidi wanne.
Akitoa utetezi mahakamani hapo, Bw. Lwakatare alikana kutamka maneno hayo na kwamba siku ya kutangaza matokeo alifika na kuingia ndani na kumwambia Msimamizi kwamba utaratibu aliotumia kutangaza matokeo, ni kinyume na alimwomba asitangaze matokeo kwani katika nchi zingine husababisha rabsha na watu kuingia mstuni.
Alitaja nchi kama hizo ambazo watu wake wameingia msituni kuwa ni pamoja na Uganda, Kodivaa, Serbia na Morisi katika mazingira kama hayo.
Hata hivyo, kwa upande wa utetezi wa mlalamikiwa ambaye alikuwa akitetewa na Wakili wa kijitegemea, Bw. Twaha Taslima, aliiomba Mahakama kutupilia mbali ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kwa upande wa mlalamikaji kwa madai kuwa mashahidi wote walikuwa na uhusiano wa kikazi.
Alidai kuwa Katibu Muhtasi wa Msimamizi huyo, angeweza kuamriwa na bosi wake kusema atakavyo.
Hata hivyo, katika hilo, hata Mahakama pia iliangalia upande wa mashahidi wa mshitakiwa ambapo mashahidi wake wawili walikuwa na uhusiano wa kikazi na mshitakiwa huyo.
Mashahidi hao walibainishwa na Mahakama hiyo, kuwa ni pamoja na mashahidi wawili, Bw. Henry Mambo, ambaye wakati wa uchaguzi huo alikuwa ni wakala wa Bw. Lwakatare na shahidi namba tatu Bw. Ignatius Robozi alikuwa mshauri wa mshitakiwa huyo.
Hivyo, kutokana na kigezo hicho, Makahama iliamua kutotupilia mbali ombi la wakili wa Bw. Lwakatare la kutaka mashahidi hao watupiliwe mbali kutokana na kila upande kuwa na mashahidi wenye uhusiano kikazi.
Pamoja na hayo, kabla ya kutiwa hatiani, Bw. Taslima aliwasilisha maelezo yake juu ya mteja wake, ambapo aliiomba Mahakama kutoa adhabu ndogo kwa mteja wake kutokana na mshitakiwa huyo, hana rekodi ya kutenda kosa na kwamba ana familia ya watoto wanne, wadogo na mke ambao wote wanamtegemea.
Pia alisema ana watoto wanne wa marehemu kaka zake ambao wanamtegemea na kwamba akipewa adhabu kwa kipindi kirefu itawaondosha watoto hao nyumbani kwake.
Hali kadhalika alibainisha kuwa mshitakiwa huyo anasumbuliwa na kisukari ka kipindi kirefu tangu mwaka 1997 amekuwa chini ya uangalizi wa daktari.
Pia, Bw. Taslima aliiomba Mahakama kuangalia nyadhifa alizonazo mshitakiwa katika jamii na Taifa kwa ujumla, kwamba ana madaraka makubwa taifani, akiwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, kutokana na hilo yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini na kutokana na hilo, kumwondoa kwa muda mrefu katika jamii, itakuwa ni kuinyima nchi nzima mchango wake wa maendeleo ya Taifa.
Pia kutampunguzia kasi ya ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini na kwamba akiondolewa kwenye uhuru alionao kwa sasa mchango wake pia utaondolewa katika jamii ya Watanzania.
Mahakama ilizingatia maelezo ya wakili huyo na kutupilia mbali maelezo yake juu ya nyadhifa alizonazo taifani na hivyo kumtia hatiani kutumikia kifungo cha nje cha miezi 15 bila kutenda kosa lolote kwa kipindi hicho kuanzia jana hukumu hiyo ilipotolewa.
Akimtia hatiani, Hakimu Mashauri alisema pamoja na madai ya Lwakatare kuwa msimamizi wa uchaguzi kutangaza matokeo, wakati yeye hakuwapo hata kumfanya achukie na kutamka nchi ambazo zimeweza kuingia mstuni kutokana na hali hiyo, si kwamba Bw. Lwakatare alikuwa anamtishia msimaizi wa uchaguzi Mkuu wa Uchaguzi wa Bukoba Mjini bali pia alitishia usalama wa Taifa, pamoja na kuwapo machafuko katika nchi alizozitaja, lakini bado zinagharimu roho za watu wa nchi hizo.
Hivyo, Mahakama ilimtia hatiani kwa kutumikia ifungo cha miezi 15 nje, na kwa kipindi hicho hatakiwi kutenda kosa lolote.
Hii ni mara ya pili mwanasiasa huyo kufikishwa mahakamani, kwani Oktoba 17 mwaka huu, Mahakama ya Wilaya ya Bukoba, ilimwachia huru, baada ya kukabiliwa na mashitaka ya kumpiga mwandishi wa habari, Bw. Renatus Mutabuzi wa ITV.