Lwakatare Afungwa miezi 15

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Naibu Katibu wa chama cha wananchi (CUF) upande wa Bara Bw. Wilfred Lwakatare amehukumikwa kifungo cha miezi 15 baada ya kupatikana na hatia na makosa ya kufanya vurugu na kumtishia msimamizi wa uchaguzi... more news to come...
 
Duh...Mungu ampe ujasiri atumikie hukumu yake then arudi tena uwanjani kuichachafya ccm kwa hoja.
 
Inaniuma sana sana , na nitajitahidi kwenda kumtembelea huko mahakamani ili kumpam pole kijana huyu amabye amejitahidi kutetea taifa lake.

Hili ni pigo kubwa sana kwa wapenda maendeleo wote na wapenda nchi wote.

Poleni sana wana CUF na wananchi wote kwa ujumla.
 
Inaniuma sana sana , na nitajitahidi kwenda kumtembelea huko mahakamani ili kumpam pole kijana huyu amabye amejitahidi kutetea taifa lake.

Hili ni pigo kubwa sana kwa wapenda maendeleo wote na wapenda nchi wote.

Poleni sana wana CUF na wananchi wote kwa ujumla.

ni kifungo cha nje yaani anaweza kufanya kazi zake zote hata zile za nyumbani eeeh cha muhimu asifanye kosa lolote ktk kipindi anachotumikia adhabu.

hili liwe fundisho kwa wanaowanyanyasa maafisa wa uchaguzi iwe tawala au tawaliwa
 
ni kifungo cha nje yaani anaweza kufanya kazi zake zote hata zile za nyumbani eeeh cha muhimu asifanye kosa lolote ktk kipindi anachotumikia adhabu.

hili liwe fundisho kwa wanaowanyanyasa maafisa wa uchaguzi iwe tawala au tawaliwa


OK, hapo sasa naelewa. Hivi si ndivyo tulivyokuwa tunajua tangu mwezi wa kumi,sasa hii habari imetoka wapi na kwa nini imeletwa tena hapa, kazi kurusha watu roho bure tu hapa! Acheni watu tukajadili mambo ya REDET kule bwana.
 
Hizi habari hazina ukweli kwani hajafungwa ila kapewa onyo na mahakama.

Hajafungwa nimezungumza naye kwa simu sasa hivi na anarudi Dar keshokutwa jumamosi jioni .

Mjadala ufungwe kwani hakuna kitu kama hicho.
 
Hizi habari hazina ukweli kwani hajafungwa ila kapewa onyo na mahakama.

Hajafungwa nimezungumza naye kwa simu sasa hivi na anarudi Dar keshokutwa jumamosi jioni .

Mjadala ufungwe kwani hakuna kitu kama hicho.

Big relief! Jamani habari sensitive kama hizi tuwe tunachukua muda kabla ya kuzipachika hapa.
 
Hizi habari hazina ukweli kwani hajafungwa ila kapewa onyo na mahakama.

Hajafungwa nimezungumza naye kwa simu sasa hivi na anarudi Dar keshokutwa jumamosi jioni .

Mjadala ufungwe kwani hakuna kitu kama hicho.

ukweli zinazo na hii hapoa news kwenye majira

Lwakatare wa CUF afungwa miezi 15

Habari Zinazoshabihiana
• Lwakatare (CUF) vs Kagasheki (CCM) kortini kesho 09.10.2007 [Soma]
• Pingamizi la Kagasheki dhidi ya Lwakatare kusikilizwa leo 17.10.2007 [Soma]
• Jaji apiga marufuku wanasiasa 10.10.2007 [Soma]

Na Theonestina Juma, Bukoba

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa Kagera, imemhukumu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Wilfred Lwakatare (45) kifungo cha miezi 15 baada ya kupatikana na kosa la kumtishia Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu na kufanya fujo baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo mwaka juzi.

Hata hivyo, kifungo hicho cha miezi 15 ni cha nje, ambapo kwa kipindi hicho, Naibu Katibu huyo ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini, kwa kipindi hicho hatatakiwa kutenda kosa lolote kuanzia jana, baada ya hukumu hiyo kutolewa.

Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Wilbard Mashauri, baada ya kuridhika na upande wa ushahidi wa mlalamikaji, na hata hivyo kutokana na wananchi kutojua kuwapo kwa kesi hiyo jana wengi hawakuwa mahakamani hapo.

Katika kesi hiyo namba 455 ya mwaka juzi, ambayo Mwendesha Mashitaka wake alikuwa ni Mkaguzi wa Polisi, Shaweji Alawi, ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 15 mwaka juzi saa 5.15 asubuhi katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu Bukoba Mjini.

Katika kesi hiyo, mlalamikaji ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu katika Jimbo la Bukoba Mjini, Bw. Faustine Fissoo, aliwasilisha madai mawili ambayo yalikuwa ni pamoja na Bw. Lwakatare kumtishia kwa kumwambia kuwa "nitakuonesha cha mtema kuni au niingie msituni," pamoja na kutumia lugha chafu dhidi yake.

Lugha chafu hiyo aliibainisha kuwa ni pamoja na Msimamizi kula njama na polisi na Rais Mtaafu wa Awamu wa Tatu, Bw. Benjamini Mkapa kutaka kuwaangusha katika uchaguzi huo.

Hata hivyo, kati ya madai hayo mawili, madai ya kwanza ndiyo Mahakama iliyatumia katika kumtia hatiani mwanasiasa huyo ya kumtishia Msimaizi na kufanya fujo ambayo kwa upande wa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa mlalamikaji, ilithibitika.

Aidha, madai ya pili ya kutumia lugha chafu yalitupiliwa mbali na Mahakama kutokana na upande wa mlalamikaji kushindwa kuthibitisha.

Kwa upande wa mlalamikaji ambao ulikuwa na mashahidi wawili ambaye ni pamoja na Katibu Muhtasi wa Msimamizi huyo, Bibi Alice Mugomba na Msimamizi wa Uchaguzi huo, Bw. Fissoo. Mlalamikiwa alikuwa na mashahidi wanne.

Akitoa utetezi mahakamani hapo, Bw. Lwakatare alikana kutamka maneno hayo na kwamba siku ya kutangaza matokeo alifika na kuingia ndani na kumwambia Msimamizi kwamba utaratibu aliotumia kutangaza matokeo, ni kinyume na alimwomba asitangaze matokeo kwani katika nchi zingine husababisha rabsha na watu kuingia mstuni.

Alitaja nchi kama hizo ambazo watu wake wameingia msituni kuwa ni pamoja na Uganda, Kodivaa, Serbia na Morisi katika mazingira kama hayo.

Hata hivyo, kwa upande wa utetezi wa mlalamikiwa ambaye alikuwa akitetewa na Wakili wa kijitegemea, Bw. Twaha Taslima, aliiomba Mahakama kutupilia mbali ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kwa upande wa mlalamikaji kwa madai kuwa mashahidi wote walikuwa na uhusiano wa kikazi.

Alidai kuwa Katibu Muhtasi wa Msimamizi huyo, angeweza kuamriwa na bosi wake kusema atakavyo.

Hata hivyo, katika hilo, hata Mahakama pia iliangalia upande wa mashahidi wa mshitakiwa ambapo mashahidi wake wawili walikuwa na uhusiano wa kikazi na mshitakiwa huyo.

Mashahidi hao walibainishwa na Mahakama hiyo, kuwa ni pamoja na mashahidi wawili, Bw. Henry Mambo, ambaye wakati wa uchaguzi huo alikuwa ni wakala wa Bw. Lwakatare na shahidi namba tatu Bw. Ignatius Robozi alikuwa mshauri wa mshitakiwa huyo.

Hivyo, kutokana na kigezo hicho, Makahama iliamua kutotupilia mbali ombi la wakili wa Bw. Lwakatare la kutaka mashahidi hao watupiliwe mbali kutokana na kila upande kuwa na mashahidi wenye uhusiano kikazi.

Pamoja na hayo, kabla ya kutiwa hatiani, Bw. Taslima aliwasilisha maelezo yake juu ya mteja wake, ambapo aliiomba Mahakama kutoa adhabu ndogo kwa mteja wake kutokana na mshitakiwa huyo, hana rekodi ya kutenda kosa na kwamba ana familia ya watoto wanne, wadogo na mke ambao wote wanamtegemea.

Pia alisema ana watoto wanne wa marehemu kaka zake ambao wanamtegemea na kwamba akipewa adhabu kwa kipindi kirefu itawaondosha watoto hao nyumbani kwake.

Hali kadhalika alibainisha kuwa mshitakiwa huyo anasumbuliwa na kisukari ka kipindi kirefu tangu mwaka 1997 amekuwa chini ya uangalizi wa daktari.

Pia, Bw. Taslima aliiomba Mahakama kuangalia nyadhifa alizonazo mshitakiwa katika jamii na Taifa kwa ujumla, kwamba ana madaraka makubwa taifani, akiwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, kutokana na hilo yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini na kutokana na hilo, kumwondoa kwa muda mrefu katika jamii, itakuwa ni kuinyima nchi nzima mchango wake wa maendeleo ya Taifa.

Pia kutampunguzia kasi ya ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini na kwamba akiondolewa kwenye uhuru alionao kwa sasa mchango wake pia utaondolewa katika jamii ya Watanzania.

Mahakama ilizingatia maelezo ya wakili huyo na kutupilia mbali maelezo yake juu ya nyadhifa alizonazo taifani na hivyo kumtia hatiani kutumikia kifungo cha nje cha miezi 15 bila kutenda kosa lolote kwa kipindi hicho kuanzia jana hukumu hiyo ilipotolewa.

Akimtia hatiani, Hakimu Mashauri alisema pamoja na madai ya Lwakatare kuwa msimamizi wa uchaguzi kutangaza matokeo, wakati yeye hakuwapo hata kumfanya achukie na kutamka nchi ambazo zimeweza kuingia mstuni kutokana na hali hiyo, si kwamba Bw. Lwakatare alikuwa anamtishia msimaizi wa uchaguzi Mkuu wa Uchaguzi wa Bukoba Mjini bali pia alitishia usalama wa Taifa, pamoja na kuwapo machafuko katika nchi alizozitaja, lakini bado zinagharimu roho za watu wa nchi hizo.

Hivyo, Mahakama ilimtia hatiani kwa kutumikia ifungo cha miezi 15 nje, na kwa kipindi hicho hatakiwi kutenda kosa lolote.

Hii ni mara ya pili mwanasiasa huyo kufikishwa mahakamani, kwani Oktoba 17 mwaka huu, Mahakama ya Wilaya ya Bukoba, ilimwachia huru, baada ya kukabiliwa na mashitaka ya kumpiga mwandishi wa habari, Bw. Renatus Mutabuzi wa ITV.
 
Kwa maana hiyu Mhe hataruhusiwa kugomeba Ubunge wa Urais wa Tanzania milele (well, mpaka hapo katiba itakapobadilishwa vinginevyo). Si ndio maana yake?
 
Mbona mwamlaumu Mkiji, wakati ni kweli majira wameandika? ama majira ni waongo/wanaturusha roho?

Hata hivo hii ni kesi tofauti na ile aliyo kwisha hukumiwa kifungo kingine cha nje, ile ilikuwa juu ya mwandishi wa habari, na hii ni juu ya msimamizi wa uchaguzi!

Hata hivo ni kumshukuru Mungu kwamba anapewa vifungo vya nje!
 
Amehukumiwa kifungo cha miezi 15 na akifanya kosa lolote wakati huu ataenda kukitumikia jela; sasa hivi yuko nje.
 
Amehukumiwa kifungo cha miezi 15 na akifanya kosa lolote wakati huu ataenda kukitumikia jela; sasa hivi yuko nje.

Tungo tata hizi!
sijui kuna ugumu gani kusema Lwakatare kahukumiwa kifungo cha nje kwa muda wa miezi 15tokea hapo awali. Mpaka watu wapoteze a lot of brain cycles kufikiri kitu ambacho kimewekwa katika utata.

We need to be objective as well as serious sometimes
just an opinion!
 
Gamba la Nyoka sawa; ndiyo maana nilisema "more info to come" kwa sababu wakati mwingine huwa tunatonywa habari wakati zinatokea so we don't have all the detail.. ningekuwa na uwezo wa kuedit mimi mwenyewe ningeedit hapa.. kwa sababu sasa ninafahamu what happened..
 
Mwanakijiji habari nyeti kama hizi inabidi uwe makini namna ya kuziweka hapa, kwa kuwa kichwa cha habari na maelezo yako mafupi yamechanganya watu 'especially' pale tunapogundua kuwa kifungo sio kile cha ndani.

Staili hiyo inatumiwa sana na watu wa magazeti ili wauze. Nitatoa mfano, unakuta title imeandikwa kwamba


RAIS AFUMANIWA NA MKE WA WAZIRI

Habari zaidi ukurasa wa kumi

- page 10 -
Rais wa chama cha wakulima wa kijiji cha xxxxxx kilichoko katika mbuga ya yyyyy amefumaniwa na aliyekuwa mke wa waziri wa serkali ya wanafunzi wa chuo cha uselemala kijijini zzzzz

Can you imagine!!!
 
To be technical ni kweli amefungwa kifungo cha miezi 15. Hapa hakuna utata. Atatumikiaje kifungo hicho ndipo imejulikana baadaye..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom