Lusinde (CCM-Mtera) apendekeza watwangane kwanza Bungeni

Kwa mara ya kwanza nimeshuhudia kioja katika ufunguzi wa bunge , leo jioni pale mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde maarufu kama Bajaji aliyeangusha Katapila (malecela),
Kasema mambo ya kushangaza yafuatayo:-
1.Baadhi ya wanasiasa wanapotosha umma kwa kusema kwamba Polisi na Serikali wanapiga wananchi mabomu.. ( hapa alikuwa akimaanisha CHADEMA na tukio la Arusha)… akasema kwamba yale sio mabomu bali bi gesi lakini wanasiasa wanapotosha umma kwa makusudi, mabomu ni yale yaliyolipuka pale Mbagala na sio yanayotumiwa na polisi
2. Kampongeza Edward Lowassa kwa kujihudhuru kutoka na uzembe uliofanywa na watendaji wa chini yake katika suala la Dowans na akazidi kusema kuna watu wengine ni wagumu kujihudhuru hata kaika timu zao zinapofanya vibaya na mambo mengine mengine
3.Suala la JK kua mvumilivu kutokana na mambo yanayoendelea , anafikiwa hatua ya kuandikwa vibaya katika vyombo vya habari na kwenye mitandao… akaongeza Hivi najiuliza huyu raisi Kikwete ujeshi wake mbona hauoneshi mbona amekua mpole kiasi hiki na angekua mtu mwingine asingeweza kuvumilia…
Aliongea mengi ambayo hayana maana mbele ya watanzani wanaopigika na maisha ikiwemo gharama za Umeme kua juu, mgao wa umeme, mfumuko wa bei za bidhaa, wanafunzi wa vyuo kikuu kuandamana na kupigana na mapolisi n.k
Note: huyu jamaa nimemuona ni mkurupukaji na anayejipendekeza kwa wakuu wake akitegemea fadhila ya vyeo na madaraka serikalini na CCM, sio mpambanaji wa kweli bali ni mropokaji anayeongea kufurahisha wabunge wenzake wa CCM na anavyoonekena ni mtu anaye danganyika kirahisi, na sio mwakilishi wa kweli pale mjengoni…
Wana JF naomba mmfuatilie vizuri huyu jamaa kila wakati anapoongea halafu baada ya kikao cha bunge kuisha mtaniambia

sidhani kama kweli walimchagua yule jamaa...inawezekana ccm waliamua kumumaliza mzee wa watu baada ya kumtumia na kumchoka!!! anaongea matapishi kwa kweli!!!
 
Kazi tunayo mwaka huu! Kama CCM ina wabunge wa aina hii wengi basi nchi itaendelea kuwa chini ya mafisadi kwa miaka mitano
 
Kazi tunayo mwaka huu! Kama CCM ina wabunge wa aina hii wengi basi nchi itaendelea kuwa chini ya mafisadi kwa miaka mitano

kazi iliyobaki ni kufanya mazpinduzi kwa kutumia nguvu ya umma tu!!! tuungane tuweke mikakati!!!!!!
 
hawa c ndio wale wabunge makuwadi wa EL. Walikuwa 123, wameingia bungeni 61
 
Nawaonea huruma wananchi wa mtera na nyuma zao za udongo na nyasi zilizoshindiliwa na udongo. Ni bora wangemwacha mzee malecela aendelee kuwa mbunge wao kuliko huyu *****... Hivi hawa jamaa wanaenda bungeni kuwakilisha wananchi wao au kuwakilisha serikali!!!??? Nadhani bado hawajui wajibu wao kama wabunge na wanaenda sababu hawana njia nyingine ya kupata kipato kizuri zaidi ya ubunge...

***** lusinde mtera ndio chanzo cha umeme lakini umeme unapatikana pale mtera tanesco station tu, chipogoro, champipuru etc kote ni giza na hazizidi hata kilomita 30 toka power station but kwako sio issue!!??

Shame on you...
 
Mbunge Lusinde wa Mtera anasema anaomba wabunge watangwane bungeni ili madhara ya vurugu yaonekane na isiwe watu kuwatumia wananchi kuwatuma wapigane ili kupata umaarufu wakisiasa!!!

Anasema wafunge milango watwangane halaf ndio watoke nje...kazi kwelikweli!!!

Napendekeza kutokana na hoja ya huyu mheshimiwa moja ya sifa za kuwa mbunge sasa itakuwa lazima mtu awe amepitia self defence. Hawa ndio wa wakilishi wa chama kikongwe na tunachokitegemea kitupe muongozo wa nchi, kazi kwelikweli. Mtu anajipendekeza kwa mtu mpaka anamuona mnafiki na kumdharau.
 
Kwa mara ya kwanza nimeshuhudia kioja katika ufunguzi wa bunge , leo jioni pale mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde maarufu kama Bajaji aliyeangusha Katapila (malecela),
Kasema mambo ya kushangaza yafuatayo:-
1.Baadhi ya wanasiasa wanapotosha umma kwa kusema kwamba Polisi na Serikali wanapiga wananchi mabomu.. ( hapa alikuwa akimaanisha CHADEMA na tukio la Arusha)… akasema kwamba yale sio mabomu bali bi gesi lakini wanasiasa wanapotosha umma kwa makusudi, mabomu ni yale yaliyolipuka pale Mbagala na sio yanayotumiwa na polisi
2. Kampongeza Edward Lowassa kwa kujihudhuru kutoka na uzembe uliofanywa na watendaji wa chini yake katika suala la Dowans na akazidi kusema kuna watu wengine ni wagumu kujihudhuru hata kaika timu zao zinapofanya vibaya na mambo mengine mengine
3.Suala la JK kua mvumilivu kutokana na mambo yanayoendelea , anafikiwa hatua ya kuandikwa vibaya katika vyombo vya habari na kwenye mitandao… akaongeza Hivi najiuliza huyu raisi Kikwete ujeshi wake mbona hauoneshi mbona amekua mpole kiasi hiki na angekua mtu mwingine asingeweza kuvumilia…
Aliongea mengi ambayo hayana maana mbele ya watanzani wanaopigika na maisha ikiwemo gharama za Umeme kua juu, mgao wa umeme, mfumuko wa bei za bidhaa, wanafunzi wa vyuo kikuu kuandamana na kupigana na mapolisi n.k
Note: huyu jamaa nimemuona ni mkurupukaji na anayejipendekeza kwa wakuu wake akitegemea fadhila ya vyeo na madaraka serikalini na CCM, sio mpambanaji wa kweli bali ni mropokaji anayeongea kufurahisha wabunge wenzake wa CCM na anavyoonekena ni mtu anaye danganyika kirahisi, na sio mwakilishi wa kweli pale mjengoni…
Wana JF naomba mmfuatilie vizuri huyu jamaa kila wakati anapoongea halafu baada ya kikao cha bunge kuisha mtaniambia

ulitegemea la ziada kutoka kwa mhitimu wa darasa la saba.... hapo bado yule wa Sumbawanga hajaongea na Lakairo....
 
Haya Mbunge wa darasa la saba huyo... sasa watanzania tumemchague tunatarajia awe na upeo kuliko darasa la saba la UPE? Waingereza wanamsemo, Nguruwe ni nguruwe tu hata umpake vipi lipstik atabaki nguruwe tu!
 
Nashangaa Mh. Spika Mama Makinda kwa nini hakutoa adhabu kwa huyu Mbunge wa CCM Bw. Lusinde!

Hivi kanuni za bunge zinasemaje kuhusu matamshi ya namna hii bungeni?
 
Cdm nawashauri wasimamishe mgombea jimbo la mtera mwk 2015 kwan watu hawampendi, mara nyingi ccm huwanunua wagombea wa ubunge ili wasigombee. Mm ni mkazi wa huko, hata anadaiwa kuwa malecela alikuwa ananunua wagombea wengne na kujitoa ktk hatua za mwisho? Ccm hata dodoma wamewachoka, mm napita
 
Jamani jamani!! Mkamateni huyo kiazi mumpeleke hapo Milembe akatibiwe maana inaonesha akiwahiwa anaweza kupona.
 
Kule kwetu jimbo la Mbozi East tunaye mdai posho Zambi G. Hata hajuwi kama kwenye tarafa yake ya Igamba kuna mgodi wa makaa ya mawe maana hata hajawahi kukaa angalau na wananchi wanaouzunguka mgodi wajuwe wanafurusa gani za kuwasaidia kutokana na kuwepo kwa ule mgodi. Weupe wanaishia kubeba mchanga na kutokomea nao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom