Lumumba hapakaliki, CCM kwafukuta

Lumumba hapakaliki, CCM kwafukuta

CCM INAHITAJI REFORMATION IKIBIDI IZALIWE UPYA!
PRES.MAGUFURI REFORM THIS PARTY ONCE AGAIN!
ii
 
Ahaaa,kumbe kuna double standards siyo.Waliruhusiwa watuibie ili watetee uovu.Inauma.Chini ya Comrade hakuna double standards.Ni lazima majipu yatumbuliwe kote.Kama CCM iliwaibia wananchi ili ijenge msingi wa mafisadi wadogo kuwalinda mafisadi wakubwa lazima tujue.Uovu wote utadhihirika.Tulisema ipo siku,hiyo siku imefika.Lazima Lumumba mtuambie walipo Ndovu wetu na Twiga wetu.
Watu wametishwa. Watu wametishika. Makada watakosa za watoto ada. Kujenga kutasimama. Miradi itapigwa radi na kuishia kuwa ahadi. Chama kina utawala wake. Chama kina Mwenyekiti wake. Si huyo Rais wa Tanzania. Kwanini majipu ya chamani nayo yapaniwe kutumbuliwa?

Tumepata taarifa, isiyo na ya kuvutia sifa,kuwa jamaa anataka kupewa nafasi ajinafasi kuyatumbua majipu ya chamani. Lakini, ameombwa asubiri wakati wake ufike. Makada wanakipenda chama kwa 'maslahi yanayoleta uhai'. Yakikaushwa ghafla,hapatatosha. Lakini, Ofisi Ndogo za CCM Lumumba hapakaliki. Hakuna raha ila karaha kusubiri pigo la ghafla.

Makada nchi nzima wanamuunga mkono Rais kutumbua majipu pengine lakini si chamani. Chamani kunafukuta kwa hofu ya 'bifu' kuporwa mnofu. Makada wanatumikia chama na wao wenyewe. Wanatamani wale waminywe na wao wasiguswe ili wasisuse. Hawataki sera ile ifike humu chamani.

Serikalini sawa, chamani si sawa. Double standards!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Tetesi zinadokeza kwamba jengo la ofisi ndogo lumumba kurejeshwa kwa wananchi ili lifanywe machinga complex ( maana liko sehemu nzuri ya biashara ) kazi ipo .
 
Tetesi zinadokeza kwamba jengo la ofisi ndogo lumumba kurejeshwa kwa wananchi ili lifanywe machinga complex ( maana liko sehemu nzuri ya biashara ) kazi ipo .
unaleta utani. jengo linamilikiwa ki halali
 
Hadi sasa wanaoisoma namba wengi ni wale aliowateua/kuteuliwa,Kama ataweza kuwanyoosha hao wakubwa na wadogo katika chama basi hakika shaka yangu na ya watanzania waliodhani mfumo utakuwa juu ya rais itaondoka.
imani yetu itaongezeka na hivyo kupata urahisi wa kulitumikia taifa.
 
Natamani sana ile katiba ya Wananchi iliyokuwa na kipengele cha uwepo wa mgombea binafsi ingepita ili Maghufuli agombee pasipo na chama next election. Nadhani Mh.Maghufuli angekuwa hana chama chochote angefanya kazi kwa nguvu zaidi. Kwa namna moja ama nyingine Mheshimiwa atapunguzwa kasi na chama chake tu.
Sisi tupo mtaani tunajionea jinsi wakubwa wa chama wanavyovunja sheria na kuibia serikali ila hakuna anayedhubutu kuwagusa.
Kwa kweli nimetokea kumkubali zaidi Maghufuli kwa mda mfupi japo sikumpigia kura. Na sikumpigia kura maana naichukia sana ccm"
"EWE MWENYEZI MUNGU TUNAKUOMBA UMLINDE RAIS WETU JOHN P MAGUFULI NA HILA ZOTE ZA ADUI SHETANI. UMLINDE NA WABAYA WOTE WANAOTAKA KUMKWAMISHA KATIKA SAFARI YAKE ALIYOIANZA YA KUIJENGA UPYA TANZANIA".

Aaaamen!
 
Hivyo ndivyo vitakavyotumiwa kisiasa,yale majipu mama na sugu hakuna mwenye ubavu wa kuyatumbua.
Huu ndio ukweli na hata DuppyConqueror na wenzie wanayajua yote haya

Mi nataka watumbue lile jipu linalomaliza tembo wetu lile ni likatibu mkuu pale Lumumba,,, hapo nitajua JPM anamaanisha anachosema
 
Wakiona anawazingua sana waropoke tu kwamba "kushinda kwenyewe hukushinda tulikubeba halafu unaleta za kuletwa?"
 
Tutegemee kuona magofu ya majumba mengi sana maana watu walipata fedha za kideal deal tu, sasa mzee kaziba deal mtajiharish......., heri yetu sisi tulisha yazoea!
 
Welcome back JF uchaguzi umeisha ni vichekesho na furaha! Mbavu zangu 'utajua tofautisha shuka na pazia' Hii ndio Tz
 
Piga ua kwa mwendo huu kama utakua endelevu nidhamu miongoni mwa watendaji wa serikali itarudi tuu
 
Sisi Wakwere tuna methali isemayo : kidege che sikiumanyile ulimbo kigwilaga na mabawa gose. Yaani, ndege asiyeujua ulimbo, hunaswa na mabawa yote. Ndege kanaswa, dawa yake ni kuliwa tu!
 
CCM ndo wanaisoma namba!

Nasikia kibao kimegeuka. Waliotegemewa kusoma namba sasa wanasomewa na waliotarajia kushereheka ndio wanazisoma namba kwa ajili yao wenyewe na kuwasomea walengwa! Labda ni mfano wa swala kumgeuzia kibao mama lion!

Ngoja tuendelee kutoa mimacho ili tufurahie sinema ya bure!
 
Tumekuwa tukisheherekea sikukuu ya UHURU wa TANGANYIKA tokea mwaka 1962 lakini Watanganyika na baade Watanzania hawapo huru katika Mambo yafuatayo;
1. Bei ya mazao ya kilimo na madini hatupangi sisi?
2. Bei ya bidhaa za kutoka nje hatupangi sisi?
3. Uhuru wa kutoa maoni umefungwa kwa makufuli?
4. Uhuru wa kuandamana,kujumuika,kujiunga na chama utakacho umewekewa mipaka,
5. Uhuru wa kuwahudumia wafu wetu wa upinzani umefungiwa minyororo?
6. Uhuru wa Viongozi wa Upinzani kuwashukuru wapiga kura wao umepigwa ribiti
7. Uhuru wa vyombo vya habari umewekewa mipaka ya mstari mwekundu,
8. Uhuru wa kukusanya matokeo ya kura zetu umefungwa kwa makufuli,
9. Uhuru wa kuhoji matumizi mabaya ya madaraka kwa Viongozi umegubikwa na vitisho vya vifo,mateso,na kutolewa kucha na meno.
10. Uhuru wetu umegubikwa na ujinga,maradhi na umaskini.
Uko wapi UHURU??..HONGERA JPM!!!
 
Unashangaa mtu anasimamisha nyumba tatu kwa mkupuo mwaka tu zimeisha, ya kwako moja miaka kumi unademadema tu watanyooka tu.
Tutegemee kuona magofu ya majumba mengi sana maana watu walipata fedha za kideal deal tu, sasa mzee kaziba deal mtajiharish......., heri yetu sisi tulisha yazoea!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom