Lumumba hapakaliki, CCM kwafukuta

Lumumba hapakaliki, CCM kwafukuta

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Watu wametishwa. Watu wametishika. Makada watakosa za watoto ada. Kujenga kutasimama. Miradi itapigwa radi na kuishia kuwa ahadi. Chama kina utawala wake. Chama kina Mwenyekiti wake. Si huyo Rais wa Tanzania. Kwanini majipu ya chamani nayo yapaniwe kutumbuliwa?

Tumepata taarifa, isiyo na ya kuvutia sifa,kuwa jamaa anataka kupewa nafasi ajinafasi kuyatumbua majipu ya chamani. Lakini, ameombwa asubiri wakati wake ufike. Makada wanakipenda chama kwa 'maslahi yanayoleta uhai'. Yakikaushwa ghafla,hapatatosha. Lakini, Ofisi Ndogo za CCM Lumumba hapakaliki. Hakuna raha ila karaha kusubiri pigo la ghafla.

Makada nchi nzima wanamuunga mkono Rais kutumbua majipu pengine lakini si chamani. Chamani kunafukuta kwa hofu ya 'bifu' kuporwa mnofu. Makada wanatumikia chama na wao wenyewe. Wanatamani wale waminywe na wao wasiguswe ili wasisuse. Hawataki sera ile ifike humu chamani.

Serikalini sawa, chamani si sawa. Double standards!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Mfano kwenye sherehe za uhuru wakuu wa wilaya na mikoa ulaji wao kwaheri.........chama kwa namna hiu kitakosa watu wa kikitumikia kilitegemea makada wake wawe wanapiga dili
 
Alisema hana uhakika kama sisiemu hakuna wala rushwa....lazima ajiridhishe kuwa hakuna wala rushwa....!
 
Mzee Tupa tupa hili nililitarajia.Na kwa kweli tutarajie mnyukano wa wenyewe kwa wenyewe pindi majipu haya chamani yatakapoanza kutumbuliwa.
 
tumemruhusu tingatinga .... kuna waliokimbia mapema kina lowasa, somaye , kingunge na wengine... waliobaki bora wachomoke kabisa....
 
Lakini, Ofisi Ndogo za CCM Lumumba hapakaliki. Hakuna raha ila karaha kusubiri pigo la ghafla.

Makada nchi nzima wanamuunga mkono Rais kutumbua majipu pengine lakini si chamani. Chamani kunafukuta kwa hofu ya 'bifu' kuporwa mnofu. Makada wanatumikia chama na wao wenyewe. Wanatamani wale waminywe na wao wasiguswe ili wasisuse. Hawataki sera ile ifike humu chamani.

Serikalini sawa, chamani si sawa. Double standards!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Ndoa ndoano?
Mbavu zangu? Yaani Magufuli asipokuwa makini atavunja ndoa ya Chama chake na Sirikali na mwisho wa siku sijui atakuwa mgeni wa Nani?
Ndoa wanajuana waliooana na thamani yake! Wale wakuja na kuingilia ndoa za watu ni kuhatarisha Ndoa za watu na watu watapigana kufa na kupona kulinda ndoa zao.

Watu wametishwa. Watu wametishika. Makada watakosa za watoto ada. Kujenga kutasimama. Miradi itapigwa radi na kuishia kuwa ahadi. Chama kina utawala wake. Chama kina Mwenyekiti wake. Si huyo Rais wa Tanzania. Kwanini majipu ya chamani nayo yapaniwe kutumbuliwa?

Tumepata taarifa, isiyo na ya kuvutia sifa,kuwa jamaa anataka kupewa nafasi ajinafasi kuyatumbua majipu ya chamani. Lakini, ameombwa asubiri wakati wake ufike. Makada wanakipenda chama kwa 'maslahi yanayoleta uhai'. Yakikaushwa ghafla,hapatatosha. Lakini, Ofisi Ndogo za CCM Lumumba hapakaliki. Hakuna raha ila karaha kusubiri pigo la ghafla.

Makada nchi nzima wanamuunga mkono Rais kutumbua majipu pengine lakini si chamani. Chamani kunafukuta kwa hofu ya 'bifu' kuporwa mnofu. Makada wanatumikia chama na wao wenyewe. Wanatamani wale waminywe na wao wasiguswe ili wasisuse. Hawataki sera ile ifike humu chamani.

Serikalini sawa, chamani si sawa. Double standards!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Tenzi mujarabu; hakuna njia ndefu isiyokuwa na mwisho, It Is payback time! Waliimba sana "Wapinzani wataisoma namba" wakiwabeza UKAWA na Lowassa! Sasa hao hao hawaisomi namba Bali WANAIONJA namba! Kiendacho hurudi!
 
Hahaaaaaa hii umehack kwa mafunzo ya Mkorea aliyekuja kugushi matokeo uchaguzi Mkuu? Ccm haipokei order toka Moshi,kila mteuzi ana madaraka yake ya kuongoza. Kama yapo majibu huko Ccm jitayarisheni kuyapokea yaje yatumbuke huko. Wameshaambiwa wanafiki waondoke. Kwa kasi hii ya Magufuli hata haitaji nguvu ya chama sisi wananchi tuko nyuma yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom