Lumumba hapakaliki, CCM kwafukuta

Lumumba hapakaliki, CCM kwafukuta

Magufuli vunja hicho chama...kimelaaniwa na tanzania chini ya ccm haiwezi kubarikiwa...

Chama si kibaya, umewahi soma imani ya ccm? Itafute. Kuna wanachama waovu ndani ya ccm, waondoke na baadhi wameishaondoka. CCM itadumu, itadumu, itadumu.
 
Wenyewe watajuana, sisi tunachotaka serikali tuheshimiane. Hongera sana JPM kama utaona infaa na chamani poa tu , ila kwanza seikalini
 
Tinga tinga has come to soon, worse at the wrong destination. Siko huku Maguu Kulee! Mwaka huu kazi kwa walio zoweya kuvuna kivulini.
 
Read my lips, "Katiba y CCM itafanyiwa marekebisho kwa kusema kwamba Rais wa JMT akiwa katoka CCM hawezi kuwaMwenyekiti wa chama bali atakuwa ni Kiongozi mkuu wa Chama"

Sababu kubwa itakayotolewa ni kuwa Raisi apate muda mzuri wa kufanya majukumu yake kama ni raisi, na Mwenyekiti aweze kutumia muda wake kukiboresha chama.
 
Hujui politics wewe...Wapinzania hawawezi kucheka kwasababu hii process yote kwa ujumla, inaongezea umaarufu CCM...sasahivi imani inaongezeka...hii sio taarifa nzuri kwa chadema & co

imani inaongezeka kwa wananchi ila ndio safar ya kifo cha ccm mana kutakuwa na mgogoro mkubwa nani ya chama kuwahi kutokea ndani ya chama
 
Ndoa ndoano?
Mbavu zangu? Yaani Magufuli asipokuwa makini atavunja ndoa ya Chama chake na Sirikali na mwisho wa siku sijui atakuwa mgeni wa Nani?
Ndoa wanajuana waliooana na thamani yake! Wale wakuja na kuingilia ndoa za watu ni kuhatarisha Ndoa za watu na watu watapigana kufa na kupona kulinda ndoa zao.

Mi naamini ndoa ni kati ya rais
na wananchi waliomchagua na wala si
kati ya rais na chama chake.Ndo maana
hata fedha inayoendesha taasisi inayoitwa rais
zinatoka kwa wananchi wote bila kujali vyama vyao.
 
salute kwako mzee edward lowassa kwa kusababisha CCM wamteue magufuli kuwa mgombea urais.vinginevyo tusinge yashuhudia/sikia haya.mungu ibariki Tanzania,mungu mbariki Edward lowassa.

Umenena ukweli kabisa coz ninachokumbuka baada ya EL Kukatwa team el waliungana na kuhakikisha wanamteua magufuli na kumzika mzima membe
 
Kuna jambo huwa linanikasirisha mimi. Ukimualika kiongozi kwenye shughuli mf kuwa mgeni rasmi lazima umpe bahasha(pesa).
Hii nayo ni kero kwelikweli.... Hotuba yenyewe unamuandalia halafu unampa posho wakati ipo ndani ya majukumu yake.
 
Ni lazima asafishe chama, wasio penda wanfate Lowassa na Mbowe. CCM lazima itakaswe
 
imani inaongezeka kwa wananchi ila ndio safar ya kifo cha ccm mana kutakuwa na mgogoro mkubwa nani ya chama kuwahi kutokea ndani ya chama
Wacha kujidanganya mkuu..chama kinaimarika...activities za Magufuli zinatetemesha!
Kama ccm haikuanguka wakat wa uchaguzi 2015, kamwe hakiwezi kuanguka- E Lowassa
 
Kwa kufafanua ni kwamba wanaoisoma namba ni team Lowassa ndani ya CCM ambao walitegemea awe rais kwa tiketi ya CCM akakatwa. Walitegemea apate kwa UKAWA akakatwa tena. Laiti angepata tungeona wakihama toka CCM kwa wingi wao kumfuata bosi wa mtandao, EL. Waliasisi MFUMO uliokichafua chama cha ccm. Hao ndo walikuwa wakiimba pale Dodoma- tuna imani na Lowassa. Hao ndo JPM aliwasema mchana ccm, usiku UKAWA. Hao ndo wanaisoma namba T2015JPM. Wengine sisi roho kwatuuu. CCM mbele kwa mbele.

Nimekupenda bila mate. ....sorry

Hivi katika kura za maoni ni team gani ilimpigia kura magufuli???????
 
Wacha kujidanganya mkuu..chama kinaimarika...activities za Magufuli zinatetemesha!
Kama ccm haikuanguka wakat wa uchaguzi 2015, kamwe hakiwezi kuanguka- E Lowassa

Nimekuwa outdated sana siku hizi,hilo alilisemea wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom