Lumumba, Dar: Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM imetoa siku 7 kwa Kamati yake ndogo kuwasilisha taarifa ya mahojiano ya Membe, Makamba na Kinana

Kile chama kikuu cha upinzani kinachosubiria mgombea wa urais kinafuatilia kwa makini juu ya maamuzi yatakayofikiwa kuwahusu wale " Wana wa ngurumo"

Kiuhakika kama Membe atavumiliwa na kuendelea kubakia CCM basi litakuwa pigo kubwa sana kwa Chadema.

Kiukweli tunayasubiri kwa hamu kubwa maamuzi ya kihistoria ya chama chetu.

Maendeleo hayana vyama!
Psychiatric minded

In God we Trust
 
Wewe unazeekea hapo lumumba, rudi kwenu Mwandiga ukalime mawese, ukavue migebuka na utengeneze kayoga
Chuki yako haita kufikisha popote
Na utaugua kiugulia bure
Makonda yupo leo Mpaka Kesho

In God we Trust
 
Hivi vikao vya chama ilitakiwa vifanyike Weekend au siku zisizo za kazi kwa kuwa Watendaji Wakuu wa chama ni watumishi wa Umma na wanalipwa mishahara na serikali.
 
Nikiangalia picha na mavazi waliyovaa hawa wajumbe wa Chama chetu kitukufu, napata picha kwamba kadri unavyochanganya chanyanya rangi za mashati yetu ndiyo hiyo hiyo picha ya jinsi ulivyo kichanganya changanya chama chetu. wengi wanaopenda kuvaa mashati ya rangi moja yaani kijani tupu na nyeusi au njano tupu na nyeusi naona ndiyo wenye dhamira ya dhati na chama.

ILA hawa wanaotuchanganyia rangi ili wapendeze mara zote hawana uchungu na Chama.

Maana kadri mtu alivyochanganya rangi ndivyo alivyo au anavyokichanganya chama.


Sijui wenzangu.

Ila ni mtazamo wangu.

Ni kujikumbusha kidogo saikolojia kidogo ya rangi ya mavazi
 
Back
Top Bottom